Hukumu hii imefuta sifa zote za Magufuli kwamba alikuwa anajali wanyonge, hukumu hii inatoa hitimisho kuwa magufuli alikuwa fisadi kwa sababu fisadi ni mtu anayetumia fedha za umma kwa kukiuka taratibu za matumizi ya fedha zilizowekwa kisheria. Magufuli badala ya kdeal na mafisadi wa fedha za umma yeye alideal na CAG. Atubu huko aliko.Mahakama ya Rufani ya Tanzania imetoa uamuzi wa kihistoria unaoweka msingi imara wa ulinzi wa taasisi huru za kikatiba nchini, ikisisitiza kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ana ulinzi kamili wa ajira yake na hawezi kuondolewa madarakani kwa kutumia sheria za kawaida za Bunge au matakwa ya muhula wa miaka mitano.
Desemba hii na katika mwendelezo wa mashauri ya kikatiba yaliyovuta hisia za wengi, Mahakama imebainisha wazi kuwa nafasi ya CAG si ajira ya kawaida ya mkataba au nafasi inayotegemea utashi wa mhimili wa utendaji, bali ni muhimili mkuu wa kikatiba wa kulinda rasilimali za umma unaopaswa kulindwa dhidi ya kuingiliwa na wanasiasa.
Mfumo wa Kikatiba na Mtego wa Sheria ya Ukaguzi (PAA)
Chanzo cha mgogoro huu wa kisheria kilianzia kwenye Kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma (Public Audit Act - PAA) ya mwaka 2008, ambacho kiliweka ukomo wa muhula wa miaka mitano kwa CAG, ukiwa na fursa ya kuongezwa mara moja pekee.
Kifungu hiki ndicho kilichotumiwa na Mamlaka ya Uteuzi kumwondoa aliyekuwa CAG, Profesa Mussa Juma Assad, mnamo Novemba 2019 kwa maelezo kuwa muhula wake wa miaka mitano ulikuwa umeisha, licha ya kwamba alikuwa bado hajafikisha umri wa kustaafu kwa mujibu wa Katiba.
Katika uchambuzi wa Mahakama, ilibainika wazi kuwa Ibara ya 144(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kwa uwazi kabisa kuwa ukomo wa CAG madarakani unatokana na umri wa kustaafu (miaka 60 au miaka 65 kama ilivyowekwa na sheria za kazi) na si kwa vigezo vya kuhesabu miaka ya muhula (term limit).
Mahakama ilieleza kuwa Bunge lilivuka mipaka yake ya kikatiba pale lilipotunga Kifungu cha 6(1) cha PAA kwa kuongeza sharti la muhula wa miaka mitano. Katiba ililipa Bunge mamlaka ya kubainisha umri wa kustaafu pekee, na si kuvumbua mfumo mpya wa ukomo wa muda unaoweka rehani usalama wa ajira ya CAG.
Kwanini Kuondolewa kwa Prof. Assad Kulikuwa Batili?
Katiba ya Tanzania imeundwa kwa namna inayompa CAG ulinzi wa hali ya juu wa kiofisi (security of tenure), unaofanana na ule wanaopewa Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani. Ibara ya 144 ya Katiba inabainisha kuwa CAG anaweza kuondolewa madarakani kabla ya umri wa kustaafu kwa sababu mbili kuu pekee:
Hata hivyo, kuondolewa huko hwezi kufanyika kwa tamko la Rais au utashi wa kisiasa, bali lazima kufuate mchakato huru wa uchunguzi unaofanywa na Tume Maalum (Tribunal) iliyoundwa kisheria, kisha kutoa mapendekezo.
- Kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa sababu ya ugonjwa au sababu nyinginezo.
- Utovu wa nidhamu au ukiukaji wa maadili ya viongozi wa umma.
Kwa kuwa Prof. Assad hakuondolewa kwa mchakato wa Tume wala hakuwa amefikisha umri wa kustaafu, Mahakama ilihitimisha kuwa kuondolewa kwake kwa kigezo cha "kuisha kwa mkataba wa miaka mitano" kulikiuka Katiba moja kwa moja na kulikuwa batili tangu mwanzo.
Mfarakano wa Kisheria: Kwanini Assad Hakurejeshwa na Kichere Kubaki Ofisini?
Eneo lililozua mjadala mkubwa miongoni mwa wananchi na wanasheria ni sababu zilizofanya Mahakama isiamuru Prof. Assad arejee ofisini au kutengua uteuzi wa CAG wa sasa, Bw. Charles Kichere.
Mahakama ilifafanua changamoto hiyo kupitia misingi miwili kuu ya kisheria:
Hukumu hii inaacha alama kubwa katika Mfumo wa Sheria na Utawala Bora nchini Tanzania kwa mambo makuu yafuatayo:
- Uhalali wa Uteuzi wa CAG wa Sasa: Licha ya kuwa kuondolewa kwa Prof. Assad kulikuwa batili, uteuzi wa Bw. Charles Kichere ulifanyika chini ya Kifungu cha 4 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma (PAA)—kifungu ambacho hakijawahi kutangazwa kuwa ni kinyume cha Katiba. Kisheria, hatua iliyochukuliwa chini ya sheria inayotambulika wakati huo inabaki kuwa halali, na ubatili wa kifungu cha ukomo wa miaka mitano hauharibu moja kwa moja kifungu cha uteuzi.
- Kuepuka Mkwamo wa Kikatiba (Dual Incumbency): Mahakama ilibainisha kuwa kuamuru Prof. Assad arejeshwe madarakani wakati kuna CAG mwingine aliyetawazwa kisheria kungetengeneza mgogoro mkubwa wa kikatiba wa kuwa na wakuu wawili wanaotambulika kwenye taasisi moja ya ukaguzi.
- Nafasi ya CAG si Ajira Binafsi ya Fidia: Mahakama ilisisitiza kuwa kesi za kikatiba hazilengi kufidia maslahi binafsi ya mtu aliyepatwa na madhara ya kiofisi (kama vile kudai kurejeshwa kazini au kulipwa fidia ya ajira), bali zinalenga kutoa tafsiri ya kisheria na kulinda Katiba kwa maslahi ya umma mzima.
Licha ya kuwa Prof. Mussa Assad hakurejea kwenye kiti cha CAG, ushindi wa kesi hii ni wa wananchi na Katiba ya nchi. Mahakama imeweka mpaka ulio wazi: Wadhifa wa CAG si nafasi ya kisiasa, na hakuna mtawala anayeweza kumwondoa njiani nje ya utaratibu uliowekwa na Katiba.
- Kuimarika kwa Utawala wa Sheria (Supremacy of the Constitution): Imetuma ujumbe mzito kwa Bunge na Muhimili wa Utendaji kuwa sheria yoyote itakayotungwa chini ya Katiba haitakuwa na nguvu kama inamnyima kiongozi wa kikatiba hifadhi ya ajira yake iliyowekwa na Katiba Mama.
- Uhuru wa Taasisi ya CAG: Hakuna CAG wa sasa au wa baadaye atakayefanya kazi kwa hofu ya kufukuzwa au kuondolewa pindi muhula wa miaka mitano unapotimia, maana sheria hiyo sasa ni mti mkavu. CAG ana uhuru wa kukagua na kutoa ripoti bila kuogopa kukatishwa tamaa na shinikizo za kisiasa.
- Ulinzi wa Rasilimali za Umma: Ili kuisimamia Serikali ipasavyo, CAG anahitaji ulinzi usiotikisika. Maamuzi haya yanamrejeshea CAG utulivu wa kufanya kazi kwa mujibu wa taaluma na kanuni za kimataifa (kama Azimio la Lima na Mexico kuhusu uhuru wa taasisi za ukaguzi).
Naongezea ukiona mtu anamsumbua na kumchukia mkaguzi wa nje au wa ndani huyo ni mwizi.Jiwe likuwa dikteta haswa na fisadi! Ukiona mtu au kiongozi mkuu anamsumbua CAG, ujue huyo ni fisadi na mwizi wa Mali ya umma.
Shangaa na wee hapo.Huyu aliyesema Katiba ni kakijitabu tu, watu wanavunja amri za Mungu nini Katiba.
Au apotee tu kama ile ndege ya Air Malaysia ilivyopotelea mbali.Kama hawezi kuondolewa KIKATIBA tutamuondoa kwa RISASI.
Achague mwenyewe anaondoka kwa kalamu au anaondoka kwa mguu wa kuku.
Cc: Tlaatlaah Lucas Mwashambwa
Hao wajinga wameshaandika hukumu kwa maelekezo toka Kizimkazi wanangojea tu kuisoma kama Bimsumi alivyokuwa anasoma hotuba kwenye IPU.CAG, kama ilivyo kwa "Majaji wa Mahakama Kuu, au Mahakama ya Rufani...." Kikatiba hawawezi kuondolewa kwenye nafasi zao kwa utashi wa kisiasa au sheria potofu zilizotungwa na Bunge.
Sasa tuwakumbushe hawa Majaji wa Kesi ya Tundu Lissu, watende haki bila ya hofu ya ajira zao.
Ndugai walimpiga mkwala wa kumbadiliashia walinzi, wasaidizi, hadi dereve just overnight mwenyewe akajua maana yake nini akasaini barua.Huyo Supika alipewa barua tu ya kujiuzulu asaini huku kawekewa bastols kichwani.
Makamu wa Rais wametumia platform ya chama kumbinya ndio akajiuzulu mwenyewe.
Unadhani kwa nini Ccm Rais lazima awe ni mwenyekiti wa chama? Yani anapewa nguvu serikalini na kwenye chama.
Justice delayed is Justice denied.Baada ya miaka saba Mahakama ya Rufani ya Tanzania hatimaye imeweka nukta na kuthibitisha rasmi kuwa hatua ya kumwondoa madarakani aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Juma Assad, mnamo Novemba 2019, ilikuwa ya kimakosa na kinyume kabisa cha Katiba ya Nchi.
Hukumu hiyo iliyosomwa na Jaji Sehel kwa niaba ya jopo la Majaji watano waliosikiliza Rufaa ya Madai Namba 176 ya Mwaka 2023 jana, Oktoba 6, 2026 imebainisha kuwa Ofisi ya CAG ilivunjiwa heshima na ulinzi wake wa kikatiba pale Mamlaka ya Uteuzi ilipomtengua Prof. Assad kabla ya kufikisha umri wa kustaafu wa miaka 65.
Shauri hilo lililofunguliwa na mwanasiasa Zitto Zuberi Kabwe, lilikuwa likipinga Kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma (PAA) cha Mwaka 2008 kilichotumiwa na Serikali kuweka ukomo wa miaka mitano wa kuhudumu kwa CAG.
Kwenye uamuzi huo wa kihistoria, Mahakama ya Rufani imetamka wazi kuwa Bunge halina mamlaka ya kutunga sheria yoyote inayopunguza kinga na ulinzi wa ajira aliopewa CAG ndani ya Ibara ya 144(1) ya Katiba. Mahakama imesisitiza kuwa CAG anaweza kuondolewa madarakani kwa njia mbili tu: kufikisha umri wa miaka 65 ya kustaafu au kupitia Tume Maalum (Tribunal) pindi anaposhindwa kutekeleza wajibu wake au kupoteza sifa.
Aidha, Hukumu hii inakuja kama fundisho na kielelezo kikubwa cha ukomavu wa mhimili wa Mahakama nchini katika kulinda Katiba dhidi ya maamuzi au sheria zisizozingatia misingi mikuu ya nchi zilizofanyika huko nyuma.
Pamoja na kubainisha kuwa utenguaji huo ulikuwa batili kikatiba tangu siku ya kwanza, Mahakama ya Rufani imezingatia misingi ya kisheria ya kulinda utendaji wa shughuli za Serikali (doctrine of operative fact), ikibainisha kuwa maamuzi na kazi zote zilizofanywa na CAG aliyefuata zinaridhiwa kisheria ili kuzuia mkwamo wa kiutendaji na ombwe la kiuhasibu katika Serikali.
Uamuzi huo unasimama kama ushindi mkubwa wa utawala wa sheria, ukirejesha heshima ya kikatiba ya Ofisi ya CAG na kuweka kinga imara kwa viongozi wa vyombo vya kikatiba kwa miaka ijayo.
Source: Mwanahalisi, Royal TV Plus
Thubutuuuuu !!Hivi jiwe bado angekuwa hai na yuko madarakani,mahakama yetu ingekuwa huru kutoa hii hukumu?
Hawa wana utaratibu tofauti ambao ni wa kisiasa.Spika? Makamu wa Rais? Havipo kwenye Katiba? Kwanza ulishaambiwa Katiba ni kijitabu tu.
Usijisahaulishe hapa.
Hii sentesi yako ya mwisho ndio ukweli na uhalisia wenyewe.Ndio maana nimekuuliza, Rais Akiamua kumfurusha huyo CAG anashindwa? Umebaki na hoja zako uchwara tu.
Sasa km Spika, mkuu wa muhimili unaojitegemea, anawekewa bastola ajiuzuru, kitashindikana nini huyo CAG kufurushwa??
Makamu wa Rais kuondolewa kupitia chama, si ndio hicho kijitabu kimeweka?
Na umejikamata mwenyewe kuwa Rais anapewa kila idara awe kiongozi, ili awe na uwezo wa kufurusha asio wahitaji.
Kwanza lini Katiba ilifuatwa? Hata hapo mahakamani penyewe, mbona case za wakati huu hazifuatwi sheria, wanabumba bumba kuogopa rungu la mteule wao, baadae akitoka madarakani ndipo wajifanye wanafuata haki na sheria. Si ni upuuzi huu sasa. Lol.
Wao waseme hili la Assad lina public interest na awamu hii, wala wasijifanye wao wako sahihi, ni UONGO.
Hakika kabisaa.Hii sentesi yako ya mwisho ndio ukweli na uhalisia wenyewe.
Umemaliza kila kitu.
"Wao waseme hili la Assad lina public interest na awamu hii, wala wasijifanye wao wako sahihi, ni UONGO."
Kwani wa kisiasa au tofauti, si inafuatwa katiba au?Hawa wana utaratibu tofauti ambao ni wa kisiasa.
Hapana, alifanya vibaya shetani , muasisi wa utekaji, mauaji, kupotea kwa watu na uchafu woooote unaendelea leoMkuu mbona una hasira sana ulitumbuliwa?
Tanzania rais akitaka kufanya chochote ana uwezo.Huu ni uongo wa wazi kabisaa, hapa ni kutaka kufanya Magufuli aonekane mbaya, japo ni kweli.
Vipi huyu wa sasa akitaka kumfurusha CAG, hawezi?? Si dkk 1 tu anaachia ofisi. Lol.
Jiwe likuwa dikteta haswa na fisadi! Ukiona mtu au kiongozi mkuu anamsumbua CAG, ujue huyo ni fisadi na mwizi wa Mali ya umma.
Hapana, alifanya vibaya shetani , muasisi wa utekaji, mauaji, kupotea kwa watu na uchafu woooote unaendelea leo
Niko tayari kuhukumiwa. Why up to now hakuna uchunguzi wowote wa risasi za Lisu?Eeeh.....tusihukumu, tutahukumiwa