Magufuli, Makonda na Sabaya; ilikuwaje tukapata viongozi wa aina hii?

Magufuli, Makonda na Sabaya; ilikuwaje tukapata viongozi wa aina hii?

Hat Uko cdm Kuna manyamela Kama ilivyo kwakina sabaya na makonda maanake cdm mnajiona Kama nyinyi Ni malaikaa hakuna vijana wahuni wote mko ckean
 
Wakuu

Historia ya nchi ina mapito mengi sana mapito mazuri na mapito mabaya, lakini ilikuaje kama nchi tukapata viongozi aina ya watu waliotajwa hapo juu,

Najaribu kuwaza nashindwa kupata jibu ilitokea nini hadi tukaongozwa na watu wa kariba hiyo natamani vizazi vijavyo visipate kufahamu historia za viongozi wa aina hiyo yaani wasikumbukwe kwa lolote kabisa maana ukihadithiwa ukweli unaweza kujikuta unaanza kulia kwa uchungu jinsi walivotuongoza hawa waliotajwa hapo juu.

Nauliza ilikuaje wakawa viongozi?
Mkuu mbona hao bado ni nafuu... iko siku fisiemu watatuletea kichaa kabisa... hapo ndipo kutakuwa kilio na kusaga meno!!
Watu wanaangalia nani atawafaa kwa maslahi yao.
 
Siyo hao tu orodha ni ndefu sana kwani Ndugai, Tulia, Chalamira, Kigwangala, Gwajima, Na wengine wengi tu wana sifa zipi za kuwa viongozi?
 
Kwa ujumla uongozi wa marehemu ilikuwa ni laana kubwa kwa Taifa.

Nadhani kumbukumbu ziwepo maana hata Hitler kumbukumbu zipo. Vizazi vijavyo vinastahili kufahamu kuwa kuna wakati nchi ilipita katika giza nene la uongozi.
 
tunataka mkomboe matako yenu sasa maana laana imeondoka,hizi blah blah zimetosha sasa.
 
Wakuu

Historia ya nchi ina mapito mengi sana mapito mazuri na mapito mabaya, lakini ilikuaje kama nchi tukapata viongozi aina ya watu waliotajwa hapo juu,

Najaribu kuwaza nashindwa kupata jibu ilitokea nini hadi tukaongozwa na watu wa kariba hiyo natamani vizazi vijavyo visipate kufahamu historia za viongozi wa aina hiyo yaani wasikumbukwe kwa lolote kabisa maana ukihadithiwa ukweli unaweza kujikuta unaanza kulia kwa uchungu jinsi walivotuongoza hawa waliotajwa hapo juu.

Nauliza ilikuaje wakawa viongozi?
Ni aibu ya kihistoria hasa Magufuli hakuwa na sifa ya kuongoza nchi, mzee mmoja alisema kuwa anafaa kuwa nyampara wa barabara tu, alikuwa sahihi kabisa
 
Exactly,kwa upande wa Magu Hana hotuba hata moja ya kuvutia,zaidi ya kufoka foka tu,na kauli Kama bakini na "Mavi yenu majumbani"
Na kule Mtwara, wananchi waliposoma risala kuwa barabara ni nyembamba, wanaomba ipanuliwe, marehemu akawajibu kwa kumwonesha mama aliyekuwa karibu na kumwuliza, "na wewe, unataka upanuliwe wapi?". Kauli za ovyo kabisa.

Na kule Tunduma, alipoona mama amenyanyua bango lililoandikwa, tunaomba maji, yeye alijibu, "kamwombe mume wako".
 
Kuna jamaa flan Tanroad alinisimuliaga magu alivyokuwa waziri alikataa kabisa kusijengwe barabara za waenda kwa miguu (sidewalks) eti ni anasa. Wakati yeye alikua akilamba na kukunja 10%
Ndio maana magonjwa yasiyoambukiza (Sukari na Pressure) yamezidi hakuna sehemu ya kutembelea watu katika miji mikubwa kama wewe in muoga wa kugongwa na pikipiki!! Hivyo no mazoezi kwa 80% ya wakazi
 
Kabisa yan!!! Yan imefikia ccm inamhonga pesa mpinzani ili aende ccm kisha anapewa ubunge na uwaziri!!! Ile ilikua ni aibu sana kwa ccm Ila magu hakujua!??
CCM inaungwa mkono na watu wajinga (TWAWEZA). Kwenye kundi la wajinga, vi vigumu sana kumpata kiongozi mzuri. Ukimwona mwenye akili au msomi, yupo CCM, 90% ni opportunist.
 
Ni heri nionekane nina roho mbaya na kauzu kuliko kufadhili binadamu, binadamu hajawahi kuwa na shukrani hata siku moja ( ni wachache mno). Magufuli alijitoa sana kwa wananchi wa Tanzania alifanya kazi usiku na mchana, aligusa kila nyanja na hakuna kipindi chochote watanzania tulichoshuhudia maendeleo ya haraka kama kipindi cha JPM. Wengi mlioshupaza shingo kutaka kuharibu legacy ya Magu wengi wenu ni wezi, majambazi, wala rushwa, wapinzani msiojielewa au watu msiolitakia mema taifa letu.

NB: mtu kama kikwete anaonekana ndio kipenzi cha wengi kwa sasa ni kwasababu alikua ni kiongozi dhaifu sana, watu walipiga sana hela hali ya kuwa yeye mwenyewe yupo bize akipiga picha na Marais wa dunia. Zaidi na zaidi Magu pia ni binadamu hivyo ana mapungufu ya kiubinadam, ila ukweli ni kwamba ukiachana na nyerere basi rais bora wa muda wote atabaki kuwa ni magufuli, ndiye rais aliyeliliwa na karibu Africa nzima pindi mauti ilipomfika .. RIP MAGUFULI MUNGU AKULAZE MAHALI PEMA PEPONI AMEEN ..
Lazima una matatizo, si bure. Ni maendeleo gani aliyoyaleta Magu ukilinganisha na watangulizi wake. Au na wewe ni kati ya wajinga waliokuwa wanadanganywa na TBC?

Ukuuaji wa uwekezaji wakati wa Kikwete 28%; wakati wa Magufuli 4%.

Ukuaji wa utalii wakati wa Kikwete 15%, wakati wa Magufuli 3.6%

Thamani ya mauzo ya nje ya mazao ya kilimo, wakati wa Kikwete 14%; wakati wa Magufuki -5%

Ujenzi wa barabara za lami awamu ya Kikwete 10,000km+, wakati wa Magufuli 2,000km+.

Uzalishaji dhahabu wakati wa Kikwete, Tanzania ilikuwa nchi ya 3 Afrika, wakati mwingine ya 4; wakati wa Magufuli ni nchi ya 6.

Wakati wa Kikwete GDP per capita iliongezeka kwa $400, wakati wa Magufuli iliongezeka kwa $80 tu.

Kwa vigezo vyote vya maendeleo ya uchumi, Magufuli aliharibu uchumi wa nchi.
 
Kila zama na kitabu chake ndio maana Marekani kuna democrats (Rais Samia) na Republicans (Rais Magufuli). Aliyoyafanya JPM yalikuwa sahihi kwa wakati wake ila sasa tumuunge mkono mama yetu kipenzi (Democrat) Samia Hassan.
Sidhani kama unajua unachoongea...Marekani unataja Republicans na Democrats, vyama viwili tofauti halafu unafananisha hilo na hapa dhalimu Magufuli na Mama Samia...chama kile kile, watu wale wale, sera zile zile, ujinga ule ule, unafiki ule uleeee...are you serious?

Kama sio Mungu sijui tungeponaje kwani mwendazake alianza kupigiwa ndogondogo asiondoke hadi kifo kimtoe na kweli Mungu akaitikia na ikawa hivyo! Ingekuwa kwa mapenzi ya shetani (CCM?) jiwe lingebaki pale pale na mateso pamoja na vilio vyote vingebaki pale pale!
 
Wakuu

Historia ya nchi ina mapito mengi sana mapito mazuri na mapito mabaya, lakini ilikuaje kama nchi tukapata viongozi aina ya watu waliotajwa hapo juu,

Najaribu kuwaza nashindwa kupata jibu ilitokea nini hadi tukaongozwa na watu wa kariba hiyo natamani vizazi vijavyo visipate kufahamu historia za viongozi wa aina hiyo yaani wasikumbukwe kwa lolote kabisa maana ukihadithiwa ukweli unaweza kujikuta unaanza kulia kwa uchungu jinsi walivotuongoza hawa waliotajwa hapo juu.

Nauliza ilikuaje wakawa viongozi?
Hili ni zao la katiba yetu,'weak constitution'
 
Hakuna kosa tulilowahi kulifanya watanzania kama kuruhusu watu wasio na uwezo kuwa wanasiasa !!!! Hili ndilo limetamalaki kwa sasa ,hasa katika chama cha mapinduzi hilo tuache unafiki ndio lililopo!!! Mtu anajifanya ni mtiifu kwa cha ana foji mpaka cheti cha taaluma ili apate cheo!! Kibaya zaidi eti hata mwanasiasa akifoji vyeti vya taaluma sheria haimgusi kama alivyofanya bashite!! Lakin mtumishi yoyote anaondolewa kazini!!? Kweli hili ni ajabu kabisa!!!
Panatakiwa katiba mpya ili upatikanaji wa viongozi wawe wanafanyiwa usaili,.
Iwe ni wazi kua Kuwa wanaccm sio tiketi ya kupata cheo!!! Cha uwaziri,ukuu wa mkoa,ukuu wa wilaya au u das!! Hivi vyeo watu wenye sifa bila kujali vyama waombe kazi na wapewe usaili!??
Yaani kweli vigezo vya uongozi makini vilitupwa pembeni, mradi ukiwa kada na at least vyeti vya Yahana University evening class, unapata cheo.... kaaazi kwelikweli.
 
Kuna jamaa flan Tanroad alinisimuliaga magu alivyokuwa waziri alikataa kabisa kusijengwe barabara za waenda kwa miguu (sidewalks) eti ni anasa. Wakati yeye alikua akilamba na kukunja 10%
Duh kama ni kweli basi jamaaa alikuwa mgumu.
 
Wakuu

Historia ya nchi ina mapito mengi sana mapito mazuri na mapito mabaya, lakini ilikuaje kama nchi tukapata viongozi aina ya watu waliotajwa hapo juu,

Najaribu kuwaza nashindwa kupata jibu ilitokea nini hadi tukaongozwa na watu wa kariba hiyo natamani vizazi vijavyo visipate kufahamu historia za viongozi wa aina hiyo yaani wasikumbukwe kwa lolote kabisa maana ukihadithiwa ukweli unaweza kujikuta unaanza kulia kwa uchungu jinsi walivotuongoza hawa waliotajwa hapo juu.

Nauliza ilikuaje wakawa viongozi?
Kwa tulipofikia nchi ilihitaji watu Kama hao ili kuirudisha kwenye mstari. Ufisadi, rushwa, madawa ya kulevya, ujangiri, ujambazi, watumishi hewa, wenye pesa na madaraka kunyanyasa masikini n.k.

JPM ilikuwa ni mpango wa Mungu ili kusafisha uchafu wote uliokuwa umeshamiri kwenye nchi hii katika awamu zilizopita. Mzee kafanya kazi yake miaka 5 tu tumeona matokeo yake. Angalau leo nchi ipo vizuri na maendeleo yanaonekana.

Wale majizi na mafisadi kamwe hamuwezi kupenda aina hii ya utawala, ndiyomaana Magufuli hatoki midomoni mwenu hata baada ya kifo chake, moto wake uliwachoma kweli kweli.
 
Wakuu

Historia ya nchi ina mapito mengi sana mapito mazuri na mapito mabaya, lakini ilikuaje kama nchi tukapata viongozi aina ya watu waliotajwa hapo juu,

Najaribu kuwaza nashindwa kupata jibu ilitokea nini hadi tukaongozwa na watu wa kariba hiyo natamani vizazi vijavyo visipate kufahamu historia za viongozi wa aina hiyo yaani wasikumbukwe kwa lolote kabisa maana ukihadithiwa ukweli unaweza kujikuta unaanza kulia kwa uchungu jinsi walivotuongoza hawa waliotajwa hapo juu.

Nauliza ilikuaje wakawa viongozi?
Nimesimuliwa jambo fulani na mtu mkubwa tu ikanishangaza sana. Kwamba JIWE alikuwa na watu wake kila kona ya nchi hii ambao walitumia ubabe, ukatili na vitisho hasa kwa wafanyabiashara wakubwa ili wawe wanatoa fedha ambazo alizitumia kujenga miundombinu mbalimbali ya serikali na yake binafsi nje ya bajeti. Lengo lilikuwa ni kujipa uhalali wa kutawala mbele ya watanzania, na pia alipiga marufuku kuwanyanyasa machinga na mama lishe ili aonekane ni mtu wa wanyonge maana ndio wengi Tanzania. Huyo mtu anasema walikuwepo wakuu wa wilaya, mikoa na viongozi wengine ndani ya chama chake waliokuwa "wanakula" pamoja naye hayo mapato haramu. Anasema fedha zingine alikuwa anatembea nazo kwenye gari yake ili azigawe kwa wanaoitwa wahitaji barabarani na kununulia mahindi ya kula. Sasa ili siri zake hizo zisifichuke aliamua na kupanga kutokomeza kabisa upinzani na wasipate ubunge maana wangeweza kubaini na kuhoji anakopata fedha za miradi mbalimbali ikiwemo ya Chato na anazogawa barabarani wakati hakuna bajeti iliyopitishwa na bunge kwa matumizi hayo. Lengo lake lilikuwa ni kutawala zaidi ya vipindi viwili. Huyo ndugu anasema hata huyo DC aliyekamatwa kwa tuhuma za ujambazi na kumiliki genge la Uhalifu ni mwanachama wa kundi hilo la JIWE. Inahisiwa kwamba wengine wapo Dar, Tunduma, Arusha, Mwanza, Mara, Mtwara, Mbeya na Kigoma.

Bahati mbaya hakutambua kuwa anamchukiza Mungu kwa yote aliyoyafanya.

Tujifunze kuwachambua vizuri watu tunaowapa dhamana ya kutuongoza hasa ngazi ya Rais. Tumejifunza, tusirudie makosa.
 
Wakuu

Historia ya nchi ina mapito mengi sana mapito mazuri na mapito mabaya, lakini ilikuaje kama nchi tukapata viongozi aina ya watu waliotajwa hapo juu,

Najaribu kuwaza nashindwa kupata jibu ilitokea nini hadi tukaongozwa na watu wa kariba hiyo natamani vizazi vijavyo visipate kufahamu historia za viongozi wa aina hiyo yaani wasikumbukwe kwa lolote kabisa maana ukihadithiwa ukweli unaweza kujikuta unaanza kulia kwa uchungu jinsi walivotuongoza hawa waliotajwa hapo juu.

Nauliza ilikuaje wakawa viongozi?
Ebu niadithie huo ukweli, nijue cha ku-comment
 
Back
Top Bottom