Pre GE2025 Mahakama Kuu yaagiza dhamana ya Dkt. Slaa ishughulikiwe haraka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
huyu babu atakuja kufia mahabusu yaani umri huo bado unashindana na wenye nguvu ? hayo matesoi anayoyapata anajipunguzia umri wa kuishi bure hela anayo ya kutosha kula vizuri huku akilea wajukuu sasa anachokitafuta sijui ni nini ana laana ya upadre huyu ndiyo maana hata mkewake alikuwa anamduda ma ngumi
Mbona povu linakutoka ovyo?
 
Hiyo yote imepangwa wanapiga danadana. Hata akitoka ameisha kaa jela zaidi ya mwezi, miezi kadhaa ni kama amehukumiwa tayari kifungo cha wiki, mwezi, miezi kadhaa.

Hii ni kama umuweke jela mtu mwenye umri kama wa Wassira, Warioba, Hafidh mume wa Samia kisa hupendi maoni yake. Hawana utu hawa mafisadi.
Maza katili haswa
 
huyu babu atakuja kufia mahabusu yaani umri huo bado unashindana na wenye nguvu ? hayo matesoi anayoyapata anajipunguzia umri wa kuishi bure hela anayo ya kutosha kula vizuri huku akilea wajukuu sasa anachokitafuta sijui ni nini ana laana ya upadre huyu ndiyo maana hata mkewake alikuwa anamduda ma ngumi
Bora afie mahabusu akipigania demokrasia kuliko wewe unafia kuwa chawa wa binadamu wenzio
 
Mahakama Kuu ya Tanzania, masijala kuu jijini Dar Es Salaam imegiza shauri la mwanasiasa Mkongwe Nchini Dkt. Wilbroad Slaa lirejeshwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kushughulikiwa kwa dhamana yake.

Dkt. Slaa na jopo la mawakili wake walifungua shauri la mapitio la kesi yake katika Mahakama Kuu akipinga mwenendo wa Mahakama ya Kisutu kuahirisha usikilizwaji wa suala la dhamana yake kutokana na maombi ya kupinga dhamana yake yaliyotolewa na Jamhuri.

Jaji Arnold Kirekiano leo Januari 30, 2025 amesema kwa kuwa kesi ya msingi iko Mahakama ya Kisutu ambayo ina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwa kuwa hoja ya uhalali wa mashtaka ilishatolewa Kisutu na inasikilizwa na kupangiwa uamuzi amesema si vyema Mahakama Kuu kuingilia kati. Hivyo Jaji Kirekiano ameelekeza Mahakama ya Kisutu itoe uamuzi ambao ilishauandaa.

Dkt. Slaa alikosa dhamana tangu alipopanda kizimbani Januari 10, 2025 kusomewa shitaka linalomkabili la kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa X.
Soma, Pia:
Muda waliotaka akae ndani naona umeisha sasa wanamuachia.... kazi kweli kweli
 
Nafikiri watamtafutia zengwe lingine kuelekea October 2025. Dr Slaa, Lissu, Mpina kwa sasa ni sauti za Watanzania.

Wanapigania maslahi, haki, uhuru, demokrasia ya ukweli kwa Watanzania kwa ujasiri mkubwa. Wanajaribu kuwafunga midomo kwa mbinu zozote zile hata kupitia magereza.
 
Mahakama Kuu ya Tanzania, masijala kuu jijini Dar Es Salaam imegiza shauri la mwanasiasa Mkongwe Nchini Dkt. Wilbroad Slaa lirejeshwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kushughulikiwa kwa dhamana yake.

Dkt. Slaa na jopo la mawakili wake walifungua shauri la mapitio la kesi yake katika Mahakama Kuu akipinga mwenendo wa Mahakama ya Kisutu kuahirisha usikilizwaji wa suala la dhamana yake kutokana na maombi ya kupinga dhamana yake yaliyotolewa na Jamhuri.

Jaji Arnold Kirekiano leo Januari 30, 2025 amesema kwa kuwa kesi ya msingi iko Mahakama ya Kisutu ambayo ina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwa kuwa hoja ya uhalali wa mashtaka ilishatolewa Kisutu na inasikilizwa na kupangiwa uamuzi amesema si vyema Mahakama Kuu kuingilia kati. Hivyo Jaji Kirekiano ameelekeza Mahakama ya Kisutu itoe uamuzi ambao ilishauandaa.

Dkt. Slaa alikosa dhamana tangu alipopanda kizimbani Januari 10, 2025 kusomewa shitaka linalomkabili la kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa X.
Soma, Pia:
CCM wanatumia Mahakama
 
Back
Top Bottom