Mahakama kutoa uamuzi wa Kesi ya Halima Mdee na wenzake Desemba 14

Mahakama kutoa uamuzi wa Kesi ya Halima Mdee na wenzake Desemba 14

Wakati baadhi ya Walalamikaji hao wameanza kuvaa sare za ccm , huku wengine wakihutubia kwenye Majukwaa ya CCM, imetangazwa kwamba hukumu ya kesi yao dhidi ya Chadema itatolewa Desemba 14 2023.

Ikumbukwe kwamba Halima Mdee na wenzake , akiwemo Dada yangu Sophia Mwakagenda walifungua kesi kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema.

===============

Hatma ya Mdee na wenzake 18 kujulikana Desemba 14, 2023

Desemba 14, 2023 saa nane na nusu mchana Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imepanga kutoa hukumu ya kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Halima Mdee na wenzake 19 ambao walifutwa uanachama katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Uamuzi huo umetolewa Oktoba 24, 2023 na Jaji Cyprian Mkeha wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kupangiwa hukumu.

Wakili wa upande wa wajibu maombi, Wakili Deogratias Mahinyira kwa niaba ya wenzake amesema Hukumu ya kesi hiyo imepangwa kutolewa ikiwa ni baada ya pande zote kukamilisha mawasilisho kama ilivyoelekezwa na Mahakama.

"Shauri leo lilikuwa linakuja kwa ajili maelekezo ya Mahakama (necessary orders), kwa sababu tarehe ya mwisho Mahakama ilikuwa imeeleza baada ya shauri kusikilizwa kwamba leo tuje Mahakama ijiridhishe kama pande zote zimeweza kufanya mawasilisho yake ya mwisho ili Mahakama iweze kupanga tarehe ya uamuzi," amesema Wakili Deogratias Mahinyira.

Halima Mdee ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na wenzake 18 walifungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama, kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama (Judicial Review).

Kesi hiyo ilifunguliwa ikiwa ni muda mfupi baada ya Baraza Kuu la Chadema kuunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho wa kuwafukuza uanachama.

Ikumbukwe Juni 2022 Mahakama Kuu Dar es Salaam ilitupilia mbali maombi ya Halima Mdee na wenzake kutokana na kuwepo kwa kasoro kuhusu jina la mjibu maombi wa kwanza, lakini walifungua shauri ambalo linatarajiwa kutolewa hukumu.

Itakumbukwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson alisema hawezi kutangaza kuwa nafasi za Wabunge hao wa Viti Maalum zipo wazi kabla ya taratibu za Kimahakama kukamilika.
Mkuu, hope utatujuza kama ulivyofanya wakati ule wa kesi ya akina Mbowe. Nimekaa mkao wa kusoma utakachotuhabarisha.
 
Mwanachama kama halima mdee yule ni likely atakuwa product ya ccm na aweza akatafutiwa jimbo kama gwajima hatampisha kawe. Kuna kuna bulaya na matiko zile nazo ni asset za ccm typically hazitakaa bure bila kufanya kazi ya za siasa. Wakikosa ubunge watalambishwa hata ukuu wa watalambishwa
It makes sense.
 
Tatizo ni masharti ya kamati ya bunge ya fedha, wenye pesa wanataka zisimamiwe na upinzani binginevyo wanasitisha kutoa! Hapo sasa hakubali mtu, liwalo na liwe.
Hao wenye fedha nao hovyo tu ina maana huu usanii wa serikali hawajaugundua?
 
Hao wenye fedha nao hovyo tu ina maana huu usanii wa serikali hawajaugundua?
Wazungu huwa hawapendi kuingilia upuuzi wetu, tuliwaona wao wabaya tukapewa uhuru sasa unatutokea puani, nchi nyingi za kiafrika ni migogoro kuliko ile ya kudai uhuru, mauaji kila siku.
 
Back
Top Bottom