Mahakama kuu imesema msanii Elizabeth Michael (Lulu) ana kesi ya kujibu

Mpo wawili tu chumbani.mmoja akafa.Unategemea nani kamuua mwenzake??
Jihu simple ni wewe uliyekuwa naye.
Ataachiwa kama alikuwa chizi
Alikuwa under 18
Ama alikuwa anajihami.Let say angekuwa kavamiwa Na Jambazi Sasa kule ile kujidefend
Kuhusu kuwa under 18,Kuna ushahidi wa video yake mwenyewe akisema yeye ni.mkubwa Sasa ndo Mana amepeqa driving license. kwenye Birt part yake.
Hapo tuombe Muujiza tu.
 
Kanumba alikuwa msukuma....Makonda Msukuma...Magufuli Msukuma.

Nakwambia hii Lulu atoki.
Si kweli. Kijana alikuwa ujanani anabembeleza utamu. Alikufa for the sake of utamu. Let it remain that way. The girl is strong and should be free.Spread some love!
 
Kwahiyo aliamua kufa tu?!
Watu wana uelewa mdogo sana.
Huenda kweli hawezi kumuua ila inawezekana katika kujilinfa akampiga Na.kitu kizito kwa nia ya kujiokoa.But unfortunately ukatokea kifo
But kesi IPO.Na kesi aina hii.ni kifungo cha maisha.
Ila angeua kwa makusudi ndo kesi yake ni kunyongwa.
 
LULU AKIJITETEA MAHAKAMANI

"Nilipofika kwa marehemu 'Kanumba' nilimkuta yupo kwenye dressing table,nilikaa kitandani kwa kuwa hapa kuwa na sehemu ya kukaa...Nilikuwa nataka kutoka ila marehemu 'Kanumba' alinikataza,alikuwa hataki nitoke na marafiki zangu,Marehemu nilipomwambia natoka na marafiki zangu alinikimbiza na taulo na mimi nilikuwa naogopa kupigwa.

Mara nyingi marehemu alikuwa ananipiga kila akilewa na sio kwa akili zake.

Alipoona simu yangu inaita akahisi ni simu ya mwanaume akasema kwanini naongea na simu ya mwanaume mbele yake,Marehemu akaingia uvunguni akatoa panga akasema leo nakuua huku akinipiga na panga kwenye mapaja.

Marehemu alianguka mwenyewe na kujigonga kwa nguvu na kuinuka sehemu nyingine alikuwa kama anatapatapa.

Nilipoona hivyo nilitoka nikakimbilia chooni na kupiga kelele, Nilipotoka chooni Nilimkuta amelala,nilihisi amejifanyisha nikaanza kumwambia kuwa wakija watu nitawambia kila kitu ulivyonipiga na panga.

Baada ya muda mchache nilisikia kishindo kama mtu anafungua mlango,Nilimwambia Seth kuwa Kanumba amedondoka na akajaribu kumuamsha hakuamka akasema anaenda kumuita daktari

Alivyosema anaenda kumuita daktari nikasema na mimi naondoka nikiogopa anaweza akaamka akaanza kunipiga tena,Niliondoka nikawasha gari kuelekea Coco Beach, Huko Coco Beach hakukuwa na kitu nilienda tu kutuliza akili.

Nilivyofika Coco Beach SMS zilianza kusambaa kuniuliza kuwa nasikia Kanumba amefariki,Nikachukua simu nikampigia kidume 'rafiki yake Kanumba' kumuuliza Kanumba yupo hospitali gani? nije kumuona

Akaniambia wewe usije hospitali,niambie uko wapi tuonane Bamaga? "

Tulivyokutana Bamaga alikuwa kama anataka kuongea na mimi ghafla wakaja askari kunikamata Na kunipeleka Oysterbay polisi,Nilipofika Oysterbay nilikuta watu wengi sana niliyemtambua ni Ray

Nilijua Kanumba amefariki nikiwa polisi,Nilipomkuta Ray Oysterbay polisi nikajua Kanumba amekamatwa kwasababu ya makelele niliyokuwa nayapiga kule nikajua watu walisikia.

Kwa namna yoyote ile mimi sijasababisha kifo cha Kanumba,na mimi ndiye nilieshambuliwa na marehemu kutokana na umbile langu nilikuwa mdogo na alikuwa na uwezo wa kufanya chochote kwenye mwili wangu kwa sababu yeye ndo alikuwa na silaha.

Huu ndio utetezi wa Lulu tusubirie Maswali ya kutoka kwa mawakili wa upande wa serikali na wale wa upande wa mtetezi
 
Masikini Lulu. Wamsamehe tu.
Ningekuwa mimi ndo mama kanumba ningesamehe tu kwani hata akifungwa mwanae hawezi kurudi
huyu ameshtakiwa na jamhuri na sio mama kanumba!! kama ana hatia au hana itaamua mahakama!!
 
hapana hakuwa naye mpaka anakata roho acha uongo
 
anaweza kuachiwa kwa hili.

aliwasha gari akaondoka.
mbona kuna maelezo kipindi cha nyuma wakati upelelezi unaendelea alikua
-hana gari...alitumoa gari la nani?
-alikuwa akivunja sheria za nchi kwa kuendesha gari akiwa hajafikisha miaka 18 si ndio?alidanganya
-inasemekana wakati wa kuja kwa kanumba alikuja kwa taxi na kuna taxi driver msiri wa kanumba ndo alikua anamleta hapo .so ikawa siri yao walimwengu hatukujua kama wanadate
-inasemelana wakati wa kutoka alimpigia ali kiba aje ampitie....na ali kiba kipindi kile alikiri ni kweli alimpa lifti usiku ule....ila hakujua kinachoendelea.
 
Huu ni utetezi wa lulu wa leo mkuu!
 
To cut the story short
ushahidi uliopo ni wa kimazingira,hakuna mtu aliyemuona lulu akimpiga ama akimsukuma Kanumba.Jamuhuri hawana ushahidi huo, pili hilo panga lililokutwa huko chumbani hakuna ushahidi walau wa finger prints unaoonyesha lulu alishika hilo panga version ama story iliyobaki ni ya lulu pekee maana ndie shahidi pekee aliyekuwepo kwenye eneo la tukio. Mahakama itaangalia factor nyingi the fact kwamba kalikuwa kasichana, umri wake uwezo wa kujitetea kama kweli alikuwa akilazimishwa kwa kifupi namuona lulu AKIACHIWA HURU .....hakuna mahakama itakayoweza kumtia hatiani huyo binti kwa kwa ushahidi dhaifu dhidi yake
 
Aendelee kunyoosha maelezo yake bila kujichanga changanya.Sijajua anatetewa na wakili gani.Ila kama alimuua basi hawezi pona.

Halafu akishinda hii kesi watasherehekea ushindi huo pamoja na wakili wake
 
haki na wajibu uchukue nafasi yake hapa,elewa ni watu wawili tu waliokuwemo kwenye kile chumba wakati haya yanatokea na bahati mbaya mmoja wao alipoteza maisha,ushahidi muhimu hapa wa polisi ni foresinc report itakayokuja na majibu ya maswali mengi,ninasubiria kwa hamu ushahidi huu wa kitaalamu,sio ule ushahidi wa watu ambao hawakushuhudia nini kilitokea usiku ule.
 
NAKAONEA HURMA NA NAUMIA SANA!
ILA HII KESI INA GAPS NYING SANA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…