Mahakama Kuu yamhukumu Grace Mushi kunyongwa hadi kufa kwa kumchoma mpenzi wake ndani ya nyumba mpaka kufa

mshahara wa dhambi ni mauti 🐒
 
All in all, sisi sote tu wenye dhambi, na tumepungukiwa na utukufu wa Mungu, Mungu anatupenda sote hivi hivi tulivyo, wengine wachawi, wengine wauaji, wengine wazinzi, wengine waongo, wengine wezi, wengine dhambi mbalimbali, Mungu anatuhitaji sote hivi hivi tulivyo tuipokee neema ya Wokovu kwa njia ya Yesu Kristo. huyo hivyo hivyo anavyoonekana na kuhukumiwa Mungu anampenda na anahitaji roho yake ipone, watu ndio tujue ukiwa nje ya Yesu lolote linaweza kukupata, shetani anaweza kukutumia kufanya kitu cha ajabu kabisa halafu ukinasa anakuacha anakutelekeza, sivyo alivyo Yesu, amesema yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe, na kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.

nakushauri wewe ambaye maisha yako bado yapo mikononi mwa shetani, mwisho wako hautakuwa mzuri ama hapa duniani ama baada ya kifo, ni heri kuwa mikononi mwa Mungu, heri uyakabidhi maisha yako kwa Mungu leo, uokoke, nawe utamwona Mungu katika maisha yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…