Mahakama kutoa uamuzi wa Kesi ya Halima Mdee na wenzake Desemba 14

Nashangaa misuli ya shingo inavyowatoka sijui wamategmea nini, hawa wasingekuwepo mbowe angekaa akaangalia mademu zake na jamaa zake na watu wake wa karibu akawapa, hakuna kitachobadilika hata hawa wakitolewa
Tanzania siasa za vyama vingi ni maigizo tu.

Siku serikali itafunga ruzuku kwa vyama vya siasa na bunge kupunguza malipo ya mishahara na posho ndipo tutapata wabunge wanoitumikia jamii kiukweli.
 
Tayari kuna maelekezo kwa majaji kuwaharass Chadema tunapokaribia uchaguzi ujao!
CDM jiandaeni wasaliti 19 watashinda na mtaamrishwa kuwapokea!!Au hata kuwalipa!! Saa100 katika uchaguzi ni jambazi mnafiki wa kutisha sana beware
Hizo ni fikra zako tu, upo huru.

Mwanasiasa yupi wa chadema au wa chama kingine chochote cha siasa ambae hanunuliki kwa pesa?
 
Ahsante kwa kuthibitisha mnada wenu wa watu/kisiasa! mapapa wa dunia!
 
Wanaoitumikia jamii kiukweli huwakuti bungeni wala kwenye NGO. Wapo wapo tu mitaani huko.
Kuna kipindi unaandika vitu vya ukweli! Nani aliyeharibu huu utaratibu wa kukosa watumishi wa jamii kuwakilisha jamii!?? Ni jambo serious mno!
 
Hizo ni fikra zako tu, upo huru.

Mwanasiasa yupi wa chadema au wa chama kingine chochote cha siasa ambae hanunuliki kwa pesa?
Unamjua Lissu?
Huyo ni jibu la swali lako.
 
Unamjua Lissu?
Huyo ni jibu la swali lako.
Unafikiri wanaomuweka mjini mpaka akaweza kupiga kelele na kusafoiri kwenda kuripoti kwao nje ya nchi, wanamtumia bure?

Fikiri japo kiduchu.
 
Lissu ni mwanasheria,anafanya kazi,analipwa kwa kazi zake zinazohusu sheria.
Tambua vilevile kua Lissu ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA,hivyo analipwa kwa hicho cheo pia.
Ni mjinga pekee ataamini kua Lissu ni mwanasiasa mwenye PRCE TAG.
JPM huko aliko anamjua Lissu vema.
 
Wakati baadhi ya Walalamikaji hao wameanza kuvaa sare za ccm , huku wengine wakihutubia kwenye Majukwaa ya CCM, imetangazwa kwamba hukumu ya kesi yao dhidi ya Chadema itatolewa Desemba 14 2023.

Ikumbukwe kwamba Halima Mdee na wenzake , akiwemo Dada yangu Sophia Mwakagenda walifungua kesi kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema.

===============

Hatma ya Mdee na wenzake 18 kujulikana Desemba 14, 2023

Desemba 14, 2023 saa nane na nusu mchana Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imepanga kutoa hukumu ya kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Halima Mdee na wenzake 19 ambao walifutwa uanachama katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Uamuzi huo umetolewa Oktoba 24, 2023 na Jaji Cyprian Mkeha wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kupangiwa hukumu.

Wakili wa upande wa wajibu maombi, Wakili Deogratias Mahinyira kwa niaba ya wenzake amesema Hukumu ya kesi hiyo imepangwa kutolewa ikiwa ni baada ya pande zote kukamilisha mawasilisho kama ilivyoelekezwa na Mahakama.

"Shauri leo lilikuwa linakuja kwa ajili maelekezo ya Mahakama (necessary orders), kwa sababu tarehe ya mwisho Mahakama ilikuwa imeeleza baada ya shauri kusikilizwa kwamba leo tuje Mahakama ijiridhishe kama pande zote zimeweza kufanya mawasilisho yake ya mwisho ili Mahakama iweze kupanga tarehe ya uamuzi," amesema Wakili Deogratias Mahinyira.

Halima Mdee ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na wenzake 18 walifungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama, kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama (Judicial Review).

Kesi hiyo ilifunguliwa ikiwa ni muda mfupi baada ya Baraza Kuu la Chadema kuunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho wa kuwafukuza uanachama.

Ikumbukwe Juni 2022 Mahakama Kuu Dar es Salaam ilitupilia mbali maombi ya Halima Mdee na wenzake kutokana na kuwepo kwa kasoro kuhusu jina la mjibu maombi wa kwanza, lakini walifungua shauri ambalo linatarajiwa kutolewa hukumu.

Itakumbukwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson alisema hawezi kutangaza kuwa nafasi za Wabunge hao wa Viti Maalum zipo wazi kabla ya taratibu za Kimahakama kukamilika.
Kesho 14-12-2023 Jaji atakuwa na kazi maalum nje ya Mahakama.Keshokutwa 15-12-2023 Mahakama inafunga shughuli zake mpaka 31-01-2024 , hivyo basi kesi itaahirishwa mpaka 6-2-2024.
 
Kila kitu tunajua , tulishavujishiwa miezi mingi iliyopita
 
Wakati baadhi ya Walalamikaji hao wameanza kuvaa sare za ccm , huku wengine wakihutubia kwenye Majukwaa ya CCM, imetangazwa kwamba hukumu ya kesi yao dhidi ya Chadema itatolewa Desemba 14 2023.

Ikumbukwe kwamba Halima Mdee na wenzake , akiwemo Dada yangu Sophia Mwakagenda walifungua kesi kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema.

===============

Hatma ya Mdee na wenzake 18 kujulikana Desemba 14, 2023

Desemba 14, 2023 saa nane na nusu mchana Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imepanga kutoa hukumu ya kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Halima Mdee na wenzake 19 ambao walifutwa uanachama katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Uamuzi huo umetolewa Oktoba 24, 2023 na Jaji Cyprian Mkeha wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kupangiwa hukumu.

Wakili wa upande wa wajibu maombi, Wakili Deogratias Mahinyira kwa niaba ya wenzake amesema Hukumu ya kesi hiyo imepangwa kutolewa ikiwa ni baada ya pande zote kukamilisha mawasilisho kama ilivyoelekezwa na Mahakama.

"Shauri leo lilikuwa linakuja kwa ajili maelekezo ya Mahakama (necessary orders), kwa sababu tarehe ya mwisho Mahakama ilikuwa imeeleza baada ya shauri kusikilizwa kwamba leo tuje Mahakama ijiridhishe kama pande zote zimeweza kufanya mawasilisho yake ya mwisho ili Mahakama iweze kupanga tarehe ya uamuzi," amesema Wakili Deogratias Mahinyira.

Halima Mdee ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na wenzake 18 walifungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama, kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama (Judicial Review).

Kesi hiyo ilifunguliwa ikiwa ni muda mfupi baada ya Baraza Kuu la Chadema kuunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho wa kuwafukuza uanachama.

Ikumbukwe Juni 2022 Mahakama Kuu Dar es Salaam ilitupilia mbali maombi ya Halima Mdee na wenzake kutokana na kuwepo kwa kasoro kuhusu jina la mjibu maombi wa kwanza, lakini walifungua shauri ambalo linatarajiwa kutolewa hukumu.

Itakumbukwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson alisema hawezi kutangaza kuwa nafasi za Wabunge hao wa Viti Maalum zipo wazi kabla ya taratibu za Kimahakama kukamilika.
Watashinda kesi ili Chadema ikate rufaa na kesi iendelee, sasa itakapoendelea mpaka bunge litakapovujwa wao itabidi waendelee kuwa wabunge kwa sababu kesi yao bado ipo mahakamani au wenye nchi wanaweza wakatuambia bunge halitavunjwa kwa sababu kuna wabunge wenzetu ambao kesi yao ya ubunge bado ipo mahakamani, hivyo likivunjwa watafungua kesi dhidi ya serikali kwa kusitisha ubunge wao kabla ya kesi yao kuisha.
 
Biblia nimeona pahala inalaanisha kula mali ya yatima na wajane.
COVID-19 wanakula vya yatima na wajane.
Biblia inasema watalipa gharama hiyo[laana]itawaandama wao mpaka kizazi cha nne.
 
Tatizo ni masharti ya kamati ya bunge ya fedha, wenye pesa wanataka zisimamiwe na upinzani binginevyo wanasitisha kutoa! Hapo sasa hakubali mtu, liwalo na liwe.
 
Back
Top Bottom