Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,524
- 13,682
Kiukweli kabisa sasa imethibitika kabisa kuwa mahakama zetu hutoa hukumu kwa maelekezo ya serikali.Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia muda huu kutoka Mahakamani .
Taarifa inaeleza kwamba Mahakama kuu imeona kwamba Fatuma Karume alihukumiwa bila kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya Kamati ya maadili ya Mawakili , hivyo imetengua hukumu yake na kuitaka Kamati hiyo kumaliza jambo hilo kwa haki
Ikumbukwe kwamba Mlalamikaji kwenye hili Sakata la Wakili Msomi Fatuma Karume lililojaa chuki , Wivu na uzandiki alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Je unadhani bado anafaa kukalia ofisi hiyo ?
View attachment 1825533
Mahakama zetu hazina uhuru wo wote hivyo ni vema mahakama zikapigania haki yake kama ambavyo katiba inataka!