Mkuu, EURA walitakiwa warudishe maombi hayo ya Tanesco mpaka ufafanuzi na makubalino na waziri Muhongo yatakapotokea.
Mramba alipaswa kumshauri waziri (ambae tayari walikuwa hawaivi kutokana na kauli yake kule bungeni kuhusu ufanisi mbovu wa Tanesco)
Hivyo utaratibu ni EWURA kurudisha maombi kwa Tanesco na kuwashauri wamwone waziri ambae ana mamlaka kisheria na kikatiba kuangalia hizo bei ya umeme na kutoa maamuzi ya mwisho.
Mtizamo wako wewe juu la hili ukoje?
Kwanza niseme jambo moja!!
Mimi sina tatizo kwa Mramba kutumbuliwa. Tatizo langu ni kwamba ilikuaje tufike kote huko hadi solution ionekane ni kutumbuana! Hii nchi bado ina uhaba wa qualified personnels... matokeo yake ndo hayo unachomoa Lecturer ili akaongoze shirika!!
Sasa hoja yangu ni kwamba, kulikuwa na sababu gani ya serikali kuacha hili jambo liendelee na hatimae solution yake kuwa kutumbua kwa sababu tu Mramba hakufuata taratibu wakati walikuwa na uwezo wa kulipiga stop prematurely?!
Kwanini tunadhani solution ya matatizo yetu ni kutumbua?
Nikirudi kwenye issue ya EWURA. Walipoletewa ombi na TANESCO kwa mara ya kwanza... ombi lile EWURA walilirudisha TANESCO kwa kigezo cha kuwapo mapungufu! Sehemu ya maelezo ya EWURA ni hii hapa:
Sasa ukiangalia hiyo taarifa hapo juu, ni kwamba EWURA hatimae waliridhika kuhusu maombi hayo ya TANESCO hata kama hivi sasa tunaambiwa hayakufuata utaratibu!!!
Na hapa pia ndipo ninahoji... kwanini serikali hawakuanza na EWURA walio-entertain maombi ambayo hayakufuata taratibu?
Ukiangalia Electricity Act 2008; hivi ndivyo inasema linapokuja suala la EWURA, Serikali na TANESCO:
Ukiangalia hapo, hakuna popote EWURA wanapotakiwa kum-consult Minister of Energy kwa issue ya kushughulikia maombi ya kupanda gharama!! Au labda tunaweza kujenga hoja kwamba hayo yaliyotajwa hapo ni baadhi tu kwavile limetumika neno INCLUDING na kwahiyo miongoni mwa yale ambayo hayatajwa ni hilo la kujadili bei ya umeme!
Kama ndivyo, ina maana kumbe nao walitakiwa kufanya consultation na Waziri! Je, tujiaminishe tu kwamba walim-consult ndo maana wao hawakutumbuliwa na TANESCO ndio hawakufanya hivyo ndio maana wametumbuliwa?!
Kama ndivyo, kumbe nongwa si kwamba serikali walikuwa hawafahamu officially bali ni kwa sababu tu TANESCO kwa upande wao hawakufanya consultation?
Kama ndivyo, kama wewe ndio Kiongozi Mkuu wa Taasisi X na unapata official info toka kwenye taasisi moja ya chini yako juu ya jambo fulani ambalo kiutaratibu unatarajia upate taarifa kama hiyo toka kwa taasisi nyingine mbia wa yule wa kwanza!
Sasa, ina maana hata ukiona siku zinaenda bila kuletewa taarifa na hiyo taasisi nyingine; utaendelea kunyoosha miguu simply because unafahamu at the end utawatumbua kwa sababu tu hawakukupa taarifa?!
Sifahamu uwezo wa Mramba kiutendaji lakini ikiwa we can just fire top executive kwa vitu rahisi kama hivi ili mradi tu kuonesha mamlaka yetu, am sorry to say we know nothing about the importance of human capital!
Aidha, ningependa kumalizia mjadala huu kwa nukuu kutoka kitabu cha Management Bible: