Mahakama ya ICSID: Professional bullying anayofanyiwa Profesa Mruma inafedhehesha jamii ya Wanazuoni

Mahakama ya ICSID: Professional bullying anayofanyiwa Profesa Mruma inafedhehesha jamii ya Wanazuoni

Hazifutiki..

Mimi pia nimeshangaa kumbe hawa ICDS wana YouTube channel Yao na hearing ya kesi hii yote imepositiwa huko..

Kuna video za kesi hii part 1 hadi 7 na zote ni za masaa kati ya 2 hadi 3½ ..

Ama kweli sasa dunia hii ni ya uwazi mno. Bila shaka hata Tanzania tunahitaji kesi zote zisikilizwe Kwa uwazi wa namna hii...
Mkuu, hapo jirani Kenya kesi zipo wazi tena nyingine online...

Huku kwetu hawataki haya mambo...
Baadhi ya kesi zimetengenezwa / kubambikiziana... Sasa zikiwa live italeta shida...
Kesi ya Mbowe kipindi kile ilikuwa live kwenye mitandao ila wakubwa hawakupenda
 
Hivi Mruma ni mtaalamu wa Sheria ama yule ni Geologist?

Why serikali inawatuma watu wa miamba wakalitetee taifa kwenye maswala ya Kisheria?

Muda mwingine unaweza kufikiria kuna baadhi ya watu wanataka Tanzania ishindwe, idaiwe Mabillion kisha nao wapate mgao.
Umeuliza swali linaloniumiza kichwa sanaaa Kuna watu wanapaswa kuwajibika katika hili

Tatizo viposho so Kila sehemu mtu awepo tu Kwa sababu yeye ni Fulani ona kashachafua Kila kitu.
 
… …
MSOMI: But you need to do expiration to solve that sometimes don't, don't you?

MRUMA : No.

MSOMI : Nooo!

Mruma: Not my understanding.

MSOMI : So if if someone gets ……license. They can have it for up to 10 years if it's extended. Do you think it's in Tanzania''s public interest for someone to simply do nothing for that entire 10 years? Is that your position?

MRUMA : We give you that period so that as you said price issues are global to be corrected and that's why we…... But not not. That's not right.

MSOMI : That's not my question. My question is during that 10 years….
Mruma: No more exploration, No more exploration after extension linces

MSOMI: Would you not agree with me that it's always in the public interest? To further explore, define and delineate mineral resources in the country. Can we at least agree that?

MRUMA: It is… … it is……

MSOMI: That's what you would tell your students at the University of Dar es salaam (UDSM)

MRUMA: Precisely Yeah,

MSOMI: don't explore ,Leave it alone[emoji1787] [emoji1787]

Kazi ipo
Kaka unajuwa hakika ujasoma kayumba
 
Kakosea wapi ? Wakati kesi tumeshindwa Kwa kuvunja mikataba ya hovyo.

Kwamba yeye alipanga kushindwa basi asingeenda kabisa,mbona una akili za kitoto sana .!!

Kila kitu unaangukia kweny upande wa siasa ndo tatizo Bado akili haijakomaa.
Hii mikataba ya hovyo, serikalini wameonywa toka lini ?!. Mbona wanayaingia kwa makusudi na kila mahali sasa tunashindwa kesi hizo.

Sijui unatetea nini, ni kama hujui nini cha kuchangia humu. !!

Professors Mruma na Osoro walipoambiwa professorial rubbish mliwaka. So what now ?!
 
Professor hata Kiingereza ni issue, lawyers siku zote ni washenzi na hapo wameshamsoma hawezi hata kujieleza kwa ufasaha kwa kiingereza, ni mashambulizi, next time watafute mkalimani au waajiri wanasheria wazungu kwenye timu yao ya utetezi, kesi tumeshindwa kabla haijaisha
Kama hatuwezi baadhi ya mambo tuombe tusaidiwe !! Sio aibu !! Au mlolongo wa kushindwa shindwa kesi nazo ni fursa kwa wajanja ??!!
 
Kwa, kuwa sote ni Watanzania Serikali wakati mwingine iombe hata backup kwa Kibatala au Tundu lisu
Hakika siasa sio uadui lakini wengine wanafikiri vinginevyo !

Mpaka wengine wapo kwa ajili ya kuwatengenezea kashfa wale ambao wanatofautiana nao kimtazamo !!
Kwa mtindo huo hatufiki popote !!
 
Tatizo kubwa la nchi hii watu hawana Professional Intergrity.
Wasomi wengi wanaendeshwa na Wanasiasa.

Kwenye la kuvunja mikataba wa kulaumiwa anajulikana wala sio Prof. Mruma
Watu wanajisahaulisha tatizo liko wapi. Shida ni Siasa kua juu kuliko taaluma
 
Sijaona tatizo la kiingereza kwa prof. Mruma, labda mimi ndio sijui zaidi.
Mlitaka profesa ajibu kitu kisicho kuwepo?

Kushindwa kwetu kesi ni hali halisi ya jinsi mambo yalivyokuwa.

Siku zile Lissu alitahadharisha, akaitwa msaliti.

Tujifunze sasa. Ukiona mtu ana kupinga mpe nafasi huenda kuna kitu utapata kikakusaidia.
 
Hii mikataba ya hovyo, serikalini wameonywa toka lini ?!. Mbona wanayaingia kwa makusudi na kila mahali sasa tunashindwa kesi hizo.

Sijui unatetea nini, ni kama hujui nini cha kuchangia humu. !!

Professors Mruma na Osoro walipoambiwa professorial rubbish mliwaka. So what now ?!
Huyo professor Mruma ni mwanasheria sio? acha kukurupuka hujui kitu
 
Profesa Mruma amepata pigo kubwa sana kwa umri wake; waliomtuma huko Duniani wamedhamiria adhalilishwe na lengo limetimia . Anaulizwa kwa fedheha " haya ndiyo unawafundisha wanafunzi wako wa UDSM?

Muuliza swali ni mtoto wake wa kumzaa. Kwanini tumeruhusu wasiojiweza watusimamie?

---
Winshear Gold Corp. Vs. United Republic of Tanzania (ICSID Case No. ARB/20/25).
Kesi hii ipo chini ya Rais Gabrielle Kaufmann Hohrer kutoka Uswizi.

Mashahidi wetu huko ni Prof. Mruma na Mwanasheria wa Serikali bwana Igenge.


---
Video 1: Profesa Mruma akihojiwa
View attachment 2698386

Video 2: Mkurugenzi wa Huduma za Sheria(Wizara ya Madini) Edwin Igenge akihojiwa na Robert Denison
View attachment 2698385

---
WASIFU WA PROFESA MRUMA

Dkt. Mruma ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye kwa sasa ni Profesa wa Jiolojia. Profesa Mruma kwa sasa anahudumu kama Kamishna wa Tume ya Madini nchini Tanzania.

Mwaka 2017 Hayati Rais Magufuli alimteua Prof. Abdulkarim Mruma kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta (TIPER)

Profesa Mruma alijizolea umaarufu 24 Mei, 2017 baada ya kuongoza Kamati maalum iliyondwa na Rais Magufuli kuchunguza mchanga ulio katika makontena yenye mchanga wa madini (makinikia) yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania

-
Dkt. Abdulkarim Hamisi Mruma Ph.D. M.Sc. B.Sc. ni Mkurugenzi wa Kujitegemea wa Tanzania Royalty Exploration Corporationration. Dkt Mruma ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako kwa sasa ni Profesa wa Jiolojia.

Masomo yake ya Uzamili yalijumuisha tafiti katika vyuo vikuu na taasisi za Serikali nchini Ujerumani, Ubelgiji, Zimbabwe na Ufini.

Ameandika ripoti za kiufundi kuhusu mada mbalimbali za kijiolojia na kuchangia katika majarida kadhaa ya kiufundi na yasiyo ya kiufundi juu ya anuwai ya masomo ya Jiolojia.

Orodha ya machapisho hayo ni pamoja na Jarida la UNESCO la Sayansi ya Ardhi ya Afrika na Jarida la Tanzania la Sayansi ya Dunia.

Mbali na majukumu yake ya kitaaluma, Dk. Mruma ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania nafasi ambayo ameitumikia tangu Oktoba 2004.

Pia anahudumu kama Mjumbe wa Bodi ya Chuo cha Sayansi za Ardhi cha Williamson Diamonds Limited cha Chuo Kikuu cha Dodoma na Shirika la Madini la Taifa la Tanzania mshirika wa ubia wa Kampuni ya Uboreshaji wa Mradi wa Buckreef Gold Mine.
Tungewapeleka magwiji wa sheria kama Mh. Chenge, Prof. Kabudi, Prof.Shivji na Dr.Nshalla angalau tungefurukuta. Vinginevyo tungewaajiri wanasheria maarufu wa huko huko.
 
Hawa Watanzania kwa kuchanganya R na L mpaka wanatia kichefuchefu.

Hivi hizo shule walienda kusomea ujinga?

 
Nimekumbuka Kikwete alivowekwa mtu kati na Shaka Ssali wa VOA, dingi akaanza kuongea kama engine yenye miss
 
ndio maana maishani mwangu sijawahi kuheshimu profesa hata mmoja, naonaga wendawazimu tu waliochanganyikiwa na kitabu hata hawana uwezo kufanyia kazi elimu yao. ona sasa anadhalilishwa na vitoto vidogo havina hata masters.
Wao wanatakiwa kufundisha tu

Ova
 
Remind me of Captain Queeg in The Caine Mutiny.

Talk about life being stranger than fiction!
 
Ogopa sana kukaa meza moja ya majadiliano na watu wanaojua jambo lao.Iwe Mweusi au Mweupe.

Halafu wewe uwe ndio mchorwaji katika majadiliano.
 
Back
Top Bottom