Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Duh huu mwaka utakua na mitumbuo mingi sana.. Ngoja tusubiri ila hii ya Tanesco ilikua kwenye target tangu wakati wa kampeni basi tu jamaa hakuinamisha kichwa kupisha kimbunga, hatimae kimemzoa.
 
Nadhani jpm hakuiangalia ile mechi ya simba na yanga. Lazima angemtumbua refarii
 
Kwa mwendo huu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitachuja.
Wataalam wote wakongwe wanateuliwa [emoji30] [emoji30]

Kata mti panda mti pale taasisi ya kuzalisha wataalamu
 
Huoni kama serikali ya awamu ya 5 kuna tatizo la flow of information kati ya watendaji wa serikali hasa wakurugenzi wa mashirika na mawaziri/Raisi

Angalia hii mifano
1.Waziri wa afya vs NIMR -Hakuna Zika/Zika ipo
2.Waziri wa afya vs MSD-Akiba ya dawa chanjo imeisha/Hakuna upungufu wa dawa/chanjo
3.Raisi vs Hazina/BOT-TRA wamefungua FDA ili wachukue interest/kufungua FDA sio tatizo
4.RCs vs Raisi-Machinga/wachimbaji wadogo waondolewe/Wamachinga na wachimbaji wadogo wasiondolewe

Iko migongano mingi ikiwemo ya kuongeza na kushusha GPA kwa admission vyuoni,Kuteuliwa kwa boss NSSF akatenguliwa baada ya siku moja.Huu ni mwaka wa 2 watendaji wa Raisi bado wanatofautiana.Kuna kipindi naona uamuzi wa JK kuwapeleka watendaji wake semina elekezi Ngurdoto ulikuwa uamuzi mzuri sana
 
Rais Magufuli na Buhari watajwa kama marais walioangusha matumaini ya wananchi::

Wakitoa tathimini ya mwaka 2016 kuelekea mwaka 2017, Redio ya idhaa ya kiswahili ya ujerumani DW wamewataja marais John Pombe Magufuli wa Tanzania na Buhari wa Nigeria kuwa ni marais walioangusha matumaini ya wananchi wao hasa vijana na ikizingatiwa kuwa ni marais walioingia kwa mbwembwe nyingi na kutoa matumaini mapya ya mafanikio.

Wakimzungumzia Rais Magufuli, walisema wanachi wengi walitegemea hali zao za uchumi zikiimarika lakini badala yake wamejikuta katika hali ngumu zaidi, huku vijana wakikata tamaa pale wanapowaona watangulizi wao wakitopea katika lindi la umasikini wa kutupwa.

Wakizungumzia demokrasia walisema rais ameshindwa kabisa katika nyanja hii, anaiendesha nchi kwa mkono wa chuma, matumizi mabaya ya madaraka na upendeleo, kuwakamata na kuwatia ndani wakosoaji wake, kusitisha taasisi mbalimbali, uhuru wa habari na kujieleza umebinywa na kuwafanya hata viongozi wa dini waliokua wanakosoa pale wanapoona hapaendi sawa ku kaa kimya.

Upande wa elimu, vijana wengi waliokua wanashangilia leo wanalia kwa kuwanyima mikopo watoto wa masikini, ajira hakuna, walimu wanayimwa stahiki zao, ufukuzaji usiofuata sheria na maslai duni. Elimu inayotolewa bure imeshindwa kukidhi matarajio.

Uchumi walisema hali ni mbaya sana, masoko yamedorora, biashara zinafungwa,ajira zinapunguzwa hali ambayo haitii matumaini kwa vijana, kodi kubwa ambazo haziendani na kipato halisi cha biashara.

Walimalizia kwa kusema hali ya matumaini kwa wanachi wa Tanzania imefifia sana na ukataji wa matumaini ni mkubwa sana hivyo inahitajika mabadiliko chanya ya kiuchumi na kisera.

Chanzo : DW
 
Angemwacha mpaka tarehe 2, kumwambia "Heri ya mwaka mpya" utaona kama unamchora!
 
Nimekuelewa sana,hizo ni athari za maamuzi mlipuko
 
Safi sanaa.. Wanadai mapato ya nchi yameongezeka mara dufu alafu wanapandisha bei ya umeme? Nilishangaa sana! Wachukue hizo pesa za kodi wachanganye na gesi iliyotoka mtwara kukava hizo cost za umeme sio kila kitu kuweka mzigo kwa wananchi.. Kama vipi atumbue na huyo wa Ewura aliyehalalisha upandishaji wa bei ya umeme.
 
Mkuu leo ni siku ya tatu ikiwa inanyesha, na leo imenyesha kuanzia saa 7 mchana mpaka saa 11 jioni. Na tena ni mvua ya nguvu.
Daah,hongereni mkuu..
Cc pande za dom hiz,tumezimic saana mvuu..hatuioni
 
Hilo ni kosa? Huyu mtu na maaskofu wake watahukumiwa!
Alicho Fanya JP ndivyo inavyo takiwa walio baki wajihadhari na maamuzi ya kilevi hawajamuelewa magufuli, anacho taka magufuli wewe kama kiongozi kila dakika ubuni mbinu za kumpa faraja mtu wa chini sio kumzidishia mzigo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…