Mnaweza msiamini, anaweza kuamua kuifumua Tume ya Uchaguzi NEC na kuunda tume huru zaidi ambayo ni inclusive!, kama ameweza kumchukua Prof. Kitila, na yule mama wa ACT, atashindwa nini kuifumua NEC ili uchaguzi wa 2020, uwe uchaguzi huru na wa haki kiukweli kweli!.
P. Prof Kitila na Anna wamehamia CCM ,walipewa nafasi hizo kwa 'sharti' hilo, hakuna ''inclusive'' unayosema
Ma-DC sharti wahamie CCM ndipo wapewe nafasi hizo, hakuna ''inclusive''
Lakini pia hiyo inclusiveness unayosema haiishi katika chama, ni pamoja na kushirikisha wasiokubaliana na wenye mtazamo tofauti.
Tumeona hawawezi kumvumilia mama Ghasia, hiyo ''inclusive'' ipo wapi?
Watawezaje kumu-accomodate Zitto ikiwa hawawezi kukaa meza moja na Hawa Ghasia?
Kuhusu NEC, tatizo si watu wanaofanya kazi NEC, ni mfumo ulioiunda.
Unaweza kuweka malaika watupu wakiwa na makarani masheikh na maaskofu bila mafanikio yoyote kwasababu wanatumikia mfumo wasio na uwezo nao.
Mwenyekiti wa NEC anateuliwa na Rais, anaweza kutimuliwa wakati wowote.
Ndivyo ilivyo kwa Wakurugenzi wa tume. Wasimamizi huko majimboni ni Wakurugenzi ambao asubuhi wanaweza kusikia fulani kateuliwa eneo lake bila yeye kujulishwa, atapangiwa kazi nyingine!
Hawa unadhani wana nguvu gani ya kufanya mambo bila kuingiliwa ikiwa wapo chini ya ofisi kuu
Unaweza kuona viongozi wa NEC ni majaji. Hata hivyo, uwezo wa kutumia taaluma yao unafungwa na teuzi zinazoshikilia kila hatma yao. Hapa ndipo makosa yanapoanzia
Kosa la kwanza, kuteua majaji kunawafanya waliobaki wawe loyal kwa mfumo uliopo wakitaraji nafuu siku za kustaafu kwao. Hili linapunguza 'independence'' ya judicial system
Kosa la pili, mfumo hauna ulinzi wa kazi yao kama ilivyo kwa CAG, na kutoa nafasi ya wao kuwa submissive kwa uongozi na si mfumo wa uchaguzi.
Kufumua NEC ni kutengeneza kitu huru, kisichoundwa na mtu bali watu, kinachojiendesha kwa bajeti yake, kinacholindwa kisheria na kinachoweza kuhojiwa kisheria.
Watu wanaotumikia mfumo huo wanatakiwa kuwa confirmed na chombo kingine na kuwajibika huko si ofisi kuu