Mahakama hazikuwa zikitenda haki kuhusu kesi za Uhujumu Uchumi

Kutoka kwa Malisa G

Nimesoma nimeishia kutetemeka kwa hasira mwili nzima
[emoji1313][emoji1313][emoji1313]

Ndugu yangu mmoja alishtakiwa kwa uhujumu uchumi akituhumiwa kukwepa kodi kwenye biashara zake. Lakini yeye anadai ni kesi ya kisiasa. Mwaka 2015 aliombwa kusupport kampeni za CCM akakataa lakini alifadhili kampeni za UKAWA. Anaamini hiki ndicho kilichomponza.

Mwaka 2018 alikamatwa na baadhi ya biashara zake kufungwa, na nyingine zikashindwa kujiendesha kutokana na makadirio makubwa ya kodi.

Baada ya kukaa gerezani miaka miwili akaona bora akiri ili atoke (the lesser evil). Wakati wa majadiliano na DPP akatakiwa kulipa zaidi ya 200M. Akakubali kufilisi biashara zake chache zilizobakia ili "kununua" uhuru wake.

Mwaka jana tulimtembelea gerezani mimi na Dr.Cyrilo. Tukamuuliza kwanini umeamua kukiri? Huoni itakuwekea doa? Kuna nchi utazuiwa kwenda kwa sababu ya "criminal record" ya uhujumu uchumi. Kuna fursa za biashara utashindwa kupata. Kwanini usingepambana ushinde badala ya kukiri.

Huku akilengwalengwa na machozi akajibu, nachotaka kwa sasa ni kuwa huru tu. Nikishatoka hiyo "criminal record" anaweza kuja Rais mwingine akaifuta, huwezi jua. Tukaagana, akarudi zake nyuma ya nondo.

Licha ya kukiri na kuwa tayari kulipa (plea burgaining) lakini bado hakuachiwa. Aliambiwa jalada bado lipo kwa DPP.

Wiki iliyopita amefutiwa mashtaka yote na kuachiwa huru, bila kulipa chochote. Siku anaachiwa wala hakujua kama angeachiwa. Ilitumwa "remove order" gerezani, akaenda mahakani bila kubeba chochote maana haikua siku ya kesi. Hata wakili wake hakuwepo.

Miguuni alivaa kandambili. Alipofika mahakamani akaambiwa, Jamhuri imekufutia mashtka yote na haina nia ya kuendelea na kesi. Akadhani ni mtego ili wamkamate tena. Akajaribu kutoka nje ya mahakama, lakini hakuna mtu aliyehangaika nae.

Akaita taxi, ikampeleka nyumbani. Mkewe akapata suprise ambayo hakuitegemea. Akaanguka, alipoamka akaanza kulia. Watoto walipomuona baba yao nao wakalia. Majirani wakaja na kumkumbatia, wakilia. Nyumba ikatawala machozi.

Hii nchi imepitia kipindi kigumu sana. Kuna jinsi Mungu anamtumia mama Samia kuponya majeraha na kuokoa mioyo iliyopondeka. Biblia inasema Haki huinua taifa bali dhambi ni aibu ya watu wowote (Mithali 14:34).!
 
Ni kweli wafanyabiashara wengi walikuwa wanazingua Ila approach za Jiwe zilikuwa za ovyo Sana , zenye kukomoa.....!! Tatizo ni katiba mianya ya utakatishaji pesa Kwa wafanyabiashara na machakato wake kisheria wa kuwawajibisha haupo real ....badala ya kukomaa kuleta katiba mpya ili impe uhalali wa kushughughulikia yeye akaamua kuwa anajiamulia tuuu, mwisho wa sku hzi lawama zote zinamwangukia
 
Mbona inafahamika kuwa alikuwa muhutu wa siasa kali za mauaji!
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Mi personally magufuli alichukua 99% ya hela yangu akaniachia one percent! Hela hutafutwa but am happiest man the guy died.
 
Na mimi nitunge ya kwangu??!!?..maana nami nina kipaji cha utunzi wa stori na hadithi za kusisimua
 
Kwa trend inayoelekea sasa kuna haja ya ku question credibility ya watoa hukumu wetu so sad.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Ni kweli wafanyabiashara wengi walikuwa wanazingua Ila approach za Jiwe zilikuwa za ovyo Sana , zenye kukomoa.....!! Tatizo ni katiba mianya ya utakatishaji pesa Kwa wafanyabiashara na machakato wake kisheria wa kuwawajibisha haupo real ....badala ya kukomaa kuleta katiba mpya ili impe uhalali wa kushughughulikia yeye akaamua kuwa anajiamulia tuuu, mwisho wa sku hzi lawama zote zinamwangukia
Magufuli hakuwa na simile kwenye issue ya kodi na biashara haramu.

Mwaka 2015 Nilikuwa nafanyakazi kwenye NGO's huko vichakani, nikafanikiwa kufanya janja fulani kupitia shughuli hivohivo za Asasi za kiraia nikapiga million of money ikaja kubumbuluka 2016 ila nilifanikiwa kuwahi kukimbia kwaiyo sikukamatwa ila A/C zote zilifungwa si ya NGO wala yangu binafsi mpaka leo sijawah kufatilia nahakika na hela walichukua ila nakiri wazi kuwa simlamu mtu cos kweli nilijipatia pesa kwa njia haramu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee ndicho ambacho umeona kinafaa kutuandikia siku ya leo, very interesting [emoji28]
 
Ndugu yangu mmoja alishtakiwa kwa uhujumu uchumi akituhumiwa kukwepa kodi kwenye biashara zake. Lakini yeye anadai ni kesi ya kisiasa. Mwaka 2015 aliombwa kusupport kampeni za CCM akakataa lakini alifadhili kampeni za UKAWA. Anaamini hiki ndicho kilichomponza.

Mwaka 2018 alikamatwa na baadhi ya biashara zake kufungwa, na nyingine zikashindwa kujiendesha kutokana na makadirio makubwa ya kodi.

Baada ya kukaa gerezani miaka miwili akaona bora akiri ili atoke (the lesser evil). Wakati wa majadiliano na DPP akatakiwa kulipa zaidi ya 200M. Akakubali kufilisi biashara zake chache zilizobakia ili "kununua" uhuru wake.

Mwaka jana tulimtembelea gerezani mimi na Dr.Cyrilo. Tukamuuliza kwanini umeamua kukiri? Huoni itakuwekea doa? Kuna nchi utazuiwa kwenda kwa sababu ya "criminal record" ya uhujumu uchumi. Kuna fursa za biashara utashindwa kupata. Kwanini usingepambana ushinde badala ya kukiri.

Huku akilengwalengwa na machozi akajibu, nachotaka kwa sasa ni kuwa huru tu. Nikishatoka hiyo "criminal record" anaweza kuja Rais mwingine akaifuta, huwezi jua. Tukaagana, akarudi zake nyuma ya nondo.

Licha ya kukiri na kuwa tayari kulipa (plea burgaining) lakini bado hakuachiwa. Aliambiwa jalada bado lipo kwa DPP.

Wiki iliyopita amefutiwa mashtaka yote na kuachiwa huru, bila kulipa chochote. Siku anaachiwa wala hakujua kama angeachiwa. Ilitumwa "remove order" gerezani, akaenda mahakani bila kubeba chochote maana haikua siku ya kesi. Hata wakili wake hakuwepo.

Miguuni alivaa kandambili. Alipofika mahakamani akaambiwa, Jamhuri imekufutia mashtka yote na haina nia ya kuendelea na kesi. Akadhani ni mtego ili wamkamate tena. Akajaribu kutoka nje ya mahakama, lakini hakuna mtu aliyehangaika nae.

Akaita taxi, ikampeleka nyumbani. Mkewe akapata suprise ambayo hakuitegemea. Akaanguka, alipoamka akaanza kulia. Watoto walipomuona baba yao nao wakalia. Majirani wakaja na kumkumbatia, wakilia. Nyumba ikatawala machozi.

Hii nchi imepitia kipindi kigumu sana. Kuna jinsi Mungu anamtumia mama Samia kuponya majeraha na kuokoa mioyo iliyopondeka. Biblia inasema Haki huinua taifa bali dhambi ni aibu ya watu wowote (Mithali 14:34).!

Malisa GJ
Criminal record huwa inafutwa na rais?
 
Aisee ndicho ambacho umeona kinafaa kutuandikia siku ya leo, very interesting [emoji28]
Ni ukweli wangu nilifanya ayo madudu sasa kama kuna mtu analalamika pia aseme ukweli wake akijipatia pesa kwa njia gani? Sema inahitaji ujasiri kisema hasa kwa ao watu maarufu lakini mimi hapa jf nani ananijua? Ila ukweli ndiyo uo na nilikiambia nakumbuka ilikuwa jumamos kuu ndiyo nilichomoka na siku ileile ilikuja Noah mchana nikipoishi kuja kunidaka kumbe mwanzao nilisha chpmoka tangia saa kumi na moja alfajiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani hadi machozi yamenilenga lenga! Inauma sana kuona mtu anatendewa uovu wa namna hii kwa kweli!

Hivi waliokuwa wanatenda huu uovu bado wapo tu wanaangalia hata hawawaombi watanzania msamaha kweli?

Mama kweli Mungu aendelee kukutuma.kuponya mioyo ya watanzania! Sijui ingekuwaje ule utawala ungendeelea hadi 2025 na bado kuna watu walikuwa na kampeni ya kudumu kwenye utawala milele, dah,

Ahsante Mungu kwa kuona machozi ya watanzania!
 
Aisee ndicho ambacho umeona kinafaa kutuandikia siku ya leo, very interesting [emoji28]
Pia na nakumbuka ndiyo uhakiki wa NGO ukaanza ikabidi kama NGO haiwasilishi taarifa ya mahesabu ya mwaka na kulipa ada yake kila mwaka inafutwa na kweli nyingi zilifutwa cos zilikuwa za ujanja ujanja tu na wengi walikuwa hawapeleki taarifa za hesabu za mwaka wala kulipa ada zao tena Tsh 150,000/= kwa local NGO ila sasa ukiwasikia wanavyolalamika kufunguwa kwa NGO zao..!! Eeeh kiukweli hatulipendi taifa letu kwakweli hatuko tayari kuumia kwaajili ya taifa letu kiujumla.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani hadi machozi yamenilenga lenga! Inauma sana kuona mtu anatendewa uovu wa namna hii kwa kweli!

Hivi waliokuwa wanatenda huu uovu bado wapo tu wanaangalia hata hawawaombi watanzania msamaha kweli?

Mama kweli Mungu aendelee kukutuma.kuponya mioyo ya watanzania! Sijui ingekuwaje ule utawala ungendeelea hadi 2025 na bado kuna watu walikuwa na kampeni ya kudumu kwenye utawala milele, dah,

Ahsante Mungu kwa kuona machozi ya watanzania!
Acheni maigizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee ndicho ambacho umeona kinafaa kutuandikia siku ya leo, very interesting [emoji28]
Nakumbuka Dkt Halison Mwakyembe alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria kipindi hicho akilizungunzia ili sakata langu ila igeneral likalipotiwa katika gazeti la Mwananchi na alilizungunzia cos yule Mkurugenzi wa Shirika lililokapa jle pesa wanafahamiana vizuri na Mwakyembe na waliwahi kufanya kazi sehemu moja hivo sikushangaa kama alimwambia na kumuomba ushirikiano rafikiyake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wangalipo wengi yule Mura alisema itachukua miaka 2.

Kazi kweli kweli!
Habari ya ''mujini'' ilikuwa ama uhujumu uchumi au utakatishaji fedha au yote kwa pamoja. Wakikukosa kabisa wanakuwekea noti ya elfu tano njiani ukidhani una bahati na kuokota unaambiwa umetenda kosa la kutakatisha pesa.
 
Ungetutajia jina kabisa lakini lazima tuwe wazi ..wafanyabiashara wamepiga sana na kuiba hela ..nchi hii ilikuwa kama gombania goli..wengi walitumia viongozi wa kisiasa wa tawala na hata upinzani kutekeleza wizi.inawezekana kabisa ushahidi ukawa haupo au kupotezwa lakini ndani ya mioyo yao wanajua waliiba kiasi gani na madhara waliyopata wengine kama ukosefu wa maji au huduma za hospitali nk vilisababisha vifo vya watu...watoke kimya kimya maana mambo yao yalikuwa wazi huku mtaani kipindi kuiba au kufisadi ni sifa.
Mimi binafsi sikatai kuna watu walikuwa wamezoea kuishi kwa ujanja wa upigaji tena wanashirikiana na viongozi wa serikali. Lakini ni vizuri mtu anapokamatwa kesi iendeshwe kwa uhalali na dhamana iwepo. Kama hakukuwa na ushahidi basi angetengeneza system nzuri na kuanza upya.
 
Wengi sana Mkuu na wameporwa mamilioni yao kama si mabilioni na yule dhalimu mwendazake na washirika wake. Huyu mmoja tu walitaka kumpora milioni 200!!!! Bado kuna wale wa maduka ya kuuza FOREX Arusha na Dar ambao nao waliporwa pesa nyingi sana zikiwemo T shs.
Nimesikitika sana sijui ni Watanzania wangapi wanateseka Magerezani kwa kubambikiwa makosa na Wadhalimu wa Awamu ya laana.
 
Back
Top Bottom