Uchaguzi 2020 Magufuli kakosea sana kampeni zake mkoani Mara. Je, haujui mkoa ule au hapendi watu wake?

Hajajua kuwa Mara ni mkoa wa kina Mura. Hawarembi. Watamfurumusha huko. Alipoingia Mara aliona kibao kimeandikwa "KARIBU MKOA WA MARA"???
Muwe mnatoka na kutembelea mikoa mingine walau mara moja moja. Sasa mkoa gani ambao ukienda hauna vibao vya karibu?!?
 
Mgombea wa aina hii hatufai wa Tanzania, Hayupo kujenga umoja wa watu bali kubomoa miaka yote CCM imekuwa madarakani waseme ni sehemu gani ndani ya hii nchi inakila kitu
 
Mkuu hicho kibao kimeandikwa " Karibu mkoa wa Mara, Be Strong"

Mkuu, nilidhani kimeandikwa "Sasa unaingia Mkoa wa Mara". Neno KARIBU hakuna. Wanaume wale. Ukiingia jiaminishe. Hakuna aliyekukaribisha. Acha kulialia. Hahaha, kumbe Magu hawajui.
 
Huu uzi huwezi kuwaona akina bia yangu..wakudadavua .. mgonjwa mtambuka..Mama ntilie wa kawe .. Pascal mayala ..sumve yao..mtashobya ..kipara kipya na USSR ...wanapita juu kwa juu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Muwe mnatoka na kutembelea mikoa mingine walau mara moja moja. Sasa mkoa gani ambao ukienda hauna vibao vya karibu?!?

Usiseme kinadharia wewe. Umefika Mara? Kibao chao kimeandikwa "SASA UNAINGIA MKOA WA MARA". Neno KARIBU halipo.
 
Mbona karibu Tanzania yote ni masikini sana ingawa CCM wanashikilia sehemu kubwa ya majimbo ya nchi hii!!?
Istoshe watanzania wote ni walipa kodi wanaostahili kupelekewa huduma bila kujali itikadi zao.
Hata hili la itikadi siyo uhaini maana limeruhusiwa kikatiba.
 
Hawa jamaa huwa hawajui kabisa kuwa kauli zao za kutulazimisha kuchagua watu wao, hata kama hawatufai, kwa vitisho vya kutunyima maendeleo, huwa ZINATUTAPISHA!

SOME PEOPLE WENT TO SCHOOL TO COLLECT QUALIFICATIONS THEY USE FOR SELFISH GAINS ONLY!
πŸ˜…
πŸ‘Š ✌️✌️✌️πŸ’₯
 
Hata mimi nashangaa anapoahidi kupeleka maji mbali wakati maeneo ya karibu ns ziwa hayana maji.
Kama anataka wagombea wake wapite ndio walete maendeleo basi afute uchaguzi anaofanya ni ufujaji wa pesa.
Kama anaona hawezi kuwapa haki sawa wananchi kwanini aliomba kuwaongoza.
 
Watendee mema watu wote lakini hasan wale wa nyumba ya Imani, wagalatia 6.10
 
Hii kauli Magufuli inabidi ashauriwe a wazee wa CCM asiitamke tena. Ipo siku mtasikia mkoa mzima wa Mtwara unadai kua nchi huru sababu wananyimwa maendeleo kisa wanachagua upinzani. Wajuzi wa mambo hivi mfano mkoa kama Mtwara, Tanga, na Mbeya zikitaka kujitoa Tanzania kila mtu mkoa wake uwe nchi huru kunaprocess gani zinafatwa.? Kuwagawa watu kimakundi mbaya sana especially sisi watanzania ambao kila Mkoa ukiamua uwe nchi idadi ya raia inatosha kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…