Mahakama Kuu yaagiza Lissu aletwe Mahakamani Juni 27, 2025 katika kesi ya marejeo aliyoifungua

Mahakama Kuu yaagiza Lissu aletwe Mahakamani Juni 27, 2025 katika kesi ya marejeo aliyoifungua

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Kesi ya Marejeo iliyopo Mahakama Kuu Dar esn Salaam iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri Na. 14496 ya 2025 ambayo ilipangwa kutajwa leo Juni 17, 2025 imeahirishwa hadi Juni 27, 2025.

Shauri hilo lilipangwa kusikilizwa kwa njia ya Mtandao mbele ya Jaji Mkwizu lakini Mahakama imeagiza kuwa itakapotajwa tena Juni 27, Lissu anatakiwa kufikishwa Mahakamani (physically).

Katika shauri hilo Lissu ambaye yupo Gerezani kutokana na kukabiliwa na shtaka la uhaini ambalo halina dhamana anaoimba Mahakama kufanya marejeo ya mwenendo wa Kesi ya tuhuma za 'kutoa taarifa za uongo Mtandaoni' ambayo inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi Muhini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Baadhi ya Mawakili waliofika Mahakamani kumuakilisha Lissu ni Wakili Hekima Mwasipu, Wakili Paul Kisabo na Wakili Jeremiah Mtobesya.

Lissu akifikishwa mahakama ya mkazi Kisutu



 
Kesi ya Marejeo ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri Na. 14496 ya 2025 imeahirishwa leo katika Mahakama Kuu-Dar es Salaam hadi Juni 27 saa tatu asubuhi, ambapo Mahakama imeagiza TunduALissu kuletwa Mahakamani ili kesi isikilizwe 'Physically'

Katika shauri hilo Lissu ambaye yupo Gerezani kutokana na kukabiliwa na shtaka la uhaini ambalo halina dhamana anaoimba Mahakama kufanya marejeo ya mwenendo wa Kesi ya 'kutoa taarifa za uongo mtandaoni' ambayo inasikilizwa mbele ya Mh.Hakimu Mfawidhi Muhini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu .

Kesi hiyo ya marejeo ambayo imetajwa leo June 17, 2025 ilikuwa inakuja kusikilizwa mbele ya Mh.Jaji Mkwizu.

Baadhi ya Mawakili waliofika mahakamani kumuakilisha Lissu ni pamoja na Wakili Hekima Mwasipu, Wakili Paul Kisabo,Wakili Jeremiah Mtobesya .

Kesi hizi ni upuuzi tupu na kupoteza muda wa Mahakama.

Mahakama badala ya kushughulikia Kesi za msingi Sasa inahangaika na masuala haya ya kipuuzi!!
 
Back
Top Bottom