Magufuli hayupo lakini vyama vya Upinzani vinazidi kusahaulika, sasa hawana wa kumsingizia!

Magufuli hayupo lakini vyama vya Upinzani vinazidi kusahaulika, sasa hawana wa kumsingizia!

Nafuatilia kwa karibu ziara ya Katibu mkuu wa CCM Komredi Chongollo akikagua miradi mbalimbali huko Shinyanga

Sijaona benders.ya Chadema.wala ACT wazalendo.kwemye kijiji chochote hii maana yake Upinzani unazidi kudorora kila uchwao

Kumbe siyo kweli Magufuli alikuwa anawabana wapinzani.ila Upinzani wa Tanzania ni lege lege na dhaifu mno.

Mungu ni mwema wakati wote
Wewe mwenyewe Kwa siku unaazisha nyuzi zaidi ya kumi juu ya Chadema,huoni kuwa unajipinga mwenyewe?
 
Kilichobadilika ni nini? Wameruhusiwa mikutano ya hadhara? Ni rahisi sana kubomoa kuliko kujenga. Uharibifu uliosababishwa na awamu ya tano unakaribiana kwa kiasi na mauaji ya kimbari. Ndo maana mnalalamika akisimangwa.Nyie ndo huwa sababu, nimeamini. Ukute hata wewe humpendi ila unaogopa kumtukana wewe moja kwa moja unajidai kuanzisha mada za kuudhi ili Magu atukanwe.
Kama unampenda kweli, uwe mkweli usijidai zuzu kwamba hujui aliharibu kiasi gani ukuaji wa demokrasia. Wape break familia yake kwa kupunguza unafiki wako.
Kwani hata wake wanaomtukana JPM wanampunguzia nini au wanamwongezea nini? Yule ni miongoni mwa watu wachache sana humu duniani ambao kwa aina ya maisha yao watakumbukwa vizazi na vizazi. Ukiachilia mbali kwamba kama ni suala la maisha ya hapa duniani alifanikiwa asilimia 100: kaacha watoto na wajukuu, kaitumikia nchi kwa utumishi uliotukuka ngazi zote (mwalimu, mbunge, waziri hadi RAIS), na pia kaacha falsafa fulani isiyofutika miongoni mwa mamilioni watanzania ya kujiamini na kujitegemea. Kama kuna mtanzania wa ngazi yeyote ile ambaye baada ya Magufuli bado anaamini katika siasa za kujikombakomba kwa watu wa magharibi ili wapate mkate wao wa kila siku, kama bado kuna watu wanaamini kwamba maendeleo ya nchi yataletwa na visiasa fulani hivi vya mrengo wa magharibi vya maneno maneno tu, propaganda fulani hivi zilizojificha kwenye neno "domokrasia" bila umadhubuti wa vitendo on the ground, kama hao wananchi wa style hiyo bado wapo, dah itakuwa ni jambo la kushangaza. Lakini kama bado wapo ukweli ni kwamba kwa Tanzania hii baada ya Magufuli watu hao hawatakuwa na nafasi tena maana wanachi tulio wengi tunawaona wamepitwa na wakati.
 
Back
Top Bottom