BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Ndugu yangu mmoja alishtakiwa kwa uhujumu uchumi akituhumiwa kukwepa kodi kwenye biashara zake. Lakini yeye anadai ni kesi ya kisiasa. Mwaka 2015 aliombwa kusupport kampeni za CCM akakataa lakini alifadhili kampeni za UKAWA. Anaamini hiki ndicho kilichomponza.
Mwaka 2018 alikamatwa na baadhi ya biashara zake kufungwa, na nyingine zikashindwa kujiendesha kutokana na makadirio makubwa ya kodi.
Baada ya kukaa gerezani miaka miwili akaona bora akiri ili atoke (the lesser evil). Wakati wa majadiliano na DPP akatakiwa kulipa zaidi ya 200M. Akakubali kufilisi biashara zake chache zilizobakia ili "kununua" uhuru wake.
Mwaka jana tulimtembelea gerezani mimi na Dr. Cyrilo. Tukamuuliza kwanini umeamua kukiri? Huoni itakuwekea doa? Kuna nchi utazuiwa kwenda kwa sababu ya "criminal record" ya uhujumu uchumi. Kuna fursa za biashara utashindwa kupata. Kwanini usingepambana ushinde badala ya kukiri.
Huku akilengwalengwa na machozi akajibu, nachotaka kwa sasa ni kuwa huru tu. Nikishatoka hiyo "criminal record" anaweza kuja Rais mwingine akaifuta, huwezi jua. Tukaagana, akarudi zake nyuma ya nondo.
Licha ya kukiri na kuwa tayari kulipa (plea burgaining) lakini bado hakuachiwa. Aliambiwa jalada bado lipo kwa DPP.
Wiki iliyopita amefutiwa mashtaka yote na kuachiwa huru, bila kulipa chochote. Siku anaachiwa wala hakujua kama angeachiwa. Ilitumwa "remove order" gerezani, akaenda mahakani bila kubeba chochote maana haikua siku ya kesi. Hata wakili wake hakuwepo.
Miguuni alivaa kandambili. Alipofika mahakamani akaambiwa, Jamhuri imekufutia mashtka yote na haina nia ya kuendelea na kesi. Akadhani ni mtego ili wamkamate tena. Akajaribu kutoka nje ya mahakama, lakini hakuna mtu aliyehangaika nae.
Akaita taxi, ikampeleka nyumbani. Mkewe akapata suprise ambayo hakuitegemea. Akaanguka, alipoamka akaanza kulia. Watoto walipomuona baba yao nao wakalia. Majirani wakaja na kumkumbatia, wakilia. Nyumba ikatawala machozi.
Hii nchi imepitia kipindi kigumu sana. Kuna jinsi Mungu anamtumia mama Samia kuponya majeraha na kuokoa mioyo iliyopondeka. Biblia inasema Haki huinua taifa bali dhambi ni aibu ya watu wowote (Mithali 14:34)!
Malisa GJ