Magufuli ili TAZARA isife, ongea na China ili iunganishwe na Malawi kupitia Mbeya au Tunduma, na pia ipitie Morogoro na Iringa mjini!

TAZARA haina hali nzuri. Na sababu kubwa ni kwamba utegemezi wa Zambia kwa TAZARA umepungua sana. Kwa sasa Zambia inaweza kupitisha mizigo yao sehemu nyingine zaidi ya Dar es Salaam, kutia ndaniMsumbiji na Afrika Kusini. Lazima tuseme ukweli Wazambia kwa sasa hawana shida sana na TAZARA, japo wao ndio wanatoa Mkurugenzi Mkuu, kosa tulilofanya huko nyuma.

Sasa ili kuinusuru TAZARA, jambo kubwa la kufanya ni kuiunganisha na Malawi kupitia Mbeya pale au Tunduma. Ukifanya hivyo TAZARA itakuwa na umuhimu mkubwa kwa Malawi na kuipa uhai mpya!

Kwa upande wa Malawi, tayari wanafikiria kujenga reli kati ya Central Region na Northern Region, na tayari wana wazo la kuunganisha hiyo reli na TAZARA kama Tanzania watakubali. Kwa hiyo wazo kwa Malawi lipo ni suala la Magufuli kukubaliana na Raisi wa Malawi mradi huo uanze mara moja.

Malawi wanataka sana kuunganishwa na TAZARA kwa sababu ya mradi wao wa makaa ya mawe wa Mchenga Coal Mine sehemu inaitwa Rumphi, mradi wa miti na mbao pale Chikangawana pia uranium pale Kayelekera. Na pia tusisahau suala la mafuta Ziwa Nyasa, yanayoweza kutoa umuhimu wa pekee kwa TAZARA .

Tukikataa kuunganisha TAZARA na Malawi, Malawi wanafikiria kutafuta namna ya kutumia mito Shire na Zambezi ili kufikia Bahari ya Hindi, kwenye mradi utakaoitwa Shire-Zambezi Waterway (SZW). Wakifanya hivyo wataacha kabisa kutumia bandari ya Dar es Salaam. Hivyo basi, ni vema Tanzania kuwafuata Malawi na kujadiliana nao juu ya kuunganisha reli zao na TAZARA

Tanzania inaweza pia kufikiria uwezekano wa kui-divert TAZARA ili ipitie Morogoro na Iringa mjini. Sijui tulitumia akili gani kuwakubalia Wachina wasipitishe TAZARA mjini kwenye mikoa hii. Ni gharama kubwa kufanya hivyo, lakini itakuwa investment itakayolipa sana tu, kama vile SGR!

Dona kantri haihitaji mchina kwenye hilo.

Tunakomaa wenyewe tu kwanza tochi hazina magunzi.
 
Mzee baba anafikiria namna ya kuipifikisha bahari ya Hindi na SGR chato kuiboost hifadhi bubu ya burigi chato(hifadhi ambayo watu wanapita kwa miguu)
 
SGR ya Dar Moro mwaka wa nne huu unakwisha bado haina matarajio wewe unaleta tazara Tena? Wabunge wakienda kuikagua utasikia imeisha kwa asilimia sabini. Ilikua iishe November 2019 Leo hii Ni November 2020 ngoma bado mbichi kabisa.
Mradi wa awamu hii niliouona imeisha kwa mafanikio Ni
Itafika Novemba 2021,bado asilimia 92.
Wapinzani walituchelewesha.
Nasema uwongo ndugu zangu
 
Major Gen.Nyirenda alisumbuliwa sana miaka 1986, aliondolewa kwa hisani ya Mzee Kaunda,hajatokea tena Gen.Manager kama Nyirenda,wazo la mtoa madam ni zuri mno,lifanyiwe kazi.
 
TAZARA haina hali nzuri. Na sababu kubwa ni kwamba utegemezi wa Zambia kwa TAZARA umepungua sana. Kwa sasa Zambia inaweza kupitisha mizigo yao sehemu nyingine zaidi ya Dar es Salaam, kutia ndaniMsumbiji na Afrika Kusini. Lazima tuseme ukweli Wazambia kwa sasa hawana shida sana na TAZARA, japo wao ndio wanatoa Mkurugenzi Mkuu, kosa tulilofanya huko nyuma.

Sasa ili kuinusuru TAZARA, jambo kubwa la kufanya ni kuiunganisha na Malawi kupitia Mbeya pale au Tunduma. Ukifanya hivyo TAZARA itakuwa na umuhimu mkubwa kwa Malawi na kuipa uhai mpya!

Kwa upande wa Malawi, tayari wanafikiria kujenga reli kati ya Central Region na Northern Region, na tayari wana wazo la kuunganisha hiyo reli na TAZARA kama Tanzania watakubali. Kwa hiyo wazo kwa Malawi lipo ni suala la Magufuli kukubaliana na Raisi wa Malawi mradi huo uanze mara moja.

Malawi wanataka sana kuunganishwa na TAZARA kwa sababu ya mradi wao wa makaa ya mawe wa Mchenga Coal Mine sehemu inaitwa Rumphi, mradi wa miti na mbao pale Chikangawana pia uranium pale Kayelekera. Na pia tusisahau suala la mafuta Ziwa Nyasa, yanayoweza kutoa umuhimu wa pekee kwa TAZARA .

Tukikataa kuunganisha TAZARA na Malawi, Malawi wanafikiria kutafuta namna ya kutumia mito Shire na Zambezi ili kufikia Bahari ya Hindi, kwenye mradi utakaoitwa Shire-Zambezi Waterway (SZW). Wakifanya hivyo wataacha kabisa kutumia bandari ya Dar es Salaam. Hivyo basi, ni vema Tanzania kuwafuata Malawi na kujadiliana nao juu ya kuunganisha reli zao na TAZARA

Tanzania inaweza pia kufikiria uwezekano wa kui-divert TAZARA ili ipitie Morogoro na Iringa mjini. Sijui tulitumia akili gani kuwakubalia Wachina wasipitishe TAZARA mjini kwenye mikoa hii. Ni gharama kubwa kufanya hivyo, lakini itakuwa investment itakayolipa sana tu, kama vile SGR!
Tazara,na Urafiki ni miradi iliyoanzishwa kipindi Cha vita baridi,Kati ya mashariki na magharibi,sie turikimbilia kwa wajamaa,china,na Urusi,ndio wakatujengea hii miradi,sasa hv,haina tija kabisa,tulikuwa na viwanda vya nguo kibao,vyote vimekufa,kimebaki Urafiki ambacho china anakitumia kuingiza bidhaa zake bila Kodi,na inawezekana kinatumika kijasusi zaidi,ni kama front tu,lakini kinafanya Kazi zaidi za Siri,
Tazara imeishajifia haina faida kabisa
 
Kwa Nini naona Ni ngumu Sana kutimiza hili, moja ni kwa sababu ya Jiografia ya nyanda za juu kusini, kupitisha Reli kwenda Malawi na milima ya Mbeya sijui Kama itawezekana, pia Reli hii ya Tazara inapaswa kuwekwa treni za kisasa, Kama Ile ya south Africa.
Kutoa reli kwenda Malawi labda kutoka pale Mpemba Hadi Ileje Kisha itoboze Malawi inaweza kuwa rahisi zaidi.
Sio kweli,kutoka Mpemba kupitia Ileje inawezekana na kutoka Mbeya Tukuyu pia inaweza maana survey ya reli ya Mbeya to Kiwira coal mine ilifanyika, kutoka hapo na kufika border haizidi 20km
 
Back
Top Bottom