Magufuli hayupo lakini vyama vya Upinzani vinazidi kusahaulika, sasa hawana wa kumsingizia!

Wewe mwenyewe Kwa siku unaazisha nyuzi zaidi ya kumi juu ya Chadema,huoni kuwa unajipinga mwenyewe?
 
Kwani hata wake wanaomtukana JPM wanampunguzia nini au wanamwongezea nini? Yule ni miongoni mwa watu wachache sana humu duniani ambao kwa aina ya maisha yao watakumbukwa vizazi na vizazi. Ukiachilia mbali kwamba kama ni suala la maisha ya hapa duniani alifanikiwa asilimia 100: kaacha watoto na wajukuu, kaitumikia nchi kwa utumishi uliotukuka ngazi zote (mwalimu, mbunge, waziri hadi RAIS), na pia kaacha falsafa fulani isiyofutika miongoni mwa mamilioni watanzania ya kujiamini na kujitegemea. Kama kuna mtanzania wa ngazi yeyote ile ambaye baada ya Magufuli bado anaamini katika siasa za kujikombakomba kwa watu wa magharibi ili wapate mkate wao wa kila siku, kama bado kuna watu wanaamini kwamba maendeleo ya nchi yataletwa na visiasa fulani hivi vya mrengo wa magharibi vya maneno maneno tu, propaganda fulani hivi zilizojificha kwenye neno "domokrasia" bila umadhubuti wa vitendo on the ground, kama hao wananchi wa style hiyo bado wapo, dah itakuwa ni jambo la kushangaza. Lakini kama bado wapo ukweli ni kwamba kwa Tanzania hii baada ya Magufuli watu hao hawatakuwa na nafasi tena maana wanachi tulio wengi tunawaona wamepitwa na wakati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…