Karltika wagombea wote wa Uraisi , JPM ndiye aliyekuja na hoja za maendeleo, Lissu alichukua muda wote wa hotuba zake kwenye mkutano wa KM ya Chadema, kuelezea yaliyomkuta na kuzungumzia uogozi wa magufuli, na alipoalikwa ACT, hotuba yake ilikuwa ileile ya kumshutumu Magufuli na kueneza uongo, eti TZ haina marafiki na haipendwi, na hilo aliliona alipotembea Ulaya na Umarekani. Kwanza Lissu katika safari zake zote hizo hakukutana na kiongozi yoyote wa maana, ni afadhali ya Zitto alikutana na kiongozi wa Labout Party ya UK.Hata kama ni kusema uongo basi na uongo wenyewe uwe na ushawishi kidogo.
Kauli kama hizi zinaonyesha kwamba Jpm hana hoja, lakini pia amewadharau wapiga kura.
Kwanini asijikite kuwaeleza atawafanyia nini waTz ktk miaka 5 inayokuja, na badala yake anashambulia wapinzani kwa hoja za uongo?
Tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe ni mpinzani gani ameharibu miundombinu ya nchi hii?
Kuhusu kulinda rasilimali zetu, kila mmoja anajua mikataba yooote mibovu ya kifisadi ilisainiwa baina ya serikali za ccm na makampuni ya kibeberu.
Video hii hapa msikilize tangu dakika ya 4:00.
Lissu alizidi na kusema eti viongozi wa EA hawakuja kwenye Mazishi ya Mkapa kwa sababu ya uhusiano mbaya na magufuli, huu ni wakati wa Maradhi ya Corona viongozi wengi hawaruhusiwi na katiba kufanya safari za njee na wanachungwa. K.m.: Raisi uhuru ameweka nchi yake kwenye Lock Down, alafu yeye asafiri itakuwaje.
Ukiangalia kwa upande wa ACT, inasikitisha kuwa Membe sio mzungumzaji mzuri, na speech yake haikuwa ya kuvutia, naye ilikuwa ya kilio, lakini ilikuwa na afadhali kwani alikipongeza sana Chama chake Kipya na kukipigia debe.