Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa yatupilia mbali mapingamizi 2 kesi ndogo ya Mbowe na Wenzake. Jaji Siyani ajitoa kuendelea na kesi

Leo nimekupa Like yangu, Mama aache kubambakia watu kesi. Huku mtaani mama anafanya vizuri sana ni vyema akaachana na hii kesi ya mbowe itamuondolea yale mazuri yote ambayo ameanza kuyafanya ndani ya miezi 7 ya uongozi wake.
 
Ile rushwa ya kupewa ujaji kiongozi haikuwa bure.

Kama hakutakuwa na jitihada nyingine, nje ya kutegemea mahakama ambayo haina uhuru, tutarajie mambo ya ajabu, yasiyotegemewa.
Hizo jitihada nyingine Ni zipi ndg, Kama katiba mpya ndiyo hyo inakula msoto gerezani , na jaji kiongozi + Hangaya ndiyo wanaikanyaga!!
 
Nadhani kama ipo fursa ya kukata rufaa katika kesi hii ndogo ndani ya kesi kubwa Mawakili wa utetezi ni bora wafanye haraka.

Jaji Kiongozi katika shauri hili alionyesha utulivu wa hali ya juu kiasi kuwaaminisha wale wote waliokuwa wakifuatilia shauri hili kwamba angetenda haki na haki ikaonekana.

Rais kwa kutumia mamlaka yake ajamteua katika nafasi ya Jaji Kiongozi.Hata namna alivyotoa hitimisho lake unaona wazi kaamua kuwafurahisha waliompatia nafasi hiyo.

Kupitia kesi hii unaona kabisa umuhimu wa katiba mpya.
 
Siamini Kama kweli Mbowe alikula njama ovu, Ila kwa trend ninayoiona, hapa anafungwa mchana kweupe.

Huenda wale waliokimbi nchi wamemponza.
 
Mengi ya gizani hatuyajuia, mambo ya kimafia hayafanyika mwangani mchana hapana hufanyika gizani.....Mawakili tujikite zaidi kwenye kesi yenyewe kupangua kila kinachokuja... Haki haishindwi...itaonekana tu nani mwenye haki nani hana haki....

Ila kama wote wamehusika kwenye michezo michafu gizani basi hapo ujue atakayeshinda ni aliyesukuma kete vizuri...
 
Shukrani ya kuteuliwa kuwa jaji kiongozi ni lazima Mbowe afungwe 😞
Mashauri yote mawili kayatupa kizembe kwa hoja ambazo ata yeye mwenyewe zinaonyesha upendeleo, yani hoja zote zilikuwa zinabana upande wa utetezi alafu mwisho anakuja anasema mimi naona ... Alafu eti court n mhimili unaojitegemea!!!
 
hiyo umesema wewe, kuna jembe linakuja lililompindua dikteta magufuli, ambalo kwa huyu mama yenu aliyepo sasa, kwake ni sawa na kunywa maji ya kunywa. Naye ni mwamba aliyeshindikana, TUNDU ANTIPHAS LISSU. Mwamba wa upinzani Africa.
😲😲🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Huyu Lissu huyu rafiki wa huyu bwana aitwaye David Mc Allister ?!!
 
Naona kila mmoja sasa anaanza kulalamika kuhusu Jaji hii ndio Tanzania yetu
 
naskia harufu ya shombo shombo hivi.....
 
jaji: Kama Shauri likienda mfululizo ingechukua Miezi kama Minne

jaji: Hivyo kwa Majukumu niliyonayo nimeona nijitoe aje Jaji mwingine haraka iwezekanavyo.
 
UPDATE: MWENYEKITI WA CHADEMA NA WENZAKE WAMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 PAMOJA NA FAINI YA MILIONI 460
 
Mahakama haitishiwi na midemuko ya JF.

Sabaya alipohukumiwa hamukusema majaji wa kuteuliwa leo kulikoni.

Jaji hakikisha unatenda haki bila kuangalia sura Wala umaarufu wa mtu,wala kuaangalia wale vibaraka waliomtuma kila siku wako mahakamani kuhakikisha hawataji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…