Mahakama imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa ATCL, David Mataka kifungo cha miaka 6 au faini ya milioni 35

Kama kuna mtu anahukumu hiyo aweke hapa tuisome. Hii itatusaidia kujua sababu zilizomfanya hakimu kutoa adhabu hii.
Pili kama serikali hajaridhika na hukumu haki ya rufaa ipo wazi kabisa na lazima hakimu aiseme wazi.
Je kosa aliloshitakiwa nalo lina adhabu gani? Kwa sababu hakimu au judge hawezi kutoa adhabu zaidi iliyopo kwenye sheria.
Ukweli ni kwamba sheria zetu nyingi za zamani zilikua soft sana kwenye makosa haya ya rushwa na ufisaidi.
Ila at least government imepata conviction.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka na mwenzake kulipa faini ya Sh35 milioni kila mmoja au kutumikia kifungo cha miaka sita jela.

Mbali na Mattaka, mshtakiwa mwingine ni Elisafi Mathew aliyekuwa kaimu ofisa mkuu kitengo cha fedha cha ATCL.

Uamuzi huo umetolewa na Mahakama baada ya upande wa Jamhuri kuthibitisha mashtaka dhidi yao pasipo kuacha shaka.

Akitoa hukumu, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa alimuachia huru William Haji aliyekuwa mkaguzi mkuu wa Hesabu za ndani ATCL, baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka dhidi yake.

Mahakama pia imeamuru Mattaka na Mathew kulipa hasara waliyoisababishia ATCL katika ununuzi wa magari chakavu 26 ambayo ni Dola 143,442.75 za Marekani ndani ya mwezi mmoja.

Washtakiwa walitiwa hatiani katika mashtaka sita yaliyokuwa yakiwakabili ya kula njama, matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara Serikali.

Chanzo: Mwananchi

Soma: David Mataka apandishwa kizimbani kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi

View attachment 587437
e914bd893ebcfd4f675db6cc8e778489.jpg

Kazi ipo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mheshimiwa wakati ule wa kihenga yuko PPF wanamuziki walikula sana fedha zake sasa wapige donee wamlipie bigboss mataka. Sijui le mutuz alikuwa wapi karibu na le super bilioneaaaz davido mataka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wangemwambia milioni 400 versus miezi mitatu, asingeopt kwenda jela. Milioni 35 huku kapiga zaidi ya Billion moja. Tanzania tuna sheria nzuri sana kwa raia wetu wanyonge
Hukumu, hatujaiona, tunajilisha upepo tu hapq jf.

[emoji106] jela miaka sita
[emoji106] kulipa 35/-mil
[emoji106] kulipa hasara ya usd 140,000/- kurejesha pesa waliyotumia vibaya. Ilipwe ndani ya siku 30 tu

Sasa isipolipwa ndani ya mwezi, what do you expect?

Ni kufilisiwa tu
f67f9aaacab677f445445d59f6fcd432.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka na mwenzake kulipa faini ya Sh35 milioni kila mmoja au kutumikia kifungo cha miaka sita jela.

Mbali na Mattaka, mshtakiwa mwingine ni Elisafi Mathew aliyekuwa kaimu ofisa mkuu kitengo cha fedha cha ATCL.

Uamuzi huo umetolewa na Mahakama baada ya upande wa Jamhuri kuthibitisha mashtaka dhidi yao pasipo kuacha shaka.

Akitoa hukumu, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa alimuachia huru William Haji aliyekuwa mkaguzi mkuu wa Hesabu za ndani ATCL, baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka dhidi yake.

Mahakama pia imeamuru Mattaka na Mathew kulipa hasara waliyoisababishia ATCL katika ununuzi wa magari chakavu 26 ambayo ni Dola 143,442.75 za Marekani ndani ya mwezi mmoja.

Washtakiwa walitiwa hatiani katika mashtaka sita yaliyokuwa yakiwakabili ya kula njama, matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara Serikali.

Chanzo: Mwananchi

Soma: David Mataka apandishwa kizimbani kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi

View attachment 587437
Mkuu badilisha kwenye heading unachanganya. Amehukumiwa miezi sita (heading) lakini kwenye taarifa yenyewe amehukumiwa kifungo cha miaka sita.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka na mwenzake kulipa faini ya Sh35 milioni kila mmoja au kutumikia kifungo cha miaka sita jela.

Mbali na Mattaka, mshtakiwa mwingine ni Elisafi Mathew aliyekuwa kaimu ofisa mkuu kitengo cha fedha cha ATCL.

Uamuzi huo umetolewa na Mahakama baada ya upande wa Jamhuri kuthibitisha mashtaka dhidi yao pasipo kuacha shaka.

Akitoa hukumu, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa alimuachia huru William Haji aliyekuwa mkaguzi mkuu wa Hesabu za ndani ATCL, baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka dhidi yake.

Mahakama pia imeamuru Mattaka na Mathew kulipa hasara waliyoisababishia ATCL katika ununuzi wa magari chakavu 26 ambayo ni Dola 143,442.75 za Marekani ndani ya mwezi mmoja.

Washtakiwa walitiwa hatiani katika mashtaka sita yaliyokuwa yakiwakabili ya kula njama, matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara Serikali.

Chanzo: Mwananchi

Soma: David Mataka apandishwa kizimbani kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi

View attachment 587437
Mahakimu wetu wana matatizo sana.Kosa la billions mtu analipa millioni 35.Huu ni uchakachuaji wa hukumu.Mahakimu wetu bado ni business as usual.Kuna haja ya kumtumbua huyu hakimu.Hayuko pamoja na watanzania kabisa kwenye vita ya uchumi inayoendelea.Watu kama hawa na akina Mataka ndio kila kukicha wanamtupia Rais madongo,haivumiliki.
 
Sheria zipitiwe upya, hukumu nyingi tu hazina uhalisia kabisa.
 
Zimepotea 1 bilion. mnamlipisha 70 mil...na mahakimu mkiambia mnachakachua maamuzi ya adhabu mnalalamika kuingiliwa kwenye utendaji wenu. Kitu gani hii!
soma vizuri ni dola laki na 20 na wameamriwa wazirudishe ndani ya mwezi mmoja
 
Hukumu ya hovyo , WEZI wa kuku miaka 12, Mwizi wa bilioni miezi sita!!!
Duuuu, hebu tuache ushabiki usiyokuwa na tija kwa taifa. Wizi wa kuku miaka 12. Tunaomba ututajie ni mtanzania yupi aliyefungwa kwa kosa hilo. Na hukumu hiyo ilitolewa na hakimu yupi???, na mahakama ipi. Na mwaka gani?? Ili tufuatilie hiyo kesi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka na mwenzake kulipa faini ya Sh35 milioni kila mmoja au kutumikia kifungo cha miaka sita jela.

Mbali na Mattaka, mshtakiwa mwingine ni Elisafi Mathew aliyekuwa kaimu ofisa mkuu kitengo cha fedha cha ATCL.

Uamuzi huo umetolewa na Mahakama baada ya upande wa Jamhuri kuthibitisha mashtaka dhidi yao pasipo kuacha shaka.

Akitoa hukumu, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa alimuachia huru William Haji aliyekuwa mkaguzi mkuu wa Hesabu za ndani ATCL, baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka dhidi yake.

Mahakama pia imeamuru Mattaka na Mathew kulipa hasara waliyoisababishia ATCL katika ununuzi wa magari chakavu 26 ambayo ni Dola 143,442.75 za Marekani ndani ya mwezi mmoja.

Washtakiwa walitiwa hatiani katika mashtaka sita yaliyokuwa yakiwakabili ya kula njama, matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara Serikali.

Chanzo: Mwananchi

Soma: David Mataka apandishwa kizimbani kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi

View attachment 587437
Ana Bahati Kesi ilianza enzi za business as usual. Vinginevyo Ilitakuwa uwe Kesi ya uhujumu uchumi. Anakaa jela. Miaka Sita na akihukumiwa miaka 6 angalau inakuwa 12 yrs. tutanyooka tuu
 
Manji yupo ndani mnalalamika anaonewa, Matajiri wakiachiwa huru mnalalamika!Mnataka nini!
 
Back
Top Bottom