Mahakama: CAG hawezi kuondolewa Madarakani kwa Utashi wa Kisiasa au Ukomo wa Muda wa Bunge

Mahakama: CAG hawezi kuondolewa Madarakani kwa Utashi wa Kisiasa au Ukomo wa Muda wa Bunge

Upo sahihi kabisa.
Namchukia sana Ngosha na nna sababu.
Nilipandishwa Daraja 2016 lile shetani lenu la Chato likanishusha mwezi Mei kwa kisingizio eti akimaliza uhakiki wa vyeti tutapandishwa. Mpk linakufa halikufanya hivyo.
Lilizuia kutupandisha mishahara kwa miaka 6! Yaani mpaka linakufa tulikuwa bado tunalipwa mshahara aliotuacha nao JK.
Huyu Mama alipoingia tu nilipandishwa daraja na kulipwa arrears zote!
So hata wewe upo huru kulipenda hilo shetani lenu la Chato kwa mazuri alokufanyia na kumchukia Samia kwa mabaya alokufanyia
Bora umewakilisha wenzio 😂😂
CHUKI BINAFSI ZINAWASAUMBUA tena kwa marehemu sijui mtapona lini huu ugonjwa maana ukimuita magu fisadi nchi nzima inakuona kichaa
 
Makumbele sasa kama hakuna fidia, wala kutoa adhabu kwa yeyote anayevunja katiba bado kunaombwe kubwa tu. Wanasiasa wanaweza kuvunja katiba kwa makusudi, ukakaa kando kisha mahakama ikaja tu kutafsi kuwa ilipaswa iwe hivi.
 
Hao uliwaowataja wanaweza kuondolewa madarakani kwa kufutwa uanachama wa chama cha siasa licha ya kutajwa kwenye katiba.

CAG sio mwanasiasa kwa nafasi yake hivyo nafasi yake haitenguliwi kama ilivyo kwa VP na Spika. Yaani VP na Spika wanaweza kuondolewa kwenye nafasi zao kwa kikao cha halmashauri kuu ya chama tu.
[/QUOTE

Mkuu, chama Cha siasa hakina mamlaka ya kumfuta kazi makamo wa RAISI.
 
Kwenye ule mdahalo wa Odemba , Khalifa alimueleza chawa Balile kwamba rais ana mamlaka ya kumtoa jaji kwenye mahakama na kumpangia majukumu mengine kwa matakwa yake , hivyo kiuhalisia rais anaweza kumteua jaji na kumuondoa nafasi yake bila moja kwa moja kumvua ujaji maana kuna mchakato wa kuvuliwa ujaji.

Kwa Kenya rais hateui majaji , majaji wanaomba nafasi , wanafanyiwa usaili wa wazi baadae hupelekwa kamati ya kijaji kuchujwa tena ndio huthibitishwa.

Kwa mlolongo huo jaji hawezi kuwa mtumishi wa rais wala kutegemea huruma zake kwa kuvunja katiba ili kumfurahisha mteule.
Halafu huyo Chawa Balile alikua anasema Uteuzi wetu wa majaji ni mzuri kuliko wa Kenya..

Ila nashukuru walimshulikia sawasawa mpaka aibu akajionea mwenyewe..
 
Inasaidia Nini CAG alishaondolewa.....! Mahakama inatakiwa kupewa uwezo wa kutoa Maamuzi hata yanayohusu Maslahi ya Taifa (Wananchi)
Hata kama Rais ndiye mpindishaji wa jambo Hilo.... Hili linawezekana kwenye Katiba Mpya tu.
 
Makumbele sasa kama hakuna fidia, wala kutoa adhabu kwa yeyote anayevunja katiba bado kunaombwe kubwa tu. Wanasiasa wanaweza kuvunja katiba kwa makusudi, ukakaa kando kisha mahakama ikaja tu kutafsi kuwa ilipaswa iwe hivi.
Kwa lugha nyingine hata aliyepo anaweza kuondolewa kama Assad tu na mahakama ikaja kujiumauma kama hivi.

Ndiyo umuhimu wa mahakama huru unapoonekana hapa!
 
Halafu huyo Chawa Balile alikua anasema Uteuzi wetu wa majaji ni mzuri kuliko wa Kenya..

Ila nashukuru walimshulikia sawasawa mpaka aibu akajionea mwenyewe..

Balile ni kubwa jinga!
 
Mtu mweusi ni mnafiki mno hivi JPM angekuwepo wangetoa hukumu kama hii? Naamini kabisa Samia akitoka madarakani usishangae makonda,mwigulu,chalamila,wasira nk wanailaani serikali ya samia kwa kuua watu October 29
 
Hukumu hii imefuta sifa zote za Magufuli kwamba alikuwa anajali wanyonge, hukumu hii inatoa hitimisho kuwa magufuli alikuwa fisadi kwa sababu fisadi ni mtu anayetumia fedha za umma kwa kukiuka taratibu za matumizi ya fedha zilizowekwa kisheria. Magufuli badala ya kdeal na mafisadi wa fedha za umma yeye alideal na CAG. Atubu huko aliko.
Hakua fisadi ila hakujali utawala wa sheria (e.g.kufuata utaratibu wa kibajeti kwenye matumizi ya fedha za umma)..Cha muhimu kwake ilikuwa ni kutekeleza maono yake hata kama yangekinzana na taratibu za kisheria...hivyo, kwa vyovyote mwenendo huu ungekinzana na Assad aliyezoea kutembea kwenye rula.....
 
Mahakama ya Rufani ya Tanzania imetoa uamuzi wa kihistoria unaoweka msingi imara wa ulinzi wa taasisi huru za kikatiba nchini, ikisisitiza kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ana ulinzi kamili wa ajira yake na hawezi kuondolewa madarakani kwa kutumia sheria za kawaida za Bunge au matakwa ya muhula wa miaka mitano.

Desemba hii na katika mwendelezo wa mashauri ya kikatiba yaliyovuta hisia za wengi, Mahakama imebainisha wazi kuwa nafasi ya CAG si ajira ya kawaida ya mkataba au nafasi inayotegemea utashi wa mhimili wa utendaji, bali ni muhimili mkuu wa kikatiba wa kulinda rasilimali za umma unaopaswa kulindwa dhidi ya kuingiliwa na wanasiasa.

Mfumo wa Kikatiba na Mtego wa Sheria ya Ukaguzi (PAA)

Chanzo cha mgogoro huu wa kisheria kilianzia kwenye Kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma (Public Audit Act - PAA) ya mwaka 2008, ambacho kiliweka ukomo wa muhula wa miaka mitano kwa CAG, ukiwa na fursa ya kuongezwa mara moja pekee.

Kifungu hiki ndicho kilichotumiwa na Mamlaka ya Uteuzi kumwondoa aliyekuwa CAG, Profesa Mussa Juma Assad, mnamo Novemba 2019 kwa maelezo kuwa muhula wake wa miaka mitano ulikuwa umeisha, licha ya kwamba alikuwa bado hajafikisha umri wa kustaafu kwa mujibu wa Katiba.

Soma pia >>> Prof. Assad: Kesi yangu ya kutenguliwa iko Mahakama ya Rufani, Mwaka wa Sita haisikilizwi

Katika uchambuzi wa Mahakama, ilibainika wazi kuwa Ibara ya 144(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kwa uwazi kabisa kuwa ukomo wa CAG madarakani unatokana na umri wa kustaafu (miaka 60 au miaka 65 kama ilivyowekwa na sheria za kazi) na si kwa vigezo vya kuhesabu miaka ya muhula (term limit).

Mahakama ilieleza kuwa Bunge lilivuka mipaka yake ya kikatiba pale lilipotunga Kifungu cha 6(1) cha PAA kwa kuongeza sharti la muhula wa miaka mitano. Katiba ililipa Bunge mamlaka ya kubainisha umri wa kustaafu pekee, na si kuvumbua mfumo mpya wa ukomo wa muda unaoweka rehani usalama wa ajira ya CAG.

Kwanini Kuondolewa kwa Prof. Assad Kulikuwa Batili?

Katiba ya Tanzania imeundwa kwa namna inayompa CAG ulinzi wa hali ya juu wa kiofisi (security of tenure), unaofanana na ule wanaopewa Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani. Ibara ya 144 ya Katiba inabainisha kuwa CAG anaweza kuondolewa madarakani kabla ya umri wa kustaafu kwa sababu mbili kuu pekee:
  1. Kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa sababu ya ugonjwa au sababu nyinginezo.
  2. Utovu wa nidhamu au ukiukaji wa maadili ya viongozi wa umma.
Hata hivyo, kuondolewa huko hwezi kufanyika kwa tamko la Rais au utashi wa kisiasa, bali lazima kufuate mchakato huru wa uchunguzi unaofanywa na Tume Maalum (Tribunal) iliyoundwa kisheria, kisha kutoa mapendekezo.

Kwa kuwa Prof. Assad hakuondolewa kwa mchakato wa Tume wala hakuwa amefikisha umri wa kustaafu, Mahakama ilihitimisha kuwa kuondolewa kwake kwa kigezo cha "kuisha kwa mkataba wa miaka mitano" kulikiuka Katiba moja kwa moja na kulikuwa batili tangu mwanzo.

Mfarakano wa Kisheria: Kwanini Assad Hakurejeshwa na Kichere Kubaki Ofisini?

Eneo lililozua mjadala mkubwa miongoni mwa wananchi na wanasheria ni sababu zilizofanya Mahakama isiamuru Prof. Assad arejee ofisini au kutengua uteuzi wa CAG wa sasa, Bw. Charles Kichere.

Mahakama ilifafanua changamoto hiyo kupitia misingi miwili kuu ya kisheria:
  1. Uhalali wa Uteuzi wa CAG wa Sasa: Licha ya kuwa kuondolewa kwa Prof. Assad kulikuwa batili, uteuzi wa Bw. Charles Kichere ulifanyika chini ya Kifungu cha 4 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma (PAA)—kifungu ambacho hakijawahi kutangazwa kuwa ni kinyume cha Katiba. Kisheria, hatua iliyochukuliwa chini ya sheria inayotambulika wakati huo inabaki kuwa halali, na ubatili wa kifungu cha ukomo wa miaka mitano hauharibu moja kwa moja kifungu cha uteuzi.
  2. Kuepuka Mkwamo wa Kikatiba (Dual Incumbency): Mahakama ilibainisha kuwa kuamuru Prof. Assad arejeshwe madarakani wakati kuna CAG mwingine aliyetawazwa kisheria kungetengeneza mgogoro mkubwa wa kikatiba wa kuwa na wakuu wawili wanaotambulika kwenye taasisi moja ya ukaguzi.
  3. Nafasi ya CAG si Ajira Binafsi ya Fidia: Mahakama ilisisitiza kuwa kesi za kikatiba hazilengi kufidia maslahi binafsi ya mtu aliyepatwa na madhara ya kiofisi (kama vile kudai kurejeshwa kazini au kulipwa fidia ya ajira), bali zinalenga kutoa tafsiri ya kisheria na kulinda Katiba kwa maslahi ya umma mzima.
Hukumu hii inaacha alama kubwa katika Mfumo wa Sheria na Utawala Bora nchini Tanzania kwa mambo makuu yafuatayo:
  • Kuimarika kwa Utawala wa Sheria (Supremacy of the Constitution): Imetuma ujumbe mzito kwa Bunge na Muhimili wa Utendaji kuwa sheria yoyote itakayotungwa chini ya Katiba haitakuwa na nguvu kama inamnyima kiongozi wa kikatiba hifadhi ya ajira yake iliyowekwa na Katiba Mama.
  • Uhuru wa Taasisi ya CAG: Hakuna CAG wa sasa au wa baadaye atakayefanya kazi kwa hofu ya kufukuzwa au kuondolewa pindi muhula wa miaka mitano unapotimia, maana sheria hiyo sasa ni mti mkavu. CAG ana uhuru wa kukagua na kutoa ripoti bila kuogopa kukatishwa tamaa na shinikizo za kisiasa.
  • Ulinzi wa Rasilimali za Umma: Ili kuisimamia Serikali ipasavyo, CAG anahitaji ulinzi usiotikisika. Maamuzi haya yanamrejeshea CAG utulivu wa kufanya kazi kwa mujibu wa taaluma na kanuni za kimataifa (kama Azimio la Lima na Mexico kuhusu uhuru wa taasisi za ukaguzi).
Licha ya kuwa Prof. Mussa Assad hakurejea kwenye kiti cha CAG, ushindi wa kesi hii ni wa wananchi na Katiba ya nchi. Mahakama imeweka mpaka ulio wazi: Wadhifa wa CAG si nafasi ya kisiasa, na hakuna mtawala anayeweza kumwondoa njiani nje ya utaratibu uliowekwa na Katiba.
So atatakiwa kufidiwa
 
Mtu mweusi ni mnafiki mno hivi JPM angekuwepo wangetoa hukumu kama hii? Naamini kabisa Samia akitoka madarakani usishangae makonda,mwigulu,chalamila,wasira nk wanailaani serikali ya samia kwa kuua watu October 29
Sahihi kabisa
 
Bora umewakilisha wenzio 😂😂
CHUKI BINAFSI ZINAWASAUMBUA tena kwa marehemu sijui mtapona lini huu ugonjwa maana ukimuita magu fisadi nchi nzima inakuona kichaa
Hiyo fisadi umesema wewe.
Lile ni shetani haswa
 
Haikumpa mamlaka. Alifanya kinyume cha katiba. Mbona Samia anateka na kuua? Katiba imempa mamlaka hayo? Tatizo la Tanzania ni watanzania wenyewe. Wananchi wamekaa na kuachia watawala wafanye watakalo.
Mamlaka hayo wanayo, ndio maana wanafanya, wewe mbona humuondoi CAG, km hakuna mamlaka kwa hao marais?
 
Hao uliwaowataja wanaweza kuondolewa madarakani kwa kufutwa uanachama wa chama cha siasa licha ya kutajwa kwenye katiba.

CAG sio mwanasiasa kwa nafasi yake hivyo nafasi yake haitenguliwi kama ilivyo kwa VP na Spika. Yaani VP na Spika wanaweza kuondolewa kwenye nafasi zao kwa kikao cha halmashauri kuu ya chama tu.
Naomba nijibu hili, Samia akitaka kumfurusha Kichere sasa hivi anaweza au hawezi?
 
Tafsiri ya Mahakama ni kwamba Prof Asad alionewa. Lakini kwa mazingira ya sasa hawezi yeye binafsi kufaidika na hukumu hiyo

Natamani mahakama ziwe zinatoa hukumu kwa wakati kwani haki iliyocheleweshwa ni haki iliyonyimwa

Hongera Tanzania, pole na hongera pia Profesa Juma Asad
Haki iliocheleweshwa ni haki ilionyimwa.
 
Sina haja ya kuhangaika na wewe, umeshajiweka wazi. Yaan kuanzia sasa huwezi ona nahadaika na wewe.
Em endelea kudeveleka na awamu hii. Wakati wako wa kudemka.
Kama hawakujiuzulu tuthibitishie hapa usihamishe magoli
 
Back
Top Bottom