Ukiona Uwanja wa Taifa ambao kwa sasa panaitwa kwa Mkapa ni landmark ambayo Mkapa kaiacha. Hata kama pasingeitwa uwanja wa Benjamin Mkapa ila vizazi vya sasa na vijavyo havitasahau nini Mkapa alifanya.
Ukiona UDOM huwezi kumsahau JK,
ukiona Mloganzila Hospital huwezi kumsahau JK,
ukiona Terminal 3 huwezi kumsahau JK,
ukiona JKCI huwezi kumsahau JK.
Ukipita Kigamboni bridge huwezi kumsahau Nyerere
Barabara nyingi nchini zimejengwa na marais 2 Mkapa na JK, kwa asilimia kubwa JPM akiwa Waziri wa ujenzi kasi ya ujenzi ilikuwa kubwa sana.
Legacy ya JPM hata isipopiganiwa kwa nafasi yake kama Rais kwa yale aliyofanya akiwa Waziri wa Ujenzi yanatosha kumpa heshima.
Stiglers gorge,
Ukuta wa Mererani,
Daraja la Selander,
Ubungo na Mfugale interchange
Miradi ya umeme vijiji zaidi ya 9000 na maji vijijini
Maji kutoka shinyanga mpaka Tabora
Bomba la hoima (initiative)
Ku-execute SGR ya umeme
Kuweza ku-negotiate makininia Tz kupata 16% shareholding ya Twiga Corporation
Ku-crack drug dealers
Kupunguza ujambazi na unyang'anyi wa fedha na wizi wa silaa
Ujenzi wa vituo vya afya, hospitali za wilaya na ukarabati wa shule kongwe
Kurahisisha upatikanaji wa hati za ardhi kwa kuwa na makamishna wa ardhi kila mkoa
kuifanya biashara ya madini hasa dhahabu kufanyika kwa uwazi na dhuluma/unyang'anyi kupungua kwa kiasi kikubwa
Watoto kusoma shule bila malipo
Kuifufua ATC na kuweza kununua ndege 12 in 6 years kutoka ndege moja ya kukodi;
Kuihamisha serikali karibu yote ika-function kutokea Dodoma, loh mzee Mwinyi alikiri wao wamekaa miaka 30, wanashangaa mwanaume in 3 years Dodoma imewezekanika.
JPM ni binadamu, tumpe heshima kwa aliyofanya; tuishi na kusheherekea mengi aliyofanya kwa faida ya Watanzania. Ameondoka mengi kayaacha kwa ajili ya familia Tanzania. Huo ni uzalendo.
Kwa uchache ni ngumu sana kuzimisha kumbukumbu njema ya huyu mwanaume. Well, miaka 5 na miezi 5 akiwa Rais wa nchi kuna mema mengi kafanya na kuna mabaya kafanya; tumheshimu kwa mema aliyofanya na tusamehe kwa mabaya aliyofanya. Hata Nyerere alifanya mengi, ila katika hayo lazima kuna mabaya alikuwa nayo. Uungwana na kukumbatia wema wa mtu kwa mema aliyofanya. Ku-fight mtu alielala haina maana yoyote, ku-embrace legacy yake ni heshima kwake na kwa Taifa kwa ujumla.
Nasi tuishi kwa kutimiza wajibu wetu.