Mahakama imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa ATCL, David Mataka kifungo cha miaka 6 au faini ya milioni 35

Hakimu hawezi kutoa kifungo zaidi ya kilichoandikwa kwenye sheria. Ukitaka peleka muswada bungeni ili kukidhi kifungo unachotaka kwa mabilioni yanapoibiwa.
SubiriJibu,
Umeongea jambo kubwa na la kweli. Wakubwa watunga sheria kama kina Andrew Chenge mbunge hawawezi kutunga sheria / adhabu kali, sana sana wakubwa watajitungia sheria za faini au kinga ya kushtakiwa n.k
 

Samahani sasa tuamini ' figure ' ya katika Headline yako ya miezi 6 au ya katika Content yako ya miaka 6? Nitashukuru nikijibiwa Mkuu.
 
Toka habari zake na Defao zilipovuma, namuona hana maana mtu mzima huyu. Nadhani hii inayompata ni laana ya kuchezea nnya ya mwanaume mwenzie. Itapendeza akifungwa maana huko atakutana na wapakua vyoo wenzie.
 
Afungwe tu no faini , CCM wekeni hata sheria ya kuwanyonga(kama China) hawa watu ili wana CCM (mafisadi) wapungue duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasheria wasom hizi sheria zenu huwa mnazitungaje mtu ana ubadhirifu wa 1Bln then unampa option ya 70M au kifungo kuna uhalisia hapo kwel
Sheria zinatungwa na kinalusinde na maji marefu huko bungeni mkuu
 
Kwahyo mwanasheria anakutana na sheria mahakaman? Ile Miswada kabla haijapelekwa Bungen huwa inaandaliwa na nan?
Inaandaliwa na sirikali kwa kushauriana na ofisi ya mwanasheria mkuu wa sirikali
 
So kumbe mwanasheria anahusika mpaka hapo?
Swadakta kabisa ila unaweza kukuta sheria yenyewe ilitungwa kwa dharura mkuu kama kawaida sasa ikakosa muda wa kusoma tukasema ndiyooo ngoma ikatiki
 
Zaidi ya bilion moja hasara mtu anarudisha milion 35 mtoa mada kama iyo hukumu ipo ivyo kweli basi wamefanya biashara nzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Da sheria hizi bwana

17 PHD these are results
 
Hata wangemwambia milioni 400 versus miezi mitatu, asingeopt kwenda jela. Milioni 35 huku kapiga zaidi ya Billion moja. Tanzania tuna sheria nzuri sana kwa raia wetu wanyonge
 
Zimepotea 1 bilion. mnamlipisha 70 mil...na mahakimu mkiambia mnachakachua maamuzi ya adhabu mnalalamika kuingiliwa kwenye utendaji wenu. Kitu gani hii!

badili kwanza sheria na katiba ya nchi ndio uanze kuwalaumu mahakimu na majaji, Mahakama huhukumu kulingana na sheria za nchi..bila shaka sheria ya nchi ndio imetoa hiyo hukumu sio hakimu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…