Erythrocyte wewe jamaa unaipenda chadema kuliko ht uhai wako aisee dahMwakilishi wa Bavicha tayari ameketi akiwa na fulana yake nzuri yenye kuchagiza Katiba mpya
View attachment 1980561
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Erythrocyte wewe jamaa unaipenda chadema kuliko ht uhai wako aisee dahMwakilishi wa Bavicha tayari ameketi akiwa na fulana yake nzuri yenye kuchagiza Katiba mpya
View attachment 1980561
Hilo halitawezekana na utakuwa mfungwa wewe in shaa Allah. AmenMbowe anasubiriwa ale mvua 30 damu ya Chacha wangwe inamlilia
Kwani kumuua jambazi muuwaji ni kosa?Sheria inasema Kila mmoja ni mlinzi wa mwenzako na Kila raia ahakikishe anajilinda dhidi ya wahalifu. Mbowe alikuwa anatishiwa kuuwa na Sabaya na ushahidi upo alipovamiwa hotelini kwake. Makosa anayotuhumiwa nayo Mbowe ni makosa ya kubumba yaani yametengenezwa na Sabaya pamoja na wahuni wachache ili kumharibia. Lakini wakasahau kuwa kosa moja kwao limemuongezea umaarufu Mbowe na kuwaanika utupu watesi wake.
Mkuu ungetuwekea na mistari ya ngapiMuovu ataaibika na kupotea mbele za Mungu na wanadamu, ila mwenye haki atachomoza kama nuru ing'aayo sana huku akilakiwa kwa mioyo yenye furaha
Atanyongwa Sabaya maana kama kufungwa ashafungwa tayariSubiri anyongwe
[emoji38][emoji38][emoji38] Nimejikuta nacheka chini kwa chini , taratibu mkuu tuko MahakamaniErythrocyte wewe jamaa unaipenda chadema kuliko ht uhai wako aisee dah
NafuatiliaMahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, leo Jumatano Oktoba 20, 2021 inatarajiwa kutoa uamuzi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.
Uamuzi huo ambao utatolewa na Jaji Mustapha Siyani (Jaji Kiongozi kwa sasa) unaweza kuwa picha ya mwelekeo wa kesi nyingine ndogo ndani ya hiyo kesi.
Kesi hiyo ndogo inahusiana na uhalali wa maelezo ya mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Adamu Hassan Kasekwa, ambayo mawakili wa utetezi waliyapinga yasipokewe kama kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.
Upande wa utetezi uliyapinga ukidai kuwa yametolewa nje ya muda wa kisheria na kwamba mshtakiwa huyo hakuyatoa kwa ridhaa yake bali kabla na wakati wa kuchukuliwa maelezo hayo alitishiwa na kuteswa.
Ikiwa mahakama itakubaliana na hoja za upande wa mashtaka, basi itayapokea maelezo hayo na kuwa kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.
Kupokewa kwa maelezo kutamaanisha kwamba mshtakiwa huyo amekiri makosa na hivyo mahakama itaweza kuyatumia maelezo yake hayo kumtia hatiani na kwa kuzingatia ushahidi mwingine wa upande wa mashtaka.
Lakini kama mahakama itakubaliana na hoja zote za utetezi au mojawapo kati ya hizo mbili, kuwa maelezo yalichukuliwa nje ya muda au kwamba mshtakiwa aliteswa kabla na wakati wa kutoa maelezo, basi itayatupilia mbali maelezo hayo.
=========
UPDATES;
=========
Tayari baadhi ya wanachama na viongozi mbalimbali wa Chadema pamoja na Wawakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa wamewasili .
View attachment 1980538
Ukumbi wa mahamama umejaa wengine wamekaa kusubiri hatma ya uamuzi mdogo wa kesi ya msingi namba 16/2021.
View attachment 1980530
Wananchi wakiwaombea watuhumiwa akiwepo Freeman Mbowe walipowalisi katika viunga vya mahakama asubuhi hii.
View attachment 1980534
Mawakili wa pande zote mbili wameshaingia mahakamanu na kukaa kwenye sehemu zao.
View attachment 1980537
Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani na Mwakilishi wa Ubalozi wa Sweden wakiwa katika ukumbi wa mahakama kusubiri uamuzi wa kesi ndogo ya kesi ya msingi namba 16/2021 inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu.
Muda huu washitakiwa wameingia katika ukumbi wa mahakama tayari kusikiliza uamuzi wa mahakama katika shauri dogo la kesi ya msingi namba 16/2021.
Jaji anaingia
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 inatajwa
Robert Kidando anawatambulisha mawakili upande wa serikali.
1. Robert Kidando
2. Nassoro Katuga
3. Ignas Mwanuka
4. Esther Martin
5. Tulumanywa Majigo
Peter Kibatala anawatambulisha pia wenzie
Gaston Garubindi
Seleman Matauka
Idd Msawanga
Michael Mwangasa
Dickson Matata
Maria Mushi
Evaresta Kisanga
Allex Massaba
Jonathan Mndeme
Fredrick Kiwhero
John Malya
Jaji: Wakili wa Serikali
Robert Kidando: Shauri limekuja kwa ajili ya uamuzi tupo tayari Mheshimiwa jaji.
Jaji: Utetezi
Peter Kibatala: tupo tayari Mheshimiwa Jaji Kiongozi.
Kimya kidogo
Bado Kimya kidogo
Jaji anachana Bahasha
Jaji: Sasa nitajaribu kusoma kadri nitakavyoweza ufupisho wa yale yaliyosemwa hapa Mahakamani kwa upande wangu ambayo ni umuhimu kama ufupisho. Na utakuwa ndiyo uamuzi wangu.
Jaji: Wakati anatoa Ushahidi Upande wa Simu Shahidi Kingai, alitoa Ushahidi kuwa Adam Kasekwa alikamatwa tarehe 05 Mwezi wa 08 Mwaka 2020.
Jaji: Kwa mujibu wa Ushahidi wake baada ya kuwakamata aliwachukua kwenda kuwasaidia kumtafuta Moses Lijenje.
Jaji: Na baada ya hapo all msafisha Kuja Central Dar es Salaam
jaji: Kwa maelezo hayo ACP kingai aliomba Maelezo ya onyo yapokelewe kama Sehemu ya Ushahidi.
Jji: Ombi lake lilipingwa na Upande wa Utetezi.
Jaji: Sababu ya Pingamizi
Jjai: Maelezo hayo yamechukukiwa kinyume na Muda wa Sheria know nyume na Sheria inayoongoza Mwenendo wa a Makosa ya Jinai kifungu namba 5 na 52.
Jaji: Na Sababu ya pili kwamba Adam aliteswa wakati anatoa Maelezo hayo.
Jaji: Mawakili wa pande zote mbili waliona kuna umuhimu wa Kisheria fanya shauri dogo
Jaji: Mawakili wa pande zote mbili waliona kuna umuhimu wa Kisheria fanya shauri dogo
Jjai: Kusikiliza shauri hili dogo
jaji: Mimi nakubaliana nao
jaji: Know kila Upande ulikuwa na Mashahidi Watatu
Jaji: Sikusudii Kurudia Kusema kila kitu ambacho Mashahidi walisema.
jaji: Isipokuwa nitapitia yale ambayo nitarejea wakati wa uamuzi.
jaji: Upande wa Jamhuri kwamba Adam Kasekwa ni kweli hakuweza kuhojiwa ndani ya masaa Manne kwa sababu Upelelezi wao ulikuwa haujakamilika.
jaji: ACP kingai na Mahita wakati wamepewa taarifa mpango wao ulikuwa kuwa ni kuwakamata watu watatu.
jaji: Licha ya hivyo hawakumkamata Moses Lijenje
Jaji: Kwa Mujibu wa Kingai ni kwamba Adam akijitolea kwenda kumtafuta Moses Lijenje sehemu mbalimbali kama Majengo, Boma Ng'ombe na Sehemu zingine bila Mafanikio. Wakarudi Central Moshi.
jaji: Kwa Mujibu huo Siku ya tarehe 06 pia Juhudi za kumtafuta Moses Lijenje zilindeleaa. Wakaenda Mpaka Arusha Maeneo ya Sakina kwa Dada yake Moses Lijenje.
jaji: Ambao tarehe 06 amri ikatolewa kuwasafirisha kwenda Dar es Salaam.
Jaji: KINGAI NA MAHITA wote wanakubali kuwa walisafiri kuja Dar es Salaam Na wakakabidhiwa kwa Msemwa.
jaji: Kingai anasema baada ya kufahamishwa haki zake Kisheria aliojiwa Siku hiyo hiyo.
jaji: Adam Kasekwa alikamatwa na kukanusha kuwaongoza Polisi wale waliomkamata kwenda maeneo kadhaa Mji wa Moshi na Arusha.
jaji: Alikanusha pia hakupelekwa Central Dar es Salaam Bali Kituo cha polisi Tazara.
jaji: Ushahidi wa Adam Kasekwa unaonyesha alipofika Dar es Salaam Siku ya Tarehe 07 Mwezi wa O8 alipelekwa Tazara na Mbweni na Siku ya tarehe 09 alitishwa ili kuweka sahihi.
jaji: Ilishabihishwa pia kupitia Shahidi wa Pili Mohamed Ling'wenya.
jaji: Kwa Mujibu wa Moses Ling'wenya alisikia walipokuwa Moshi akilia kwa Sauti ya zege.
jaji: Lilian pia kama Shahidi wa tatu ambaye ni Mke wa Adam Kasekwa alithibitisha kuwa alimuona Adam Kasekwa kuwa kateswa na kwa kuthibisha kwa makovu. ...Na alivyokuwa anatembea
jaji: Hivyo baada ya kupitia pia mawasilisho yao ya pande zote, nawashukuru sana.
jaji: Kwa Upande wa Jamhuri wao walisisitiza kuwa Maelezo yalichukuliwa kwa Mujibu wa sheria kwamba Kifungu cha 50(2) unaondoa Muda huo katika Hesabu za Masaa Manne toka awekwe Chini ya Ulinzi
jaji: Hivyo kwa Mujibu Wa Robert Kidando Muda uliotumika KusafiriSha watuhumiwa haupaswi kuwa sehemu ya Masaa Manne.
jaji: Kuhusiana na Shauri hili sasa Upande wa Jamhuri wanakiri kuwa walikuwa na Adam kasekwa.
jaji: Upande wa Jamhuri sasa wameniletea Kesi Mbalimbali kwa ajili kufanya Rejea
jaji: Kuhusiana na Uamuzi sasa kwanini Adam Kasekwa amekamatiwa Moshi na Kuja kuhojiwa Dar es Salaam.
jaji: Kwa Mujibu wa Robert Kidando sasa anasema ni sababu ya Uzito wa tuhuma, kuzingatia pia Makosa yalitakiwa kufanyika sehemu mbali mbali
jaji: Kuhusu Pingamizi la pili kuhusiana Adamoo kulalamika kwamba Ameteswa
jaji: Wakili wa Serikali amesema Maelezo hayo yaliandikwa Siku ya tarehe 07 Mwezi wa 08? Na Kwamba Upande wa Utetezi wameshindwa Kuibua shaka.
jaji: Upande wa Utetezi umeshindwa Kuwahoji Mashahidi wa Jamhuri
jaji: Maelezo ya Adam Kasekwa ni kwamba Japo alitoa Maelezo lakini hakutoa kwa ridhaa yake.
jaji: Kuhusiana na Ushahidi wake hauonyeshi kuwa alitoa Maelezo au Kuteswa akiwa Central Police Dar es Salaam.
jaji: Kwa hiyo kwa Upande wa Serikali ni kwamba Ushahidi uliachana na Pingamizi
Badala yake ukawa ni wakufikirika
jaji: wakanirejesha kwenye kesi ya Rugemalila VS Jamuhuri
jaji: Kwamba Kingai hakuhojiwa kwa Mateso aliyopewa Adamu Kasekwa akiwa Moshi.
jaji: hakuhojiwa pia kuhusiana na Maelezo aliyoyachukua Dar es Salaam
jaji: Kwa Mujibu wa Robert Kidando akaeleza athari za kutokuhoji Mambo ya msingi.
jaji: Pia amezungumzia kukinzana kwa Maelezo ya Ushahidi kati ya Adam Kasekwa na Mohammed Ling'wenya
Kuhusiana na Upande wa Utetezi Mawasilisho yaliandikwa na John Malya
jaji: Kwamba Maelezo yalichukuliwa Siku ya tarehe 07 ambapo Masaa Manne yalikuwa yameshapita
Kuhusiana na Mazingira yaliyowekwa na Sheria kifungu cha 50 kwamba Mahakama inapaswa kingatia Masaa Manne na kuyaondoa yale ya kusafirisha Watuhumiwa
jaji: Moshi palikuwa na Nyenzo zote ambazo zingeweza kuwezeha Maelezo kuchukuliwa
Kuhusiana na Mateso, Wakili Malya anasema Mateso siyo lazima yawe ya kimwili, Bali Fikra na utu.
Au Mateso yanayotweza Utu wa Mtu
jaji: wakili mallya akaturejesha Kwenye katiba pia
Na Pia akaturejesha Kwenye Tamko la Umoja wa Mataifa linalozingatia Mateso na Utu wa Mwanadamu.
Wakili Malya ametutaka Mahakama tuzingatie Nyaraka hizo.
jaji: wakili mallya ametupa kesi za Marejesho
jaji: Kutokana Nyaraka hizo alizowasilisha Wakili Malya, Amesema ingawa hapakuwa na Ushahidi wa kitabibu Lakini ametutaka tuzingatie Ushahidi wa kimazingira.
Wawekee link ya martin masese jamaa anaflow direct huko tweeter[emoji38][emoji38][emoji38] Nimejikuta nacheka chini kwa chini , taratibu mkuu tuko Mahakamani
Kishaingia Roving Journalist , ngoja tumuombe afanye hivyoWawekee link ya martin masese jamaa anaflow direct huko tweeter
Yes ni Jaji Kiongozi lazima apewe heshima yake!! heshima haiombwi bali ni wajibu, asante Wakili msomi Kibatala kutukumbusha hilo.Peter Kibatala: tupo tayari Mheshimiwa Jaji Kiongozi
Poa jamaa yupo on time sana maseseKishaingia Roving Journalist , ngoja tumuombe afanye hivyo
Kwahiyo Juma huwa anateleza mata tatu zote kwa nyakati tofauti na matukio tofauti?Hukumu ni hukumu
Sio story useme mtu anaweza teleza ulimi
Hii comment vipi?Erythrocyte wewe jamaa unaipenda chadema kuliko ht uhai wako aisee dah