Sidhani kama ni sahihi kusema wameiaibisha Nchi. Unless hujui rigors za mahakamani wewe. Alicho kuwa anahojiwa Mruma ni uwepo na kushughudia nyaraka ya Hati ya dharura "certificate of urgency" Sababu zilizopelekea hiyo udharura. Nadhani tatizo ni upangaji wa mashahidi, kwamba nani aende aka shuhudie jambo gani alilohusika nalo kwa vipi. Purely maswala yale alipaswa kuuulizwa AG.
Iwe iwavyo, Tanzania tuna wasomi wazuri sana. Tattizo ni viongozi wetu. Kwamba viongozi wanaharibu mambo kwa mihemko Yao na maubaavu Yao baadae wasomi ndio waende kuetetea kilichotokea.
Ni vema wasomi Hawa Wakawa wanahusika na mambo yote toka mwazo na kushauri bila kuingiliwa ingiliwa na Viongozi.
Hata kama Kesi hii Tanzania itashindwa, tatizo sio wasomi (wanasheria) tatizo ni papara za Uongozi wa Nchi. Mfano sakata hili la madini Nina uhakika Magufuli alikuwa anali guide kwa nguvu sana. Na Alisha declare kuwa Nchi Iko katika vita ya kiuchumi na yeyote ambaye angeenda kinyume alipaswa kuwa dealt with. Nina hakika wakumshauri ukweli, walijawa na woga na wakasema kile kilichomfurahisha.
Mambo ya Kesi mahakamani hayaendeshwi kwa mihemko na hisia za kisiasa, Bali yanahitaji hoja, ushahidi, na logic. Yeye alijigamba amekuwa serikalini kwa Miaka 20 hivyo hakuna asichokijua.
Ifike mahali wataalam wetu waaminiwe na watoe ushauri kwa uweledi na sio kwa kuongozwa na woga au kumfurahisha mtawala.