Elections 2015 Magufuli lugha za Kimataifa ni Kizungumkuti, wenye ufahamu tujadiliane

Elections 2015 Magufuli lugha za Kimataifa ni Kizungumkuti, wenye ufahamu tujadiliane

Wewe! tulia upakatwe acha kutapatapa. Magufuli yuko vizuri sana. halafu ngeri sio kigezo. tunachagua Rais wa Tanzania na sio rais wa ughaibuni. plz kuwa muelewa
 
ndugu zangu wakawa kwasasa ni magufuli kushinda na kuingia ikulu kuhusu kizungu tutashughulikia baadae
 
QUOTE=;14126205]

"I am a politicians". "I dont want to take this time as saying so many political...."

"Simple and clear is only congregations to you.."

"To the University Korindor... , Co... Cor,.. Colimbia univeristy to the assistance we are getting to this hospt"..

Bila shaka huyu jamaa anatamani KIMATUMBI iwe lugha ya kufundishia Tanzania.

Kwa kuwa alisoma katika mfumo wa lugha ya Kiingereza, na Katiba ya nchi inahitaji awe na kiwango sahihi cha elimu, huyu jamaa anayo hiyo elimu?

Kwa harufu ya degree za magumashi, ni dhahri alipishana na wahadhari mlangoni. Kwa mtino huu bado anasifa ya kugombea hata ubunge?

Unapochangia, ulinganishe na "SADDAM wa LiBYA/KUWAIT"

LINGANISHA NA MGOMBEA WA UKAWA
MHESHIMIWA LOWASA.

[/QUOTE]

Kuishiwa hoja huko...kiingereza kinahusiana vip na maendeleo yetu..
 
Last edited by a moderator:
ndo maana mikataba inasainiwa miaka 100 kumbe lugha hamna kwa viongozi wetu
 
Nasikia eti baada ya kuhutubia hapo ikawa zamu yao hao wazungu kuhutubia na yeye akawa mtafsiri. Walipomaliza wakawaaga wananchi Bye! Bye! Na yeye akawatafsiria Nunua! Nunua!

Ha ha haaaaaaa tehe tehe tehe
 
Ni kweli, ila ishu ya hapa ni je doctorate yake aliipata kwa lugha gani? maana haiwezekani kama mtu uko sawa ukasoma mpaka Phd kwa lugha ya kizungu alafu sentence rahisi tu ya kizungu ukashindwa unga! Hapa ni kwamba eidha mtu haufundishiki au ulikuwa haufiki darasani ila umepitishwa tu na kupewa elimu uliyonayo, haukuitafuta!

Magufuli ni mtu wa Kemia na mathematics, matumizi yake ya kiingereza yako limited katika kubalance equations, tests, na vitu related. Pia, Magufuli sio Muingereza, Ni Mtanzania aliekulia na kusomea Tanzania katika shule za kawaida. Hadhira yake katika siasa kwa kiasi kikubwa imekuwa ya Watanzania, sasa kuna umuhimu gani wa yeye kukijua kiingereza kama anaotarajiwa kuwasiliana nao ni watu wasiokijua kiingereza. Tunahitaji kumuelewa anachozungumza na si kusikilizwa na wazungu hasa katika kipindi hiki ambapo tumejidhatiti katika kupunguza utegemezi wa misaada ya hao wenye kiingereza chao. Issue ya kushangaza, ni mtu wa arts asieweza kuongea kiingereza kwa nadhani hilo ndilo la msingi.
 
Yaani nilisikiza ile clip anayosema -'' I am poritishians... I don't want to take this eehh!!! This time as saying so many poritical words, simple and crear is only I congrugation to you, to the University corumbi.... you... Corumbia University for good assistance we are getting to this hospital.. '' Huyo ni mwalimu wa secondary, na PhD holder. Sipati picha wanafunzi wake..

anazidiwa hata na diamond platenum mwenye elimu ya darasa la saba
 
Magufuli ni mtu wa Kemia na mathematics, matumizi yake ya kiingereza yako limited katika kubalance equations, tests, na vitu related. Pia, Magufuli sio Muingereza, Ni Mtanzania aliekulia na kusomea Tanzania katika shule za kawaida. Hadhira yake katika siasa kwa kiasi kikubwa imekuwa ya Watanzania, sasa kuna umuhimu gani wa yeye kukijua kiingereza kama anaotarajiwa kuwasiliana nao ni watu wasiokijua kiingereza. Tunahitaji kumuelewa anachozungumza na si kusikilizwa na wazungu hasa katika kipindi hiki ambapo tumejidhatiti katika kupunguza utegemezi wa misaada ya hao wenye kiingereza chao. Issue ya kushangaza, ni mtu wa arts asieweza kuongea kiingereza kwa nadhani hilo ndilo la msingi.

Asante, nimekuelewa vizuri.
Mimi nilihoji tu, ila NIMESHAMPIMA KWA VIGEZO VYANGU na kapita with flying colors, ndiye mwenye kura yangu tarehe 25.10.2015.
 
Magufuli ni msomi aso na shaka, inawezekana hata darasani somo la lugha lilimpiga chenga maana hata ukisikiliza anapozungumza kiswahili ni dhahiri(anafikiri) anatafsiri toka kikwao, raisi wa japan hajui kingereza, hata putin hajui kingereza, na lugha sio kigezo cha weledi wa uongozi, uongozi hauna lugha ni karama toka kwa muumba, kama kuna wasiwasi na usomi wake ulinganishwe na wakemia wenzake, watoeni popote ulimwenguni uwafanyie majaribio uone -HAPA KAZI TU.
 
Yaan hii ni aibu sana pombe hajui kiingereza mm nimeleta hapa uzi kuhusu kingereza cha pombe magamba wakabisha.

Tena wengine wakasema eti pombe atauwa anatembea na mkalimani. Hiyo bajeti itatoka wapi?

Mjionee bandugu pombe ni aibu
 
Nasikia alisomea Lake Sekondari ya Mwanza. Kwa wakati wake yeyote aliyemaliza sekondari ya Lake ni wale waliokuwa na kiwango kidogo cha ushindi kwa maana nyingine kwa wakati ule walikuwa wanaenda walioshindwa na kama Baba yako ana uwezo wa kifedha unapelekwa Lake.
 
Yaan hii ni aibu sana pombe hajui kiingereza mm nimeleta hapa uzi kuhusu kingereza cha pombe magamba wakabisha.

Tena wengine wakasema eti pombe atauwa anatembea na mkalimani. Hiyo bajeti itatoka wapi?

Mjionee bandugu pombe ni aibu

Lowassa mnatarajia kuwa atakuwa anatembea na watu wangapi wa ziada ukiacha Walinzi, mpambe na mkalimani? Kuna watu wa kutunza na kunote mawazo yake, kuna mtu wa kumkumbusha vitu basic kabisa vya maisha yake ya kila siku, kuna mtu wa kuzungumza na kuhutubia kwa niaba yake maana Sumaye hatakuwa karibu, kuna madaktari, kuna mtu wa kumpigia signature maana kwa mambo yalivyo! Sasa wote hao ni kwa bajeti ipi? Msitudanganye kuwa eti ana pesa, maana tunajua mpaka sasa mtaji umekata.
 
Magufuli ni msomi aso na shaka, inawezekana hata darasani somo la lugha lilimpiga chenga maana hata ukisikiliza anapozungumza kiswahili ni dhahiri(anafikiri) anatafsiri toka kikwao, raisi wa japan hajui kingereza, hata putin hajui kingereza, na lugha sio kigezo cha weledi wa uongozi, uongozi hauna lugha ni karama toka kwa muumba, kama kuna wasiwasi na usomi wake ulinganishwe na wakemia wenzake, watoeni popote ulimwenguni uwafanyie majaribio uone -HAPA KAZI TU.

Watu wametengeneza video halafu wanajaribu kufosi kingi kisela tu.
 
Natumia simu ya mkononi kwa sasa na bahati mbaya imeshindwa kufungua hiyo You Tube video.Ila niseme wazi,kama dokezo hilo kweli ndiyo sample ya kingereza chake it's a disaster.Something is seriously wrong.Daktari wa Filosofia awe na kingereza kibovu namna hiyo.Hapana,ipo shida.Na itakuwaje sasa katika mawasiliano ya kimataifa?Yetu macho.

Back
Top Bottom