Mahakama hazikuwa zikitenda haki kuhusu kesi za Uhujumu Uchumi

Habari ya ''mujini'' ilikuwa ama uhujumu uchumi au utakatishaji fedha au yote kwa pamoja. Wakikukosa kabisa wanakuwekea noti ya elfu tano njiani ukidhani una bahati na kuokota unaambiwa umetenda kosa la kutakatisha pesa.

Walikuwa kama wamepagawa. Kidogo nikiazima kutoka kwa beberu - "they're like possessed by the devil himself!"

Hiiiiii bagosha!
 

Huyo ndiyo tukiaminishwa ana legacy ya kulindwa. Tukisukumwa kuridhia jiwe day na yeye kuwa baba wa taifa.

Washindwe, watepete na kubaki na m@vi yao.

Katelefoni swahiba wake mkuu angalipo kule anafanya nini Yarabi?
 
Reactions: BAK
Huu msamiati wa Uhujumu Uchumi una shida sana, ulianza na Mwl Jk, PM akiwa Edo, kweli watu walienda ndani baadae akaja mzee Ruksa na wengine hadi awamu jumuishi, sasa kumekuja awamu juimushi .
Huu msamiati UFUTWE kwanza hatuna watu wa namna hiyo Tz,
Tunao wafanyabiashara wazalendo wa kwetu, pia wawekezaji wenye uweledi hizi hujuma zinatoka waaapi?

Watu watoke, anagalau mtaani tuweke heshima ajira zimwagike,
Nani anasema huyu anahujumu, Umemuaona? Thibitisha.
Nani anaweza kuiba vya kwao? Hamna
Nani anaweza ku risk afunge safari toka mbali kwa lengo la kuhujumu serkali na watu wake? Hakuna

Msamiati huu ufutwe. Wivu tu

Huwezi kupora mali halali ya mwenzako ukabaki salama
 
Reactions: Qwy
Wale wapuuzi wake ndani ya chama na Serikali eti walitaka TUMUENZI!!! Una enzi kipi kwa mtu muovu kama yule!?

Huyo ndiyo tukiaminishwa ana legacy ya kulindwa. Tukisukumwa kuridhia jiwe day na yeye kuwa baba wa taifa.

Washindwe, watepete na kubaki na m@vi yao.

Katelefoni swahiba wake mkuu angalipo kule anafanya nini Yarabi?
 
Wale wapuuzi wake ndani ya chama na Serikali eti walitaka TUMUENZI!!! Una enzi kipi kwa mtu muovu kama yule!?

Walivyopoa sasa hivi bila shaka busara imeanza kuwarejea na kutambua kuwa wamepwelewa.

Bado tuna yetu Mama itabidi atupe kwani twayaomba kwa nia njema na kumsaidia yeye pia:

1. Ripoti ya tume za CAG BOT na TPA.
2. Hitajio la Katiba mpya.
3. Mikutano yake na vyama vya siasa.
4. Haki kwa wote waliodhulumiwa awamu ile.

Moja moja tutalidondoa kwa mapana na marefu yake. Tulishaumwa na nyoka. Hatuwezi kuwaweka rehani watoto au watoto wa watoto wetu tena.

Hakuna ajizi, maana hiyo ni nyumba ya njaa.

La Corona amekishaliwekea mwelekeo. Hapo tunatarajia takwimu kuelekea chanjo.

Mola na amjaliei afya, utashi na uthubutu Mama yetu huyu dhidi ya yaliyowashinda.

Nisiache kumsalimia Mama kwa jina la JMT.
 
Reactions: BAK
Yule muovu kaondoka kwa laana ya machozi ya wengi,angepewa haki ya kugawa pumzi duniani wallahi hakuna angebakia hai.Hata kama ungebakia hai ungeinunua kwa bei kubwa Sana.
 
Kuna kapewa uhujumu uchumi kwa sababu ya elf 5 na akalipa milioni 15 Ili kununua uhuru wake sembuse hayo mamilioni.
 
Hivi tunawezaje kuacha mambo haya bila kulipa visasi ?
 
Kwa nini chama tawala huwa kinafikiri ni lazima wafanyabiashara wakichangie?

Chini ya jiwe walijimilikisha nchi na vyote vilivyomo. Walikuwa wakituona kama mifugo tu.

Tulipo upepo umegeuka. Tunataka haki sawa kwa wote na vikorombwezo vyake vyote. Wala hatutanii.

Tunayemwelewa Mama. Katelefoni hata akirudi Ruangwa wala hatuna pressure naye iwapo hatatajwa kwenye kadhia za kina Ben, Azory, na wote waliopotea.

Kwani haki sawa ni nini basi?
 
Reactions: BAK
Sio tu uhujumu uchumi, chochote kile kilichokuwa kinaanza na neno vita hakikiwa fair, ile vita ya madwa ya kulevya ya DAB isikie tu, nigekuwa ndani sasa hivi kama sio kuhamisha makazi kwa muda usiojulikana🤣
 
Hivi Mustapha Sabodo yupo wapi kwa sasa?

Enzi za Kikwete Mr Sabodo alikuwa anatoa msaada wa hela, kwa CCM na Upinzani. Ilikuwa wazi kabisa, wala haikuwa siri. Alikuwa neutral.

Tangu alipoingia jiwe hakusikika tena! Yupo wapi kwa sasa?
 
Sio tu uhujumu uchumi, chochote kile kilichokuwa kinaanza na neno vita hakikiwa fair, ile vita ya madwa ya kulevya ya DAB isikie tu, nigekuwa ndani sasa hivi kama sio kuhamisha makazi kwa muda usiojulikana🤣

Pole sana mkuu.

Kenya wanawaita wakora. Wale jamaa walikuwa wakora tu.

Wakora - wezi, vibaka, majambazi, mabazazi, Mabedui, majahili, mafedhuli, nk. Yaani mkuluro wote huo.

Huna utu, huruma wala hujali haki za wengine, wewe ni mtu wa namna gani?
 
Nchi ina usalama wa taifa halafu mtu bogazi kama Magufuli anaruhusiwa kugombea urais!!!.
 
Hivi kile kipengele ch " Awe na akili timamu" huwa wanakifuata kweli?
Maaana MAGUFULI hakuwa na akili timamu.
 
Acha uongo mbona huyo ndugu yako humtaji jina. Mnatunga uongo kumdemonise magufuli na kujidai samia ni mtu wenu wapinzani. Mijitu ilikua inafanya magendo au kukwepa kodi mnajifanya ndio wema. Unafikiri bila kodi nchi itafanyaje maendeleo. To hell na li chadema lenu. Jpm yupo tu wala hamuwezi kufuta legacy yake kwa uongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…