Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) yatangaza hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) yatangaza hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Wakuu,

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetoa hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, na waziri wa zamani wa ulinzi, Yoav Gallant, kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.

Uamuzi huu unamaanisha kwamba nchi 124 wanachama wa ICC zinapaswa kuwakamata Netanyahu na Gallant watakapokanyaga katika maeneo yao.

Soma pia: Pamoja na “Arrest Warrant” ya Mahakama ya ICC, Putin atua Mongolia kibabe

Mahakama hiyo pia ilidai kuwa walikusudia na walijua kwamba Netanyahu na Gallav waliwanyima raia wa Gaza chakula, maji, dawa, vifaa vya matibabu, mafuta, na umeme kwa makusudi.

Netanyahu alikataa madai hayo akiyaita “ya kipuuzi na ya uwongo” na akasema ni “upotoshaji.”

Israel pia imepinga mamlaka ya ICC kwa kusema kuwa nchi nyingine za kidemokrasia hazijawahi kutendewa kwa njia ya upendeleo mbaya kama hiyo, huku ikisisitiza kwamba inaheshimu utawala wa sheria.

Aidha, ICC pia imetoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa Hamas, Mohammed Deif, kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifunime wa kivita.

Hata hivyo, Israel ilidai Agosti kwamba ilimuua Deif katika shambulio la anga lililofanyika Gaza mwezi mmoja kabla.
nimewasikiliza al jazeera ndio habari pekee wanaiongelea leo. ajabu yake, hawajui kuwa hata PUTIN aliwahi kupewa arrest warrant, what happened then? viongozi kibao tu hapa duniani walishawahi kupewa arrest warrant. ICC haina meno, ni kibogoyo, inategemea netanyahu na mwenzake wakitembelea nchi wanachama wakamatwe na hizo nchi, ni nchi gani netanyahu alishawahi kutembelea kwa miaka 20 iliyopita, utaona ni Marekani peke yake. hawana shida kutembelea nchi zingine. na Israel sio member state wa ICC, so is the US and Russia.

kitu kingine, al jazeera huita vita ya Gaza ni GENOCIDE, wajiulize, kwanini ICC kwenye arrest warrant yake hajataja kosa la genocide? wamesema wanakamatwa kwa WAR CRIMES kwa minajili ya kuzuia chakula kuwafikia watu wa Gaza. jambo ambalo Netanyahu na mwezake hata wangekamatwa, wana justification, hata al jazeera na dunia nzima na UN yenyewe imeona kuwa kule GAZA misaada inayoenda ilikuwa inaishia kwa adui ambaye Israel anapigana nao, hata juzi waliteka malori mengi, kuna ushahidi mwingi hamas walishateka malori ya chakula, kwa hiyo it is justifiable kwa ISrael kuzuia chakula kwenda kwa adui. pamoja na kwamba hajazuia kabisa, amekuwa akiruhusu malori in a limited kwa uangalizi maalumu, hivyo hawawezi kuprove kosa hilo dhidi ya netanyahu na mwenzake kama wangekamatwa kweli.

swahi ni, nani wa kumkamata? Marekani na nchi yeyote ya ulaya hawawezi, na Netanyahu na mwenzake hawana interest kutembelea nchi zingine hizo, na inawezekana hawajawahi kutembelea, wakafanye nini? hivyo arrest warrent hii kwa mtu mwenye akili anajua ni butu, haina meno na wanajifurahisha tu.
 
Gaidi kwako, kwangu ndiye mchambuzi bora wa siasa za Kimataifa.
Namkubali na kumheshimu sana.
marwan ni Mpalestina anayeishi Ufaransa na nchi kadhaa za ulaya,ni mkimbizi. hawezi kuwa impartial hata siku moja, na al jazeera huwa wanamtumia kama silaha kuwapa moyo watu kama wewe waone kuna ushindi unakuja. NI marwan aliyesema mbele ya tv kwamba Israel haiwezi kuingia Gaza kwamba haina uwezo, ni yeye alikuwa anawaambia wa hezbollah wana jeshi bora na alikuwa na imani na viongozi wa hezbollah ambao wote sasaivi wanaliwa na funza ardhini huko. kama unamsikiliza basi unafanana naye upungufu wa akili.
 
Usinipangie wa kumsikiliza tafadhali, namsikiliza na kila anachosema nakikubali 100%

Yani niache kumsikiliza mtaalamu wa siasa za dunia, akili kubwa Marwan Bishara nikusikilize wewe mnywa mataputapu?
 
Usinipangie wa kumsikiliza tafadhali, namsikiliza na kila anachosema nakikubali 100/%

Yani niache kumsikiliza mtaalamu wa siasa za dunia, akili kubwa Marwan Bishara nikusikilize wewe mnywa mataputapu?
hakuna anayekupangia, unafaa kumsikiliza kwa sababu akili zenu zinafanana.
 
Unless kama hufuatilii international news, netanyahu hataki vita iishe kwa sababu zake binafsi wala siyo october 7, hata wananchi wa israel wanalijua hilo , na hata biden alihojiwa akasema wana kila sababu netanyahu ana personal interest na kuendelea kwa vita, tumieni akilo basi msiwe mnadanganyika kiurahisi hivyo

Hizo sababu zake binafsi ni zipi mkuu?
 
Wakuu,

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetoa hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, na waziri wa zamani wa ulinzi, Yoav Gallant, kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.

Uamuzi huu unamaanisha kwamba nchi 124 wanachama wa ICC zinapaswa kuwakamata Netanyahu na Gallant watakapokanyaga katika maeneo yao.

Soma pia: Pamoja na “Arrest Warrant” ya Mahakama ya ICC, Putin atua Mongolia kibabe

Mahakama hiyo pia ilidai kuwa walikusudia na walijua kwamba Netanyahu na Gallav waliwanyima raia wa Gaza chakula, maji, dawa, vifaa vya matibabu, mafuta, na umeme kwa makusudi.

Netanyahu alikataa madai hayo akiyaita “ya kipuuzi na ya uwongo” na akasema ni “upotoshaji.”

Israel pia imepinga mamlaka ya ICC kwa kusema kuwa nchi nyingine za kidemokrasia hazijawahi kutendewa kwa njia ya upendeleo mbaya kama hiyo, huku ikisisitiza kwamba inaheshimu utawala wa sheria.

Aidha, ICC pia imetoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa Hamas, Mohammed Deif, kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.

Hata hivyo, Israel ilidai Agosti kwamba ilimuua Deif katika shambulio la anga lililofanyika Gaza mwezi mmoja kabla.
Haya ndo matokeo ya kushabikia vita na kushiriki kutendea unyama wanadamu ambao siyo nasaba yao.

Nakubaliana na HAKI ya Israel kujilinda. Lakini kujipa haki ya kuua, kuchinja na kuwatendea unyama wanadamu wengine kwa kigezo cha vita ya kihayawani ni kosa baya sana kwa ubinadamu.

HAMAS wanastahili kushtakiwa kwa kufanya ugaidi dhidi ya Israel. Lakini Israel nayo inastahiki kushtakiwa kufanya ugaidi dhidi ya Palestina na majirani zake.
 
Back
Top Bottom