Mahakama imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa ATCL, David Mataka kifungo cha miaka 6 au faini ya milioni 35

Mahakama imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa ATCL, David Mataka kifungo cha miaka 6 au faini ya milioni 35

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka na mwenzake kulipa faini ya Sh35 milioni kila mmoja au kutumikia kifungo cha miaka sita jela.

Mbali na Mattaka, mshtakiwa mwingine ni Elisafi Mathew aliyekuwa kaimu ofisa mkuu kitengo cha fedha cha ATCL.

Uamuzi huo umetolewa na Mahakama baada ya upande wa Jamhuri kuthibitisha mashtaka dhidi yao pasipo kuacha shaka.

Akitoa hukumu, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa alimuachia huru William Haji aliyekuwa mkaguzi mkuu wa Hesabu za ndani ATCL, baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka dhidi yake.

Mahakama pia imeamuru Mattaka na Mathew kulipa hasara waliyoisababishia ATCL katika ununuzi wa magari chakavu 26 ambayo ni Dola 143,442.75 za Marekani ndani ya mwezi mmoja.

Washtakiwa walitiwa hatiani katika mashtaka sita yaliyokuwa yakiwakabili ya kula njama, matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara Serikali.

Chanzo: Mwananchi

Zaidi...

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka na mwenzake Elisaph Mathew, aliyekuwa Kaimu Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha cha ATCL kwenda jela miaka sita kila mmoja au kulipa faini ya jumla ya Sh. Milioni 70 (Milioni 35 kila mmoja).
Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka alipofika leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kutolewa hukumu.

Mbali na adhabu hiyo, mahakama pia imewaamuru watuhumiwa hao kulipa hasara waliyoisababishia ATCL katika ununuzi wa magari chakavu 26 ambayo ni dola za Marekani 143,442.75 sawa na Sh. Milioni 322.

Aidha mahakama hiyo imemuachia huru William Haji ambaye aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani za ATCL.

Mattaka alipandishwa kizimbani mara ya kwanza mwaka 2008 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akituhumiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi kwa kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. bilioni moja zilizotumika kununua magari machakavu.

Soma: David Mataka apandishwa kizimbani kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi

DJmJigOX0AA8Ylf.jpg large.jpg
 
Tulia tafuta taarifa kamili, waliohukumiwa ni wawili na kila mmoja analipa 35 million au 6 years jela
 
sijaelewa miaka 6 au miezi 6, manake kutokana na kosa lake miezi 6 naona ni mchezo, wanasiasa wanatumikia vifungo vya miaka kadhaa mpaka wanaomba dhamana ndio wanatengua, sasa huyu alisababisha mpaka shirika likatetereka mpaka leo halijakaa sawa, miezi 6, duu haya
 
Wanasheria wasom hizi sheria zenu huwa mnazitungaje mtu ana ubadhirifu wa 1Bln then unampa option ya 70M au kifungo kuna uhalisia hapo kwel
 
Hakimu hawezi kutoa kifungo zaidi ya kilichoandikwa kwenye sheria. Ukitaka peleka muswada bungeni ili kukidhi kifungo unachotaka kwa mabilioni yanapoibiwa.

Wanasheria wasom hizi sheria zenu huwa mnazitungaje mtu ana ubadhirifu wa 1Bln then unampa option ya 70M au kifungo kuna uhalisia hapo kwel

Zimepotea 1 bilion. mnamlipisha 70 mil...na mahakimu mkiambia mnachakachua maamuzi ya adhabu mnalalamika kuingiliwa kwenye utendaji wenu. Kitu gani hii!
 
Wenda wazimu hawa yaani 1 bilioni analipa faini ya milioni 70?

Kuna maelezo mengine yakuweza kunishawishi kwamba kilichofanyika ni sahihi kama hakuna maelezo mengine basi kua hakimu makama ya serikali ni bora kesi ziamuliwe na wapiga debe wa ubungo

Amini usiamini, ukihitimu shule ndio utaanza masomo.
 
Back
Top Bottom