Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

mramba nimependa confidence yako japo kuna jambo umetuangusha raia... why unagawa umeme bure.. kwa watumishi wako halafu unapandishia wananchi maskini bei....

tunapata shida kukutetea.. sababu ya kugawa umeme bure kwa wafanyakazi.wako.ambao wana underperform
 
Hapana, ni team Against Vs President, government na team yake.

Hawa team against wapo wameungana na ndiyo wanakosea katika timing zao katika kutoa taarifa yote ikiwa ni katika kutaka kumharibia raisi na serikali ili awe discredited.

Flow of information ipo njia mbili kulekea Ikulu na kuna aina tatu za haya mawasiliano- yaani kuna downward, upward or horizontally.

Halafu kuna barrier yaani vizuizi na hivi ndivyo raisi anajaribu kuviondoa ili apate kuwa na effective communication na watu walio chini yake au "subordinates".

Ila huwezi kuwa na mtitiriko mzuri wa taarifa kama hakuna nidhamu iwe kwenye timu nzima, vikozi kazi au kamati mbalimbali.

Hivyo raisi ananyoosha hii kitu aondek vizuizi na awe na mawasiliano ya moja kwa moja na wasaidizi wake ambao wataelewa yeye anataka nini.
Maamuzi yanayotolewa yanaonyesha kabisa hakuna mawasiliano kati ya Raisi na watendaji wake Kwa nini Raisi asiwe anafanya vikao na watendaji wake kuwaonyesha/kuwaeleza anachokitaka kuliko kusubiri wanavyokosea na kuwatumbua ?
Unafikiri huu utaratibu wa kuwavizia wanapokosea na kuwatumbua utamsaidia Raisi ?
 
Hivi kosa ndio hilo la kuiomba EWURA ipandishe bei ili kuweza kujiendesha?au kuna mengine?
Mauza uza ya tanesco yoooote huyu jamaa anayajua vizuri, mi nashangaa kamaliza mwaka na JPM. Mwingine ni gavana, bado nashangaa yupo mpaka leo, ama bahati katiba inamlinda.
 
Huyu Mramba akae kimya tu.Anachofanya sasa ni chokochoko.
Waswahili wanasema Chokochoko mchokoe pweza binadamu hatawaweza.
 
Hiyo madhani sio barua rasmi. Haina tarehe, haina saini, haina japo muhuri.

Hii itakuwa imeandikwa bar.
 
Huyu Mramba akae kimya tu.Anachofanya sasa ni chokochoko.
Waswahili wanasema Chokochoko mchokoe pweza binadamu hatawaweza.
Uwoga nao ugonjwa!! watumbuliwa wengine wanajikunyata kama vifaranga vya bata!! Bravo Mramba
 
Mkuu huwa nakubaliana sana na mabandiko yako lakini umekosea sana kubeza ubobezi wa Mwinuka kwenye eneo lake umahiri yaani Mech Eng. uliposema mambo ya lathe sijui kitu gani. Wakati mwingine jaribu kuwa na staha kama kitu haufahamu.

Pia huyo Kimambo naye ni Mech Eng japo kaspecialize kwenye energy lakini bado ni Mech. na sidhani kama ana sifa za ziada za kusimamia Tanesco. Mradi wa incubator pale Kibaha ulikufa mikononi mwake sembuse Tanesco ataiweza. Nasema hivi purely on belief kwamba usimjaji mtu kwa alichosoma ila kwa uwezo wake wa utendaji. Wote hawa Kimambo na Mwinuka ni academician na sio watu wenye uzoefu kama CEO's

Kama ni Tanesco ni bora angechukua kabisa mtu wa ECSE au BCom. Penye ukweli tuwe wakweli tuache ushabiki.
Umenena sawa kabisa Mkuu watu wanafikiri eti ukiwa Na Phd au unnaweza kila kitu....jama hawajifunzi Private sector Nchini na hata Duniani zinavyofanya vizuri????? only CVs....not Academician....Au angalia CV za "CEOs roundtables" wana basic degree then uzoefu labda kidogo na Masters....but uzoefu mwingi kwenye eneo lake....kifupi ni amefanya nini kwenye sector husika...
hivi ECSE Ni nini Mkuu??
 
IMG-20170101-WA0055.jpg

Hii hapa ndio format ya barua za tanesco.
 
Duh...... Yaani siku ya kwanza tu ya mwaka 2017, tayari Magu kauanza kwa kutumbua mtu!

Basi tutarajie mwaka huu utakuwa wa utumbuaji wa kutisha zaidi .......
Mh utumbuaji umeanza tangu mwaka Jana kutumbua vijipu uchungu huu Ni mwendelezo
 
Bwana Mramba tayari umepita katika nun-return valve inabidi uendelee tu na process ya waliotumbuliwa. There is no backward motion here!
 
..Duh!!

..yaani kila anayekosoa basi ana chuki.

..huo ni mtizamo hasi sana kuwa nao hasa ukiwa na madaraka.
Kwanini iwe kukosoa tu!!?
Tens upande wa Serikali pekee
Upande wa cdm hujawahi kukosoa zaidi ya kuunga mkono hata kama ni ujinga
 
JF kwanini manalizimasha huu uzi uunganishwa, kama vile nashindwa kuwaelewa
 
Back
Top Bottom