KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Katika kuifahamu dhana ya 'Balance and Check' katika mihimili ya Dola kwa maana ya Serikali, Bunge na Mahakama sijawahi kujua hii dhana inafanya vipi katika eneo la Mahakama.
Kwa mfano Bunge linapoisimamia Serikali tunaona Balance and Check na pia Shauri lolote la Serikali au Bunge kupelekwa mahakamani tunaona uwepo wa dhana ya 'Balance and Check' lakini hatuoni popote dhana hii ikitumika kwa mahakama na zaidi dhana inayofanya kazi sana ni maamuzi ya mahakama ndio ya mwisho.
Kwanini Mahakama iwe na maamuzi ya mwisho ikiwa dhana ya Balance and Check inaamimini mihimili yote ni sawa?
Hoja yangu juu ya uwepo wa Chombo maalumu cha kusimamia Mahakama inakuja baada ya malalamiko juu ya chombo hiki kuwa mengi na wanaolalamika ni viongozi. Kwa mfano, Makonda alipokuwa katibu wa NEC wa CCM alilalamika, Jerry Sliaa waziri wa Ardhi na yeye anaonekana kusikitishwa na utendaji wa mahakama kwenye masuala ya Ardhi
Je, hatuoni umuhimu wa kuunda chombo cha kuisimamia Mahakama ili dhana ya Balance and Check itekelezwe kikamilifu kwa mihimili yote ya Dola?