Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Hivi ndg akija mtu mwenye njaa akaleta ombi LA kupewa chakula na wewe ukampa hicho chakula ambacho nilikua cha watoto, Je hapo nani mwenye makosa? Je ni mwenye njaa aliye kuja kuomba au ni yule aliyetoa?

POINT TO NOTE
 
Sioni kosa mtu kutoa proposal! You can reject his proposal and move on! Nambie kosa ni lipi? Anyway, sijui nabishana na mtu wa namna gani education-wise!
Kwanini unafikiri kujua level yangu ya elimu itakusaidia wewe kunijibu hilo swali nililokuuliza?
 
Mkuu, EURA walitakiwa warudishe maombi hayo ya Tanesco mpaka ufafanuzi na makubalino na waziri Muhongo yatakapotokea.

Mramba alipaswa kumshauri waziri (ambae tayari walikuwa hawaivi kutokana na kauli yake kule bungeni kuhusu ufanisi mbovu wa Tanesco)

Hivyo utaratibu ni EWURA kurudisha maombi kwa Tanesco na kuwashauri wamwone waziri ambae ana mamlaka kisheria na kikatiba kuangalia hizo bei ya umeme na kutoa maamuzi ya mwisho.

Mtizamo wako wewe juu la hili ukoje?
Kwanza niseme jambo moja!!

Mimi sina tatizo kwa Mramba kutumbuliwa. Tatizo langu ni kwamba ilikuaje tufike kote huko hadi solution ionekane ni kutumbuana! Hii nchi bado ina uhaba wa qualified personnels... matokeo yake ndo hayo unachomoa Lecturer ili akaongoze shirika!!

Sasa hoja yangu ni kwamba, kulikuwa na sababu gani ya serikali kuacha hili jambo liendelee na hatimae solution yake kuwa kutumbua kwa sababu tu Mramba hakufuata taratibu wakati walikuwa na uwezo wa kulipiga stop prematurely?!

Kwanini tunadhani solution ya matatizo yetu ni kutumbua?

Nikirudi kwenye issue ya EWURA. Walipoletewa ombi na TANESCO kwa mara ya kwanza... ombi lile EWURA walilirudisha TANESCO kwa kigezo cha kuwapo mapungufu! Sehemu ya maelezo ya EWURA ni hii hapa:
EWURA3.png
Sasa ukiangalia hiyo taarifa hapo juu, ni kwamba EWURA hatimae waliridhika kuhusu maombi hayo ya TANESCO hata kama hivi sasa tunaambiwa hayakufuata utaratibu!!!

Na hapa pia ndipo ninahoji... kwanini serikali hawakuanza na EWURA walio-entertain maombi ambayo hayakufuata taratibu?

Ukiangalia Electricity Act 2008; hivi ndivyo inasema linapokuja suala la EWURA, Serikali na TANESCO:
EWURA4.png


Ukiangalia hapo, hakuna popote EWURA wanapotakiwa kum-consult Minister of Energy kwa issue ya kushughulikia maombi ya kupanda gharama!! Au labda tunaweza kujenga hoja kwamba hayo yaliyotajwa hapo ni baadhi tu kwavile limetumika neno INCLUDING na kwahiyo miongoni mwa yale ambayo hayatajwa ni hilo la kujadili bei ya umeme!

Kama ndivyo, ina maana kumbe nao walitakiwa kufanya consultation na Waziri! Je, tujiaminishe tu kwamba walim-consult ndo maana wao hawakutumbuliwa na TANESCO ndio hawakufanya hivyo ndio maana wametumbuliwa?!

Kama ndivyo, kumbe nongwa si kwamba serikali walikuwa hawafahamu officially bali ni kwa sababu tu TANESCO kwa upande wao hawakufanya consultation?

Kama ndivyo, kama wewe ndio Kiongozi Mkuu wa Taasisi X na unapata official info toka kwenye taasisi moja ya chini yako juu ya jambo fulani ambalo kiutaratibu unatarajia upate taarifa kama hiyo toka kwa taasisi nyingine mbia wa yule wa kwanza!

Sasa, ina maana hata ukiona siku zinaenda bila kuletewa taarifa na hiyo taasisi nyingine; utaendelea kunyoosha miguu simply because unafahamu at the end utawatumbua kwa sababu tu hawakukupa taarifa?!

Sifahamu uwezo wa Mramba kiutendaji lakini ikiwa we can just fire top executive kwa vitu rahisi kama hivi ili mradi tu kuonesha mamlaka yetu, am sorry to say we know nothing about the importance of human capital!

Aidha, ningependa kumalizia mjadala huu kwa nukuu kutoka kitabu cha Management Bible:
EWURA5.png
 
Nimekupata mkuu, kama wewe ungekuwa Mangu namfahamu vizuri na ule undugu wake na Tundu Lissu.

Usikute vetting yake imepitia mezani kwangu.

Nimepiga sana biashara za ujasirimali Singida.

JF ni sebule ya majadiliano tuondoe personal issues.

😀😀😀
Tupo pamoja kwa 101%!!!
 
It was staged na sarakasi nyingi na walijua tu watamfukuza. Umeme utapanda bei tuu, si tupo humu JF.

God bless you Injinia
Ndiyo na ww umetumwa uje na hilo aliyekuambia umeme utapanda tu ni nani pumbafu kabisa
 
It was staged na sarakasi nyingi na walijua tu watamfukuza. Umeme utapanda bei tuu, si tupo humu JF.

God bless you Injinia


Kwa hiyo kwa akili yako ulifikiri bei ya Umeme itabakia hivyo ilivyo mpaka siku Yesu anarudi? Kuna watu hawana akili mpaka wanatia kinyaa na cha ajabu zaidi wengi wao wanaishi nchi za watu ndo maana USA wanalalamika IQ yao inashuka shauri ya baadhi ya stupid immigrants!
 
Ila kuna jambo hapa ambalo sijaelewa... naomba wajuvi wanijuze! Hivi unachomoa vipi Mwalimu wa Chuo kuwa Managing Director wa shirika lenye changamoto lukuki?! Hivi PhD inaweza ku-solve changamoto za TANESCO pasipo na kuwa na uelewa kwa mapana na marefu ya changamoto za TANESCO na energy sector kwa ujumla?! Au Mheshimiwa Daktari alitokea private/public commercial sector kabla hajawa Mhadhiri?
Ndo yaleyale ya kuamini Ryoba anaweza kuibadili TBC kwa sababu ya kuwa mwalimu wa waandishi wa habari, leo TBC ni absolute toilet kuliko alivyo Magufuli!
 
Hivi mnafikiri raisi JPM hafahamu mambo yalokuwa yakifanywa na mtandao wa mafisadi katika nchi hii?
Chifu, do you honestly think kwamba Magufuli anapambana na mtandao wa mafisadi? How, kama anasema hawezi kufukua makaburi? Mitandao ya ufisadi karibu yote inahusiana na viongozi waliotangulia katika awamu zilizopita, akiwemo Magufuli mwenyewe!
Kwa mfano katika hili la sasa: kama yupo serious na 'msema kweli' kama anavyojiita, mbona haongelei masuala ya IPTL na Richmond/Dowans/Symbion?

By the way kufahamu siyo hoja. CCM inasifika kwa kufahamu mambo, lakini haiyashughulikii. Aende mbele zaidi ya kufahamu, ashughulikie mitandao kwa kuweka misingi imara ya kisheria na kitaasisi, ambayo itamshughulikia kila kiongozi akiwemo yeye. Je, yupo tayari kwa hilo? Ama yeye anajiona siyo mkosaji?
 
Umemtisha sana chige kwa kueleza kuwa unamfahamu.
Unapokuwa humu jamvini inatakiwa uvumilie yote lugha kali zinatumika sana hasa na wakosoaji, kama hazinjavunja sheria za humu basi hakuna utata.

Hata mimi ni muumini wa lugha kali lakini simvunjii mtu heshima na hakuna ubaya kwenye hilo.

Kwa yanayoendelea sasa serikalini inaonekana wazi lipo tatizo tena kubwa hakuna coordination hata kidogo waziri leo anaeza sema hivi kesho katibu wa wizara akaja na kauli nyingine inayopingana na waziri.

Ni kama ishu ya Dangote mpaka rais anakuja kuingilia lakini tuliskia kauli nyingi zinazopingana kutoka kwa mawaziri.
Hata hili la kupanda kwa bei ya umeme ni hivyohivyo mei naona hii ni michezo tu ya kisiasa tena siasa chafu na hazina tija kwa maendeleo ya taifa.
Ah! Wapi... Mie nazeekea JF ndugu yangu kwahiyo sio rahisi kutishika kwa hoja kama hizo... no way! Hata huyo Richard mwenyewe najua he's just bluffing... hana cha kunijua wala nini!!

Na uzuri mwingine ni kwamba I don't fake my life hapa JF kwahiyo mtu anayenisoma mara kwa mara; siku nikikutana nae akakuta kumbe choka mbaya; wala hawezi kushangaa kwa sababu haijatokea hata mara moja nikajifanya kabosi fulani au msomi fulani hivi!

Na ndio maana hata stori zangu nyingi hapa JF ni za akina Diamond na Ali Kiba... stori za watu wa aina yangu!!! Stori za watu ambao tupo tupo tu... karibu nyumbani Jukwaa la Entertainment & Celebrities
 
Haiitaji kuwa na Phd kujua kuwa umeme utapanda muda mfupi ujao,na Tanesco inaelekea kubaya zaidi ya ilipo.
 
It was staged na sarakasi nyingi na walijua tu watamfukuza. Umeme utapanda bei tuu, si tupo humu JF.

God bless you Injinia
Hata kama utapanda lkn huu si wakati muafaka wakati sahihi ni jambo la muhimu. Nikupe mfano binti akipata mimba nje ya ndoa kwa family nyingi za kitanzania ni tatizo lkn mimba ile ikipatikana ndani ya ndoa ni chereko. Timing ni muhimu pia.
 
Hivi kosa ndio hilo la kuiomba EWURA ipandishe bei ili kuweza kujiendesha?au kuna mengine?
Nionavyo mimi kubadilisha uongozi siyo kutatua tatizo kuna somo linaitwa Crisis management hawa viongozi wetu inabidi wapate training vinginevyo kila kukicha itakua kutumbua
 
Back
Top Bottom