Mahakama ya kadhi ndani ya Katiba - Tanzania

Mahakama ya kadhi ndani ya Katiba - Tanzania

Kuna uvumi kuwa bunge maalum la katiba limeongeza kifungu kipya kinacho ruhusu uwepo wa MAHAKAMA YA KADHI ndani ya katiba mpya.
Jambo hili tayari limeanza kuanzisha mijadala
indani ya forum yetu,na zimaanza kuleta hisia za udini.Wako wanaodhani kuwa uwepo wa mahakama hizo ni kama kuisilimisha Tanzania.Wako wanaoihusisha na vita vya kidini,lakini hawatowi hoja zilizo na mashiko Ajabu hii,watanzania na imani zetu tulio owana na kuchanganya damu bado tunaogopana?Serikali ni yetu wote.kama tunaipa dhamana fulani yenye maslahi kwa dini fulani yasiyo idhuru dini nyingine kuna ubaya gani?Mbona hata wakiristo wanafungu kubwa la fedha wanachotewa toka serikalini ili luendesha taasisi zao kama mahospitali na vyuo na tumeridhia.! Kwasababu sisi ndio wadau husika wa taifa na hizi ndizo haja zetu.Kwa nini munataka kuzua mgogoro wa kijinga?Waislamu ni sehemu ya Taifa hili .Katiba inayohaki ya kuweka utaratibu wa kila kundi katika taifa wa kuendesha shughulozake za kidini kwa uhuru na haki bila ya upendeleo wala kuathiri imani nyingine
Ila naona wanasaha:-
 
Kwa nchi kama Tanzania si sahihi kuweka mambo ya dini ndani ya katiba.Sababu ni nchi kwanza yenye watu wa dini nyingi mno na wapagani wengi mno,Kuweka ndani ya katiba ni kama kupendelea kundi fulani katika jamii kwa kuangalia imani ya mtu.kitu ambacho hakitakiwi kuonekana katika katiba.Hata katika ajira za umma sasa hivi ni marufuku mtu kuonyesha ni dini gani sababu lengo la ajira za umma hazilengi dini ya mtu.Sasa serikali ukisema haina dini utawekaje tena kipengele cha dini fulani kwenye katiba?

Pili ni namna ya kupata pesa hizo mahakama za kadhi Kiutaratibu watu wanataka serikali ndio iendeshe hizo mahakama za kadhi kwa kutoa hela.Swala ni kuwa kumtoza mtu asiye mwislamu kuendesha uislamu, uislamu hauruhusu kabisa.Huwezi kuchukua kodi ya mkristo au mpagani kwa ufupi kafiri ukajenge msikiti au kumlipa imamu na kadhi!

Tatizo kubwa lingine linapokuja ni hivi Tanzania kodi kubwa inatokana na pombe mahakama ya kadhi ikitaka kodi za kuendeshea hizo mahakama ina maana inataka ipate mgawo toka kwa walevi ili waendeshe hizo mahakama! Ni mtego kwa uislamu na waislamu.Hayo mambo yafaa zaidi kwenye nchi za kiislamu ambako pesa yao inatokana na biashara halali na si za kutoza kodi za pombe,madanguro, na kodi za wauza bucha za nyama za nguruwe.
 
Waislam wa tz ni kundi kubwa wanahaki ya kupata kila kitu kutoka serikalini kama makundi mengine ya wtz..
Umesema kipengele cha dini ya muombaji ktk ajira kimeondolewa hiyo ni hatua 1 mbele tutegemee kuondolewa kipengele hicho Polisi,Hospitali na sehemu zingine.na tutegemee pia makabila yetu kuondolewa pia ibaki utz wetu tu.
Lakini ufaham hapa tz kuna mahakama na zinashughulikia kesi za waislam za kiislam je huwoni kama zinaigharimu serikali pesa nyingi.?
Tz kunamahaka za nyumba zinazo gharamiwa na serikali je wtz wote wananyumba? Pia tuna mahakama ya biashara na serikali wanaigharamia je wtz wote ni wafanya biashara? Unapozungumzia gharama kwa serikali huo ndio wajibu wa serikali kutafuta pesa ili kuweza kuhudumia wananchi wake.na uhalali wa pesa ktk uislam hilo lisikusumbuwe mbona hukusema kodi zinazokusanywa kutoka vyanzo vingine kama azam,mo,oil com,lake oil,azani nk.
Hili suala la kadhi ni jepesi tu ila kwa mtu usie watakia mema waislam wa tz kama vile Lukuvi utaliona ni gumu na baya..hebu lifanyie utafati msikurupuke tu
 
Lakini si mlipita mitaani kutaka maoni ya wananchi? Sasa wananchi wa kiisalamu wanataka Mahakama ya Kadhi, hayo ni maoni yao, kwanini hamtaki kuyaheshimu?. Laana ya Udini ndio inaitafuna rasimu ya Katiba ya Joseph Warioba, Joseph Butiku na John Kabudi.
Pole pole kitaeleweka tu!

Halijaharibika neno. Hapo ndipo tunapohitaji utaalamu wa mabingwa wa katiba kutuongoza technically nini kiwekwe kwenye katiba, na sio wanasiasa muchwala kama wa kwetu- wajali matumbo na si mustakabali wa taifa
 
mahakama yan kadhi,baraza la walei, baraza la kkt,baraza la ephata,baraza la fulu gospel,baraza la ufufuo,daahh hii katiba itakuwa safi sana haki bin haki kila dhehebu linaruhusiwa kuwa na chombom cha maamuzi na kutoa hukumu na tena mahakama ya kdhi ruksa kutoa adhabu za mawe na kukatana mikono na vichwa
 
Lakini ufaham hapa tz kuna mahakama na zinashughulikia kesi za waislam za kiislam je huwoni kama zinaigharimu serikali pesa nyingi.?

Mahakama za Tanzania hazijawahi wala hazishughulishi na kesi za dini.Mahakama za tanzania zinaendesha kesi za wahalifu au wagombanao.Kesi hizo zaweza kuwa za wahalifu au wagombanao kwa mambo ya ndoa,mirathi n.k wanaotaka talaka au kurithi mali za marehemu.Au zaweza kuwa kesi za watu wahalifu wagombanao misikitini au makanisani kwa kutwangana mabakora wakigombea misikiti au makanisa au mali za misikiti au makanisa na kusababisha uvunjifu wa amani n.k

Mahakama zetu hazina dini na hazijawahi kuwa za dini.Hela zimetumika sawa tu.Hakuna muislamu anayeweza kwenda mahakamani ni mhalifu na mgombea kitu fulani tu ndio aweza onekana huko.Ukiona mtu aenda mahakamani ujue si mkristo wala muislamu ni mhalifu au mgombea kitu fulani aweza kuwa kavaa koti la dini lakini ni either mhalifu au mgombea kitu.
 
mahakama yan kadhi,baraza la walei, baraza la kkt,baraza la ephata,baraza la fulu gospel,baraza la ufufuo,daahh hii katiba itakuwa safi sana haki bin haki kila dhehebu linaruhusiwa kuwa na chombom cha maamuzi na kutoa hukumu na tena mahakama ya kdhi ruksa kutoa adhabu za mawe na kukatana mikono na vichwa

Inamaana haujui tofauti ya hivyo unavyo visema au ndio hicho kiroba ndani ya Mtori kinavyo kutuma???. Unalinganisha kuku na mende!
 
Bona watanzania wenzangu muna jazba!
Katiba lazima iweke taratibu za itawala kwa watu wote kiujumla na kimalundi na kwa kuzingatia maadili ya imani zetu tunazozihishimi na kuzilinda kwa usalama na mustakbali wa amani ya taifa.Wanaodhani kuwa jambo la mahakama liwe chini ya taasisi fulani ya dini na si serikali,wanafaya hatari ya utii kwa serikali kuondoka,na pengine kusababisha migogoro uraiani.Kwani hawa makadhi ambao ni watu tu wa kawaida mitaani watakosa nguvu za kulazimisha maamuzi yenye ukinzani wa pande mbili.mfano mke kafiwa na mumewe,ndugu wanataka kumnyima haki stahiki ya mirathi kidini,hukumu ya kadhi isiyo na nguvu ya dola haitotekelezwa. Hali hiyo hiyo kinyume chake
 
Ndugu zangu, nimeshtushwa sana na habari niliyoisoma hata jukwaani kwamba ccm inaandaa sura mpya katika katiba ya nchi itakayosimamia mahakama ya kadhi. Sichukii dini na imani za watu lakini ninaangalia amani na mwelekeo wa tiafa hili kwa sasa. Kwa muda wote katia historia ya nchi yetu, serikali haijawahi kuwa na dini lakini raia wake wamepewa uhuru wa kuabudu dini wanazozitaka ili mradi wasivunje sheria. Ni jambo lisilomithirika, kwa ccm kuiingiza nchi yetui kwenye dhahama hii wakat dunia nzima ikishuhudia tabu ambazo watu wanapata kutokana na kuwa na serikali zenye udini. Ninaomba ndugu zetu wa ccm, acheni jambo hili. Hamjalifanyia utafiti ila mnafanya kinafiki ili kuwa impress wazanzibar wawape 2/3 na kutafuta kura kwa misingi ya udini. Msitupeleke huko. Mnafanya jambo la hatari kuliko yote mliyowahi kufanya. Ninaomba suala la kadhi waachiwe waislam wenyewe walisimamie na kulitekelza kuliko serikali kujiingiza katika jambo la namna hii. Ninatetemeka, nashindwa kuandika. Wanaoitakia mema Tanzania, wakiwemo wana ccm, waisllam na watu wa dini zote, naomba tusimamie amani ya taifa hili ambayo sasa ccm imeama kuizika rasmi. SITA UMEFANYA LINI RESEARCH HADI UKA VALIDATE KWAMBA MAHAKAMA YA KADHI ITAONDOA KERO ZA MUUNGANO? UNA MAAGANO GANI NA DAMU YA WANTANZANIA?
we need a new honest conversation on how we as free people are going to defeat the forces of evil who stalk the planet!
 
Ndoo maana suala la kufunga na kuswal ijumaa havipo kwenye katiba so hatuna sababu ya kujadli mahakama ya kadh kwenye katiba ya watanzania.hiyo mkajadiliane mskitn
 
Mimi sina tatizo kama Waislamu wameamua
1. Kukatana mikono na miguu
2. Mwanamke kumiliki 1/3 ya mali aliyochuma na mme wake
3. Kuhukumiwa kifungo mwislamu anapobadili dini kutoka uislamu kwenda dini nyingine (Ref kesi ya Maryam wa Sudan)
4. Kuwalazimisha wasio kuwa Waislamu kutokula hadharani wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani (Ref Case ya Zanzibar)

Hata kama mambo hayo (call mahakama ya kadhi) yatainginzwa kwenye katiba, lakini PESA YANGU (read kodi yangu ya pombe) kuruhusu kwenda kuendesha hayo mambo ambayo kwanza yananikandamiza mimi mtoa pesa, THAT NEVER TO MY DEAD BODY.

Kikwete aliwaambia waislamu kwamba kama wanaitaka mahakama ya kadhi milango iko wazi, waanzishe na waindeshe wao wenyewe, Kesho yake Mufti Simba akateua makadhi wa mikoa yote ya Tanganyika. Hivi kuna ugumu gani waislamu kuendeshe hizo mahakama zao za kadhi?!

Ngoja tuone wale akina Yuda Isikarioti (Askofu (SIC!) Mtetemelwa) watakavyowauza Wakiristo wote kwa vipande vya fedha.
 
Umesema sahihi. Hatuhitaji kuishi maisha ya kinafiki na hasa unafiki huo unapopelekea umwagaji damu. Kuna watu wanasema hakuna tatizo Tanzania kwa kuwa kuna wazee watawaonya. Hao wazee wakusikilizwa wako wapi? Huko kulikooza na mizoga ya wanadamu hawana hata mtu wa kuwazika hapakuwa na wazee?

Iraq, Iran, Syria kabla hawajaingiza ushetani huu kwenye seriakli zilikuwa nchi nzuri sana. Watoto walienda shule wakicheza kwenye mwanga wa matumaini. Wazazi waliona kesho ya watoto wao kupitia nuru ya jua la jioni. Usiku walilala usingizi mwema wakiota ndoto za faraja na uzima.

Baada ya kuruhusu unafiki na kuingiza masuala ya dini hii kwenye serikali, ndipo ukawa mwanzo wa laana inayofanya anga la nchi za kiarabu ligubikwe na giza lililojaa miavuli myeusi inayopeperushwa na viumbe wenye kutisha. Wana sura na maumbile ya kibinadamu usoni lakini mifupa yao na maumbile wanayofunika yasionekane ni ya viumbe wasiotokana na jamii ya binadamu.

Nina rafiki zangu wako Pasktani na Afghan, wananiambia wanaishi kwa majuto na lawama ziko kwa wazazi wao walioshindwa kusimamia utaarabu na kupelekea waishi jehanum wakiwa bado duniani. Hakuna mtu mwenye amani hata mmoja.

we need a new honest conversation on how we as free people are going to defeat the forces of evil who stalk the planet!
 
Lakini si mlipita mitaani kutaka maoni ya wananchi? Sasa wananchi wa kiisalamu wanataka Mahakama ya Kadhi, hayo ni maoni yao, kwanini hamtaki kuyaheshimu?. Laana ya Udini ndio inaitafuna rasimu ya Katiba ya Joseph Warioba, Joseph Butiku na John Kabudi.
Pole pole kitaeleweka tu!

Utasubiri sana hiyo laana na pengine ikampata JK!
Soma hapo chini pengine utaelewa:

Mahakama ya kadhi yageuka kaa la moto!

.Aliendelea kusema Rais Jakaya Kikwete aliwahidi waislam kuwa Bunge litashughulikia suala hilo na kutoa maamuzi yatakayo waridhisha hivyo, Bw. Chikawe asiwachonganishe na Rais."Rais anania njema na waislam lakini Bw. Chikawe na jopo alilosaidiana nalo kufanya maamuzi hayo ndiyo wamepingana na nia ya Rais," alisema Mufti Simba
 
Mimi sina tatizo kama Waislamu wameamua
1. Kukatana mikono na miguu
2. Mwanamke kumiliki 1/3 ya mali aliyochuma na mme wake
3. Kuhukumiwa kifungo mwislamu anapobadili dini kutoka uislamu kwenda dini nyingine (Ref kesi ya Maryam wa Sudan)
4. Kuwalazimisha wasio kuwa Waislamu kutokula hadharani wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani (Ref Case ya Zanzibar)

Hata kama mambo hayo (call mahakama ya kadhi) yatainginzwa kwenye katiba, lakini PESA YANGU (read kodi yangu ya pombe) kuruhusu kwenda kuendesha hayo mambo ambayo kwanza yananikandamiza mimi mtoa pesa, THAT NEVER TO MY DEAD BODY.

Kikwete aliwaambia waislamu kwamba kama wanaitaka mahakama ya kadhi milango iko wazi, waanzishe na waindeshe wao wenyewe, Kesho yake Mufti Simba akateua makadhi wa mikoa yote ya Tanganyika. Hivi kuna ugumu gani waislamu kuendeshe hizo mahakama zao za kadhi?!

Ngoja tuone wale akina Yuda Isikarioti (Askofu (SIC!) Mtetemelwa) watakavyowauza Wakiristo wote kwa vipande vya fedha.

Hivi huyu Askofu ni wa Kanisa Gani ? Ebu tusaidieni yuko Kamati namba ngapi?

Huyu mzee na wasiwasi Imani imekwisha mshinda na Tamaa ya Mali imemnyemelea na Shatani kamkamata sawa sawa!
 
Kaka hiyo ni muvu ya kisiasa.Ili wanaopinga mahakama ya kadhi waichukie ukawa,itachorwa picha kuaminisha watu kama ukawa wangekuwepo suala hilo lisingepita.hapo ndipo ukawa wanaweza kupoteza wafuasi.Lakini bado mchakato kaka tusubri kura ya maoni,ikubukwe nafasi ya kampeni itakua sawa kwa kila mtu

Anyesubiri kura ya maoni ameliwa maana kura hiyo inasimamiwa na tume ya uchaguzi - hii ya sasa isiyo huru, inayotekeleza matakwa ya ccm!
 
Naziona hasira na hofu zawatoto wa michepuko juu ya mahakama ya kadhi..mi sioni ubaya wa hii mahakama kama kweli itadeal na mambo hayo matatu tuu.yaani ndoa,mirathi nann sijui....ila habari zaku pigana mawe,.kukatana mikono tuwaachie waarabu jamani😎😎
 
Ogopa sana suala ambalo si rahisi kulibadilisha, ukaliingiza kwenye katiba. Ukisharuhusu mahakama ya kadhi kwenye katiba, likileta shida huko mbele utaliondoaje? Unadhani hao watakaokuwa tayari wamejikita katika mahusiano ya ki-kadhi watakubali mliondoe?
Kama suala la serikali 2 kulirekebisha kuiwa serikali 3 imekuwa taabu wakati liko wazi, je hilo la kadhi ambalo ni la kiimani itakuwaje. Si rahisi kubadili imani za watu
 
Naziona hasira na hofu zawatoto wa michepuko juu ya mahakama ya kadhi..mi sioni ubaya wa hii mahakama kama kweli itadeal na mambo hayo matatu tuu.yaani ndoa,mirathi nann sijui....ila habari zaku pigana mawe,.kukatana mikono tuwaachie waarabu jamani😎😎
Umesahau islamic courts za Somalia!
 
Umesema sahihi. Hatuhitaji kuishi maisha ya kinafiki na hasa unafiki huo unapopelekea umwagaji damu. Kuna watu wanasema hakuna tatizo Tanzania kwa kuwa kuna wazee watawaonya. Hao wazee wakusikilizwa wako wapi? Huko kulikooza na mizoga ya wanadamu hawana hata mtu wa kuwazika hapakuwa na wazee? Iraq, Iran, Syria kabla hawajaingiza ushetani huu kwenye seriakli zilikuwa nchi nzuri sana. Watoto walienda shule wakicheza kwenye mwanga wa matumaini. Wazazi waliona kesho ya watoto wao kupitia nuru ya jua la jioni. Usiku walilala usingizi mwema wakiota ndoto za faraja na uzima. Baada ya kuruhusu unafiki na kuingiza masuala ya dini hii kwenye serikali, ndipo ukawa mwanzo wa laana inayofanya anga la nchi za kiarabu ligubikwe na giza lililojaa miavuli myeusi inayopeperushwa na viumbe wenye kutisha. Wana sura na maumbile ya kibinadamu usoni lakini mifupa yao na maumbile wanayofunika yasionekane ni ya viumbe wasiotokana na jamii ya binadamu. Nina rafiki zangu wako Pasktani na Afghan, wananiambia wanaishi kwa majuto na lawama ziko kwa wazazi wao walioshindwa kusimamia utaarabu na kupelekea waishi jehanum wakiwa bado duniani. Hakuna mtu mwenye amani hata mmoja.
Mkuu! War is not desirable but sometimes necessary. We must protect those who suffer from unjust aggresion!
 
Back
Top Bottom