Mahakama ya ICSID: Professional bullying anayofanyiwa Profesa Mruma inafedhehesha jamii ya Wanazuoni

Mahakama ya ICSID: Professional bullying anayofanyiwa Profesa Mruma inafedhehesha jamii ya Wanazuoni

Sidhani kama ni sahihi kusema wameiaibisha Nchi. Unless hujui rigors za mahakamani wewe. Alicho kuwa anahojiwa Mruma ni uwepo na kushughudia nyaraka ya Hati ya dharura "certificate of urgency" Sababu zilizopelekea hiyo udharura. Nadhani tatizo ni upangaji wa mashahidi, kwamba nani aende aka shuhudie jambo gani alilohusika nalo kwa vipi. Purely maswala yale alipaswa kuuulizwa AG.

Iwe iwavyo, Tanzania tuna wasomi wazuri sana. Tattizo ni viongozi wetu. Kwamba viongozi wanaharibu mambo kwa mihemko Yao na maubaavu Yao baadae wasomi ndio waende kuetetea kilichotokea.

Ni vema wasomi Hawa Wakawa wanahusika na mambo yote toka mwazo na kushauri bila kuingiliwa ingiliwa na Viongozi.

Hata kama Kesi hii Tanzania itashindwa, tatizo sio wasomi (wanasheria) tatizo ni papara za Uongozi wa Nchi. Mfano sakata hili la madini Nina uhakika Magufuli alikuwa anali guide kwa nguvu sana. Na Alisha declare kuwa Nchi Iko katika vita ya kiuchumi na yeyote ambaye angeenda kinyume alipaswa kuwa dealt with. Nina hakika wakumshauri ukweli, walijawa na woga na wakasema kile kilichomfurahisha.

Mambo ya Kesi mahakamani hayaendeshwi kwa mihemko na hisia za kisiasa, Bali yanahitaji hoja, ushahidi, na logic. Yeye alijigamba amekuwa serikalini kwa Miaka 20 hivyo hakuna asichokijua.

Ifike mahali wataalam wetu waaminiwe na watoe ushauri kwa uweledi na sio kwa kuongozwa na woga au kumfurahisha mtawala.
Lakini pia maana ya kuwa msomi ni kusimamia unachokiamini hata kama kitakugharimu. Msomi unayeyumbishwa na kukubali kuwa mjinga mbele ya wajinga, wewe ni msomi njaa.
 
Kina Mruma si ndio tuliambiwa ni Ma nguli nchini hapa[emoji3]
Hawa maprofesa feki Mruma na mwingine Ososrro ndio walimuingiza chaka Magufuli kenye MAKINIKIA mpaka akatuahidi NOAH kila mwananchi lakini mwisho akasepa bila kutupa NOAH zetu!! Bado mnawaamini Mruma na OSORRO ambao wanatakiwa kuwa jela kwa kumshauri vibaya Jiwe?

Serikali itafute watu wengine competent kwenye mambo ya sheria zetu ndio waende kutuwakilisha kwenye hizo kesi zilizobaki na Mruma na huyo mwenzie wasionekane tena huko!!
 
Kama wengi mnavyofahamu, Tanzania imekuwa ikishtakiwa na makampuni ya madini kwenye mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara, ICSID kwa kosa la kufuta leseni za makampuni ya kigeni yaliyokuwa yameingia nchini kwa kufuata sheria zote, kisha yakafanya utafiti, na baadaye kupewa Retention Licenses, halafu kwa ubabe, Serikali ikazifuta leseni hizo.

Kampuni zilizokuwa zimefanyiwa uhuni huo ni takribani 6, mpaka sasa kampuni 3 zimefikisha malalamiko yake kwenye mahakama ya ICSID. Shauri la kwanza lilikuwa ni la kampuni ya Indiana, limekwisha, kama ilivyotegemewa, Tanzania tumeshindwa, na tumeamriwa kuilipa fidia kampuni ya Indiana ya Australia AUD 127m (zaidi ya shilingi bilioni 210). Montero ya Canada inadai fidia ya CAD 90m (zaidi ya shilingi bilioni 170), na Winshear ya Canada inataka fidia ya CAD 124m (zaidi ya shilingi bilioni 230).

Kesi ya pili inaendelea sasa, ikiwa kwenye hatua ya mwisho, na hakuna dalili yoyote ya Tanzania kushinda. Kesi ya 3, kati ya Montero v. Tanzania nayo inaendelea.

Kesi ya pili ni:

Winshear Gold Corp. V. United Republic of Tanzania (ICSID Case No. ARB/20/25).
Kesi hii ipo chini ya Rais Gabrielle Kaufmann Hohrer kutoka Uswizi.

Mashahidi wetu huko ni Prof. Mruma na Mwanasheria wa Serikali bwana Igenge.

Nimesikiliza mahojiano kati ya Wakili wa Winshear bwana Fordin na Prof. Mruma na mwanasheria Igenge, kwa kweli ni aibu tupu. Mapungufu yapo kuanzia kuonekana mtu unasema uwongo, kushindwa kuelewa maswali yanayoulizwa, kutoa majibu ya kujichanganya, kushindwa kuelewa hata sheria zetu, mpaka kushindwa kuongea Kiingereza vizuri. Igenge muda mwingine akabakia kusema tu yes, lakini akimaanisha no. Ni aibu tupu.

Nadhani hawa mashahidi walichokuwa wanaangalia zaidi ni kupata tu posho zao lakini siyo kufanya chochote cha maana. Fikiria mtu kama Igenge, eti ni mwanasheria, halafu hazielewi hata sheria zetu. Yaani mawakili wa Winshear ambao siyo Watanzania, inaonekana wanazijua vizuri zaidi sheria zetu kuliko wanasheria wetu.

USHAURI KWA SERIKALI:
Kama hatuna mashahidi kwa sababu utetezi wa kimaandishi tulioutoa ni wa uwongo, au tunaona hatuna utetezi, si afadhali tuwaite hao wanatushtaki, tukubaliane kuwalipa hiyo fidia wanayotudai kuliko kuendelea kuongeza hasara kwa kuwalipa watu kwenda huko Marekani wakati tunajua hawana msaada wowote, na wala hawawezi kubadilisha chochote?

Yaani tuwalipe hawa walioenda kutalii Marekani, halafu tuwalipe tena wanaotudai, hasara mara mbili, na wala hatujifunzi chochote.

Viongozi wa Serikali ni watu wa ajabu ajabu sana. Ni watu wanaopenda kutumia zaidi nguvu kuliko akili. Hawawezi hata kuelewa kwa nini tembo pamoja na ukubwa wote, na nguvu zote, lakini anaishi mwituni, na mwanadamu ana uwezo wa kumwua wakati wowote. Binadamu asiyetumia akili lakini anajivunia mabavu, hana utofauti na mnyama. Anaweza kufanywa chochote na wanaotumia akili. Usiyetumia akili, wakati ukifika utanyolewa na wanaotumia akili.

Nchi hii ni masikini sana katika kutumia akili, ndiyo maana kidogo tunachokipata kinachukuliwa na wenye akili. Sasa zile tozo za kwenye miamala ya akina mama nitilie zinaenda kuwalipa matajiri wa Indiana Resources, Winshear Corp na wengineo wanaotushtaki.

Kama una muda na bando la kutosha sikiliza mashahidi wetu Prof. Mruma na Igenge wanavyonyolewa bila maji na mawakili wazungu.

PROF. NA WAKILI WAKE AIBU KUBWA
 
Sikioni Profesa Mruma alichoshindwa kuelewa na alichoshindwa kujibua Bado naendelea kutazama clip
Acha kujitoa ufahamu wakati nchi imevuliwa nguo na vilaza wakubwa. Profesa mzima anajibu maswali kwa kuzingusha mkono au kutikisa kichwa? Profesa mzima anafundishwa namna ya kujieleza na mpinzani wake tena kijana mdogo tu? Pumbavu kabisa!
 
Serikali ya CCM ndiyo iliyowa invite Wawekezaji kuja kuwekeza humu nchini. Serikali hiyo hivyo wakatumia ubabe kuvunja mikataba bila kufuata utaratibu.

Ningeshauri wahusika wote washitakiwe humu humu nchini kwa kesi ya uhujumu uchumi. Pili fidia zote zilipwe kwa fedha za CCM na sio fedha za umma. Hili litasaidia hawa Wajanja wachache kujifunza kuwa Umma hauchezewi.

ROYAL TOUR SI NDIO ILIKUWA VEHICLE YA KUWASHAWISHI WAWEKEZAJI?
 
Mimi nashangaa sana Mwanasheria kuwa goigoi kwenye lugha ya Kiingereza, hii inawezekanaje?

Hivi kweli mtu unasoma hadi level ya kuwa na PhD halafu unashindwa kumudu lugha uliyotumia kujifunzia? Uliandika vipi hayo maandiko?
Kiingereza cha kuandika wa level ya PHD ataandika vizuri tu tatizo kuongea sasa na ukute anaongeleshwa na mtu ambaye english ndo lugha yake aisee atatamani ardhi ipasuke afichwe kingine kumbuka hao mawakili walioenda huko si ajabu kukuta hawana uzoefu wa kuwakilisha washtakiwa kwenye mashauri magumu na kwenye mahakama za kimataifa usije fikiri wakili aliyezoea mahakama za kisutu eti ataweza shindana na maadvocate ambao leo yupo mahakamani new york kesho yupo paris mtondogoo yupo london keshokutwa yupo durban wiki ijayo yupo sao paulo wiki ijayo yupo abu dhabi
 
PROF. NA WAKILI WAKE AIBU KUBWA

Sio aibu tu hawa watu wametutia hasara kubwa sana ya mabilioni ya shilingi ; wanatakiwa jamii iwatenge kama sio kuwafunga! Fedha za kuwalipa hawa jamaa zinatokana na kodi Samia anazoongeza kila siku hivyo kuwa mateso makubwa kwa wananchi masikini sababu ya ubwege wa hawa jamaa.
 
Hawa maprofesa feki Mruma na mwingine Ososrro ndio walimuingiza chaka Magufuli kenye MAKINIKIA mpaka akatuahidi NOAH kila mwananchi lakini mwisho akasepa bila kutupa NOAH zetu!! Bado mnawaamini Mruma na OSORRO ambao wanatakiwa kuwa jela kwa kumshauri vibaya Jiwe?

Serikali itafute watu wengine competent kwenye mambo ya sheria zetu ndio waende kutuwakilisha kwenye hizo kesi zilizobaki na Mruma na huyo mwenzie wasionekane tena huko!!
[emoji3][emoji3]
 
Mtu aliyempeleka huyu bwana kutuwakilisha kwenye hii kesi must be criminally prosecuted. Ni lazima kulikuwa na conspiracy kuwa ile kesi nchi ishindwe ili watu wapate mgao wao!! How come huyo jamaa anashindwa hata kuzungumza? You cannot win when you send zombies like this man to represent you!
Kbsaa yaani nililiwaza hili mapema jmn mm ccm lkn SAS inatosha tunatakiwa tuondoke haraka madarakani huu Ni upuzi haki ya nani
 
Back
Top Bottom