Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa yatupilia mbali mapingamizi 2 kesi ndogo ya Mbowe na Wenzake. Jaji Siyani ajitoa kuendelea na kesi

Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa yatupilia mbali mapingamizi 2 kesi ndogo ya Mbowe na Wenzake. Jaji Siyani ajitoa kuendelea na kesi

Hili likesi na makesi yote yaliyoanzishwa awamu ya 5 kwa nia ovu yafutwe, Hangaya na vyombo vyake vya usalama wanashindwa kuona hili? Asubiri hawa akina Mwamba kama watafanya makosa (Ya ukweli) kwenye awamu yake ndipo "arare nao mbere", makesi mengi ya awamu ya 5 yana ukakasi sana. Mfano mmoja tu, Bwana Mrosso asingekuwa na mil 90 ya kumpa Sabaya leo hii angekuwa ndani kwa kesi ya kubambikiwa ya uhujumu uchumi na utakatishaji!! DPP na watu wako futeni hii kesi......

Hakuna rais mwenye uwezo wa kuingilia mahakama. mama mwenyewe ni mtu wa kufuata katiba na utawala wa sheria na kuzingatia uhuru wa mahakama. Ushauri wako feki haujafatwa, haufatwi, na hautafatwa
 
Naona kila mmoja sasa anaanza kulalamika kuhusu Jaji hii ndio Tanzania yetu
cheo kinapandaje katikati ya shauri, hii si ni rushwa kama zilivyo rushwa zingine.

Hata ningekuwa mimi ni jaji, siwezi kumwangusha anayenipa ugali wa watoto wangu, pambaneni mbadilishe katiba msinilaumu mie - mie ni mtumishi tu wa bwana wangu.
 
Ile rushwa ya kupewa ujaji kiongozi haikuwa bure.

Kama hakutakuwa na jitihada nyingine, nje ya kutegemea mahakama ambayo haina uhuru, tutarajie mambo ya ajabu, yasiyotegemewa.
Siyani Jk
Amesema Kwenye Ruling yake Kwamba zile confession statement zilipatikana Kwa usahihi, Hakukuwa na mateso na wala hazikupatikana nje ya muda wa kisheria.

Kwa hiyo zimepokelewa na kesi kubwa itaendelea Kusikilizwa

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Kwa Sabaya Judiciary Itakuwa Huru Ila Mjuba akili Vyuma Judiciary Itakuwa Sio Huru. Tungoje Wakuu [emoji120][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwani haiwezekani Mbowe akakiri makosa ili kupunguza usumbufu?
 
Jaji Kiongozi: ni sawa tunapaswa Kunaendele na Shahidi Lakini nikaomba nishauriane na Mawakili. Sasa Nimeona kwamba Shauri hili ni Moja ya Shauri linalopaswa kuisha kwa haraka.

Jaji: Kama Shauri likienda mfululizo ingechukua Miezi kama Minne

Jaji: Hivyo kwa Majukumu niliyonayo nimeona nijitoe aje Jaji mwingine haraka iwezekanavyo zekanavyo

Jaji ananyanyuka anaondoka Zake.
 
Leo nimekupa Like yangu, Mama aache kubambakia watu kesi. Huku mtaani mama anafanya vizuri sana ni vyema akaachana na hii kesi ya mbowe itamuondolea yale mazuri yote ambayo ameanza kuyafanya ndani ya miezi 7 ya uongozi wake.
Tatizo la Mbowe anataka kuleta league.

Lazima anyoooshwe. Yeye ni nani kwani ??

Kwani kuna makundi mangapi ya kijamii nchi hii.

Kwanini genge la wanasiasa lenyewe lijione ni special sana kwamba kila wanachotaka ni lazima wasikilizwe.
 
Hili nililitarajia!!
Na ndio mpango mkakati ulivyokuwa!
 
Sijui kwa nini mheshimiwa Mbowe aliamua kurudi bongo asee..yani hata jiwe hakuwahi kumtesa kiasi hiki kwa kumpa kesi ngumu namna hii..
 
Wote wenye roho za kishetani mtashindwa, maana giza halijawahi kushinda mwanga! Mola wetu ni mwema na atatenda, Mbowe atatoka!
 
Alipewa rushwa ya cheo. Ametimiza matakwa ya mteule wake. Sasa atapewa jaji mwingine atakayepangwa na yule jaji miongoni mwa wasiojulikana, jaji simba.

Marehemu kwa kuwapachika wasiojulikana kuwa majaji, aliua kabisa mfumo wa mahaka huru.

Uharibifu wa marehemu kwenye maeneo mbalimbali ya taasisi za utawala na serikali, itachukua miaka mingi kuurekebisha. Na bahati mbaya Hangaya naye, anaenda kiunafiki kuihadaa jamii ya kimataifa huku moyoni akiwa hana dhamira ya dhati ya kuondoa uchafu walioutengeneza wakati wa awamu ua 5.
 
Vipi jaji anaendelea au kaona heri kusepa?
Mbowe na Genge lake la kihalifu hawapo juu ya Sheria.
Kama ikithibitika kuwa alikuwa anachezea amani ya nchi yetu basi sheria ifanye kazi yake ili iwe fundisho kwa wengine ambao wanadhani amani yetu ni jambo la kuchezea.
 
Back
Top Bottom