Mahakama Kuu: Kutangaza Washindi wa Uchaguzi waliopita bila kupingwa ni Kinyume cha Katiba

This is huge for Tanzanians
Hakika huu ni ushindi mkubwa sana kwa wapenda demokrasia

DED waliipindua kabisa katiba ya Jamhuri inayo sema mtu ata zuiwa kugombea nafasi ya kuchaguliwa kama:

1-Atatumikia kifungo zaidi ya miezi 6 jela
2-Atahukumiwa kifungo chochote kwa kosa la kukwepa kulipa kodi(hata ukifungwa kifungo cha nje au siku moja kwa kosa la kukwepa kulipa kodi huwezi gombea)
3-Mahakama imethibitisha sio raia wa TZ

Magu yy alikua anamuambia tu DED kata wote
 
Kwanza Mimi niwape pongezi sana watu waliohusika na mchakato wa kuamua kufungua kesi ya kupinga utaratibu wa wagombea kupita bila kupingwa hali hiyo iliwalazimisha watendaji wa tume hasa wakurugenzi wa halmashauri pamoja maveo na maweo kufanya kila namna kuhakikisha wagombea wa upinzani wanahujumiwa ili wagombea wa CCM wapite bila kupingwa.Rais wa sasa ni muungwana wapenda demokrasia hatutegemei serikali yake kwamba itaanza michakato ya kuikatia rufaa hiyo hukumu kama walivyofanya watangulizi wake huko nyuma ilipotolewa hukumu ya maded wasimamie uchaguzi.Hongereni majaji wetu kwa your rulling
 
Nendeni mkasome shule muache ulalamishi. Kama hukuelewa katafute mtu akutafsirie
Nani amelalamika? nani amekwambia kua haelewi?

Au na wewe mradi tu u comment ili usisahauliwe kua upo humu JF?
Jaribu kua na akili ya uelewa,kama huelewi swali basi piga kimya kuliko kupayuka hovyo.
 
Nani amelalamika? nani amekwambia kua haelewi?

Au na wewe mradi tu u comment ili usisahauliwe kua upo humu JF?
Jaribu kua na akili ya uelewa,kama huelewi swali basi piga kimya kuliko kupayuka hovyo.
Duh wewe @icebreaker ni punguani sasa. Kasome mwenyewe ulichoandika kwenye post #2
 
Duh wewe @icebreaker ni punguani sasa. Kasome mwenyewe ulichoandika kwenye post #2
Huna akili wewe,

Nimeuliza kwanini mambo ya sheria huandikwa Kingereza na sio Kiswahili,hiyo haimaanishi kua sijaielewa post au la,nimetaka tu kujua kwanini hua hawaandiki kwa Kiswahili? ila wataalamu wameshanijibu,
 
Kuna wagombea walitekwa, wakapigwa na kutupwa msituni, na wengine wakawekwa lupango Ili kupisha wagombea wanaotakiwa kupita bila kupingwa!!!
Mahakama pia ingetamka jambo juu ya hawa washindi haramu..
 
Kuna wagombea walitekwa, wakapigwa na kutupwa msituni, na wengine wakawekwa lupango Ili kupisha wagombea wanaotakiwa kupita bila kupingwa!!!
Mahakama pia ingetamka jambo juu ya hawa washindi haramu..
Kumbuka Waziri mkuu naye alipita bila kupingwa Ruangwa.
 
Jamhuri hawachelewi kukata rufaa na kushinda! Kama wachawi vile. Maana hata kwenye hukumu ya kuruhusu Mgombea binafsi, walifanya hivi hivi.
Kwenye mgombea binafsi sababu walishindwa kwenye mahakama ya Afrika walileta utetezi kwamba swala hilo limepitishwa kwenye mchakato wa katiba, ila kwa sababu tuna majaji njaa wakakubali hoja yao wakati wao walitakiwa kukazia hukumu.
wakija wagombea binafsi tutaondokana na wagombea wazembe na hapo ndipo tutaanza kuonja matunda ya demokrasia.
 
Hivi ni kwanini mambo ya sheria huandikwa kwa lugha ya Kiingereza na sio Kiswahili?
Huwa ni utahira tu,yani jamii yako 99% watu wanazungumza Kiswahili hata hiyo 1% iliyobaki inafahamu kiingereza kwa shida bado unaandjka nyaraka kwa Kiingereza what for?

Kuna baadhi ya vitu Magufuli alikuwa sahihi sana.
 
Ila bado wataweza enda Mtu 1 pekee kugombea ambayo automatically atashinda yeye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…