Kesi ya Marejeo ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri Na. 14496 ya 2025 imeahirishwa leo katika Mahakama Kuu-Dar es Salaam hadi Juni 27 saa tatu asubuhi, ambapo Mahakama imeagiza TunduALissu kuletwa Mahakamani ili kesi isikilizwe 'Physically'
Katika shauri hilo Lissu ambaye yupo Gerezani kutokana na kukabiliwa na shtaka la uhaini ambalo halina dhamana anaoimba Mahakama kufanya marejeo ya mwenendo wa Kesi ya 'kutoa taarifa za uongo mtandaoni' ambayo inasikilizwa mbele ya Mh.Hakimu Mfawidhi Muhini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu .
Kesi hiyo ya marejeo ambayo imetajwa leo June 17, 2025 ilikuwa inakuja kusikilizwa mbele ya Mh.Jaji Mkwizu.
Baadhi ya Mawakili waliofika mahakamani kumuakilisha Lissu ni pamoja na Wakili Hekima Mwasipu, Wakili Paul Kisabo,Wakili Jeremiah Mtobesya .