Magufuli angekuwepo sio tu vitu vingepanda bei, vingeadimika kabisa

Magufuli angekuwepo sio tu vitu vingepanda bei, vingeadimika kabisa

Nonsense,😎
😁😁😁😁 Nonsense kwa sababu nimekuelza ukweli na wapuuzi ndio mkawadanganye..

Ni Jiwe ndio aliwaambia watu kwamba wajenge viwanda vyao ilinwauze bidhaa bei ya chini hapo ni baada ya Bei za bidhaa hasa za ujenzi kuanza kupanda..

Ni Jiwe ndio aliwaambia watu kama wanaona chakula kimepanda.bei nao wakalime akisisitiza kufa kufaana na hapo ni 2019 mafuta ya kula yalipanza kupanda bei..

Jiwe alipoambiwa vyuma vimekaza alikuwa anasingizia wapiga dili wakati Uchumi unaanguka..

Kwa hiyo Jiwe angekuwepo saizi uchumi ungekuwa very worse na angezidi kuwa katili Ili kujihami na kuficha udhaifu wake kama tuu alivyokuwa analeta Takwimu za uongo..
 
Na tozo watu wangelipa na hakuna wa kunyanyua mdomo..

Ujue mkiwa na Rais mwenye kiburi huwa ni disaster,imagine ndani ya miaka yake 5 mafuta ya magari yaliwahi adimika mara 2,sukari mara 2 na saruji mara 1 na hakukuwa na balaa kama za Uongozi wa Sasa..

Mwendazake angekuwepo Hali ingekuwa mbaya na angekuwa katili zaidi akiogopa kupinduliwa.
Sio wangelipa walikua wanalipa tayari, alianza na tozo ya sh100 kwenye mafuta ikamnogea mwaka uliofuata ikawa sh200 na watu hawakulalamika sababu ya kuogopa wasiojulikana,

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
 
Wakuu, kwema

Kama mnavojua kuna inflation kubwa kila nchi duniani nimeweka screenshot chache kuonyesha hilo.

Sasa watu wasioelewa wanasema inflation imesababishwa na Samia na Magufuli angekuwepo bidhaa zingekuwa chini sana

Kanuni ya msingi kabisa kwenye uchumi ni kuwa bei za vitu zinakuwa determined na demand vs supply au uhitaji vs upatikanaji.

So uhitaji wa bidhaa fulani ukiwa mkubwa ila upatikanaji wake ukawa mdogo lazima hiyo bidhaa itapanda tu bei hata rais angekuwa nani

Mfano mavuno ya mahindi mwaka huu yamekuwa kidogo kutokana na ukame lakini uhitaji wa mahindi ni mkubwa, so matokeo yake lazima ni bei ya mahindi kupanda, simple as that

Sasa hebu tuangalie historia ya Magufuli katika ku deal na matatizo ya kiuchumi yalivyokuwa na tutajua kama angeleta unafuu katika hali ya sasa au ndio angeogeza balaa

Sakata la sukari: Kama mnavyokumbuka mwaka 2016 Magufuli kwa papara alipiga marufuku sukari kutoka nje ya nchi, matokeo yake ni sukari kuwa adimu hence bei yake kupanda, ila cha ajabu kwa uelewa mdogo wa Magufuli, alianza kusema wafanyabishara ndio wanafanya hujuma kupandisha sukari na akaagiza sukari kusakwa na jeshi, matokeo yake sukari ikapanda zaidi.

Sakata la korosho: Kuna muda korosho zilinunuliwa kwa bei nzuri sana huko Mtwara, watu wakafaidi, hii ni kwa sababu bei katika soko la dunia ilikuwa nzuri, so hata wafanyabishara watanunua kwa bei nzuri kutoka kwa wakulima, ila misimu uliofuata bei ikashuka, kwenye soko la dunia, so hata wafanyabishara nao wakatoa bei ndogo huku, Magufuli kwa akili zake pia akasema ni wafanyabishara wanamhujumu, akaagiza jeshi kununua korosho wazibangue hata kwa mabomu, matokeo yake ni korosho zile zilishindikana kubanguliwa na zikawa zinaozea kwenye maghala na watu wengi waliporwa korosho zao bila kulipwa.

Sasa kwa mifano hiyo michache tu inaonyesha jinsi gani Magufuli alivyokuwa akifanya vitu kwa impulse, (kwa hasira bila kufikiri)

huyo mtu angekuwa rais kipindi hiki ambacho dunia ina struggle na inflation unajua angefanya situation kuwa mbaya zaidi, pengine angeagiza jeshi lifanye biashara ya mafuta ili yashuke bei.

View attachment 2369424View attachment 2369425
screenshot_20220721-072018-png.2369426
Una elimu gani?!
Umeajiliwa au umejiajili?!
Milembe una vyeti vingapi?!
Bado unaishi nyumbani ehh?!
Em kaongee na mama ako muulize wanapata vp pesa ya chakula hapo ndani?!
 
Tunamuongelea hadi Hitler itakuwa huyo dictator uchwara wa juzi?
Hitler haongelewi kama JPM, JPM anawatesa sana nyie walamba asali.

Kuna mda mnatamni mbomoe hata daraj ala Ubungo/Ubungo fly over.
 
Huwa nikikumbuka sakata la sukari na korosho hakika dhalimu alikuwa na maamuzi ya hovyo Sana ila ndo rais aliye pendwa na masikini wengi kwa jina la rais wa wanyonge
Huwa nafurahi sana ninapoona mnamsema jinsi alivyokuwa mweupe kichwani. Kaharibu sana nchi yetu.

Rais wa hovyo kuwahi tokea ulimwenguni
 
Naongezea Mama mbali ya mzigo mkubwa miradi mikubwa na kimkakati aliyo ridhi kapambana kupata mikopo nafuu na wahisani huko duniani kwa diplomasia ya uchumi.

JPM mbali ya kumaliza kukamua akiba mfano mifuko hifadhi na Watanzania wengine Hadi kufikisika na mauti, alinza kukopa mikopo ya kibiashara kwa riba kubwa!

Angefanya Nini kwa mtetemo huu uliokumba Dunia?

Tumshukuru Mola kwa yote.
Alikuwa rais wa hovyo mpuuzi kuwahi kutokea kwenye USO wa dunia
 
Vitu vingeadimika na Watu wakilalamika wangeendelea kubambikiwa kesi na kupotezwa.

Ole Sabaya na wenzake wangeemdelea kuharass Wafanyabiashara wa Kilimanjaro na Arusha na hueda angepewa ukuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Maiti na mizoga ya Wananchi ingekuwa imetapakaa kwenye kila Mito na Misitu.
 
Mfumo imara! Hupi?
"Kwa kuwa sisi Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya Uhuru,haki,udugu na amani" kipengele cha kwanza katika Utangulizi wa Misingi ya Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.
 
"Kwa kuwa sisi Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya Uhuru,haki,udugu na amani" kipengele cha kwanza katika Utangulizi wa Misingi ya Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.
Umesikia yaliyotokea Mara? umesikia aliyokutanayo Catherine Ruge? ndicho unacho kizungumzia au?
 
Hata wewe watakutafuna tu wakati wako ukifika hakuna ujanja kwa hilo Acha viroja
Mimi siyo muaji,mimi sikandamizi watu,mimi sibagui watu,mimi nathamini kila Mtanzania awe ccm ni ndugu yangu,awe chadema ni ndugu yangu,awe ACT ni ndugu yangu,awe tlp ni ndugu yangu,awe chauma ni ndugu yangu,awe wa rangi gani ni Mtanzania kwa hiyo sikuwahi mchukia au kumwonea mtu yeyote kwa matakwa yangu hivyo basi nitakufa kama wanadamu wengine wafaavyo ila siyo kifo cha dharau kama cha
Umesikia yaliyotokea Mara? umesikia aliyokutanayo Catherine Ruge? ndicho unacho kizungumzia au?
Hayo hawezi kuisha ila baraka za kipumbavu za Tembeeni kifua mbele nitawalinda hazipo tena.
 
Back
Top Bottom