Mahakama Kuu yatengua hukumu ya kuvuliwa Uwakili dhidi ya Fatuma Karume

Mahakama Kuu yatengua hukumu ya kuvuliwa Uwakili dhidi ya Fatuma Karume

iyo katiba itakusaidia nini kwa sasa

nchi inahitaji mambo mengi zaidi ya katiba mpya
Ikiwa kama kiongozi anaweza kuamua nani ahukumiwe na nani aachwe basi bila shaka hatutanyamaza , ni mpaka itengenezwe Katiba mpya itakayoonda Rais kuwa mungu
 
Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia muda huu kutoka Mahakamani .

Taarifa inaeleza kwamba Mahakama kuu imeona kwamba Fatuma Karume alihukumiwa bila kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya Kamati ya maadili ya Mawakili , hivyo imetengua hukumu yake na kuitaka Kamati hiyo kumaliza jambo hilo kwa haki

Ikumbukwe kwamba Mlalamikaji kwenye hili Sakata la Wakili Msomi Fatuma Karume lililojaa chuki , Wivu na uzandiki alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Je unadhani bado anafaa kukalia ofisi hiyo ?

View attachment 1825533
Lile jitu life mara 1000 huko kuzimu. Mungu ibariki Tanzania. Mungu mbariki Rais wetu SSH mpe miaka mingi atuongoze mpaka nchi na demokrasia inyooke. Hongera sana Wakili msomi Fatuma Karume.
 
Kila jiwe halitaachwa salama, kazi iendelee.


Tufanye rejea: 20 Septemba 2019

Fatma Karume: Mwana wa Abeid Karume avuliwa uwakili Tanzania​

20 Septemba 2019
Wakili Fatma Amani Abeid Karume ni mwana wa aliyekuwa rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume

CHANZO CHA PICHA,FATMA KARUME/FACEBOOK
Wakili Fatma Karume amesimamishwa kufanya kazi za Uwakili Tanzania bara,

Maamuzi hayo yametolewa na Jaji Feleshi kwenye kesi iliyofunguliwa na katibu wa Uenezi wa chama cha ACT wazalendo Ado Shaibu akipinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG).

Hatahivyo Fatuma Karume amesema kuwa maamuzi hayo yametolewa bila yeye kusikilizwa.

Mahakama Kuu imeamuru Fatma apelekwe kamati ya maadili kwa madai ya kushambulia ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

Karume amesimamishwa kazi huku sababu yake
ikitajwa kuwa kile alichokizungumza katika kesi iliofunguliwa na katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano katika chama cha Wazalendo, Ado Shaibu kupinga uteuzi wa Mwanasheria mkuu wa serikali Dkt Adelarus Kilangi

aliyeteuliwa na rais John Pombe Magufuli mnamo February Mosi 2018 kulingana na gazeti la Mwanachi.

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
Shaibu amesema kwamba mawakili wa serikali walilalamikia maneno yalioandikwa na Fatma wakati walipokua wakifungua kesi hiyo mahakama kuu.

''Na nakuu gazeti la mwanachi: hata iwapo kesi hii itashindwa ataendelea kupambana nayo, rais akiondoka madarakani mwaka 2020 au kama ataondoka 2025 au kama mahakama itabadilika ataendelea kupambana''.

Shaibu amenukuliwa na gazeti hilo akisema kwamba uamuzi huo umetangazwa huku madai katika kesi ya msingi yakitupiliwa mbali kwa hoja kwamba rais hawwezi kusimamishwa mahakamani.

Alipoulizwa kuhusu hatua dhidi yake, fatma amesema kuwa anakusudia kufungua kesi katika mahakama ya haki afrika mashariki EACJ kupingana kusimamishwa kwake uwakili bila kupewa nafasi ya kujieleza.

Amesema kwamba hashangai kusimamishwa kazi au kuvuliwa uwakili kwa sabbau yapo mengi yaliotokea nchini,
Mimi sishangai kuvuliwa au kusimamishwa uwakili ,pengine Mungu hataki niendelee kuwa huko , pengine anataka niingie kwenye siasa au nifanye kingine tofauti. Nitakaa na kutfakari alinukuliwa na mwananchi akisema.

Hatahivyo amesema kwamba hatua hiyo haitabadili maisha yake bali itabadilisha uwezo wake wa kusimamia kesi za kikatiba , akibainisha kuwa bado ni wakili Zanzibar, ana ofisi na ataendelea kusimamia kesi za kikatiba.
Source : courtesy of Kwanini Fatma Karume amevuliwa uwakili Tanzania? - BBC News Swahili
 
Na mambo haya yanatokea kwa kasi sana. Yaelekea mama alikuwa amechefukwa lakini hakuwa na la kufanya. Mungu kamfanyia wepesi
Waswahili walisema pia "Funga bakuli, mwanaharamu apite".

Mama alijua maana ya methali hii, ndiyo maana muda wote akawa kafunga bakuli, sasa mwanaharamu kapita, tumejua mbivu mbichi kuhusu amesimamia wapi.
 
Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia muda huu kutoka Mahakamani .

Taarifa inaeleza kwamba Mahakama kuu imeona kwamba Fatuma Karume alihukumiwa bila kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya Kamati ya maadili ya Mawakili , hivyo imetengua hukumu yake na kuitaka Kamati hiyo kumaliza jambo hilo kwa haki

Ikumbukwe kwamba Mlalamikaji kwenye hili Sakata la Wakili Msomi Fatuma Karume lililojaa chuki , Wivu na uzandiki alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Je unadhani bado anafaa kukalia ofisi hiyo ?

View attachment 1825533
Bila kupepesa macho ile mamlaka iliyoamua ku suspend uwakili wa Bi Fatma ilikengeuka sana. Jopo likikuwa chini ya Jaji Kiongozi Feleshi na wenzie. Bi Fatma alisema "Feleshi kanivua uwakili wakati nilikuwa sipo Mahakamani. Hajanipa notice ya malalamiko dhidi yangu na wala kunipa muda wa kujitetea. Pengine Siasa na si Mahakama ndio italeta mabadiliko."

Kama Jaji Kiongozi Eleazar Feleshi alivunja msingi mkubwa wa haki 'right to be heard', basi HASTAHILI kuwa msimamizi wa Mahakama Kuu, chombo kikubwa cha kutoa haki nchini.

Kama Jaji Kiongozi anakwngeuka hivyo, itakuwaje kwa Majaji walio chini yake na Mahakimu?

Kwa ajili ya kulinda heshima ya Mahakama ni bora Rais SSH ambadilishie Jaji Feleshi majukumu atuletee Jaji atakayefanya kazi kwa haki bila uwoga.
 
Back
Top Bottom