Huyu Magufuli naanza kuona licha ya kutawala kwa muda mfupi, lakini anaonekana ndie ataongoza kutawala vichwa vya wengi zaidi ya marais waliopita.
Ukiuliza kwanini anasemwa hivi, utajibiwa lazima asemwe kwa mabaya yake, naona wajinga siku hizi wanajificha kwenye kivuli cha ubaya wa Magufuli, ili wao waonekane/wajione watakatifu, huku ni kujidanganya tu.
Magufuli hakuwa malaika, lazima kama mwanadamu wa kawaida alikuwa na mazuri na mabaya yake, lakini kwa baadhi hili hawalioni, wao kwao Magufuli alikuwa ni shetani tu, this is insanity & mental slavery.
Nikitizama vizuri hoja za mleta mada, naona ameamua kulaumu kwa kujua/kutojua, ili aendeleze tu kasumba ya kumsema vibaya Magufuli.
Mfano, anazungumzia sakata la sukari 2016 lililosababisha bei ya bidhaa kupanda, analaumu uamuzi wa Magufuli kuzuia uagizwaji wa sukari toka nje, kwamba huo ndio ulisababisha bei ya sukari kupanda.
Kwangu haya ni mawazo ya mtu anayefikiria kwa upande mmoja tu, tena negatively; kwasababu kama angeamua kufikiria positively ule uamuzi wa Magufuli kuzuia sukari toka nje, naamini angepata jibu zuri tu, kwamba alikuwa ana promote viwanda vyetu vya ndani, na kukuza ajira.