nyboma
JF-Expert Member
- Aug 29, 2021
- 2,308
- 7,366
Leo nimekupa Like yangu, Mama aache kubambakia watu kesi. Huku mtaani mama anafanya vizuri sana ni vyema akaachana na hii kesi ya mbowe itamuondolea yale mazuri yote ambayo ameanza kuyafanya ndani ya miezi 7 ya uongozi wake.Hili likesi na makesi yote yaliyoanzishwa awamu ya 5 kwa nia ovu yafutwe, Hangaya na vyombo vyake vya usalama wanashindwa kuona hili? Asubiri hawa akina Mwamba kama watafanya makosa (Ya ukweli) kwenye awamu yake ndipo "arare nao mbere", makesi mengi ya awamu ya 5 yana ukakasi sana. Mfano mmoja tu, Bwana Mrosso asingekuwa na mil 90 ya kumpa Sabaya leo hii angekuwa ndani kwa kesi ya kubambikiwa ya uhujumu uchumi na utakatishaji!! DPP na watu wako futeni hii kesi......