Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) yatangaza hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) yatangaza hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Wakuu,

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetoa hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, na waziri wa zamani wa ulinzi, Yoav Gallant, kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.

Uamuzi huu unamaanisha kwamba nchi 124 wanachama wa ICC zinapaswa kuwakamata Netanyahu na Gallant watakapokanyaga katika maeneo yao.

Soma pia: Pamoja na “Arrest Warrant” ya Mahakama ya ICC, Putin atua Mongolia kibabe

Mahakama hiyo pia ilidai kuwa walikusudia na walijua kwamba Netanyahu na Gallav waliwanyima raia wa Gaza chakula, maji, dawa, vifaa vya matibabu, mafuta, na umeme kwa makusudi.

Netanyahu alikataa madai hayo akiyaita “ya kipuuzi na ya uwongo” na akasema ni “upotoshaji.”

Israel pia imepinga mamlaka ya ICC kwa kusema kuwa nchi nyingine za kidemokrasia hazijawahi kutendewa kwa njia ya upendeleo mbaya kama hiyo, huku ikisisitiza kwamba inaheshimu utawala wa sheria.

Aidha, ICC pia imetoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa Hamas, Mohammed Deif, kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.

Hata hivyo, Israel ilidai Agosti kwamba ilimuua Deif katika shambulio la anga lililofanyika Gaza mwezi mmoja kabla.
Sio Ayatollah but Netanyahu..
 
Hawa wapo tayari kumkamata ikiwemo germany ,uingereza ,spain na nchi nyingine 92
Hata wakati icc inaanza uchunguzi na kupokea vitisho kutoka kwa marekani na israel wote mlisema icc haitofanya kitu, ila viongozi wachache wa ulaya ambao walitamka hadharani kwamba wanaheshimu uhuru na utendaji wa icc
Si mpaka aende huko?
 
Sasa mchungaji yesu si aliwaambia mtu akikupiga Kofi shavu la kushoto
We mgeuzie na lakulia ,,
Mbona hamfati maandiko ya kitabu chenu .,
Wayahudi wana fata TORATI ya Musa Jino kwa jino, nako to nako, akuanzae mmalize.
Ndio hivyo sheikh.
NB, ukiandika yesu kama ni yule wa Nazareth anza na herufi kubwa yaani Yesu.
 
Unless kama hufuatilii international news, netanyahu hataki vita iishe kwa sababu zake binafsi wala siyo october 7, hata wananchi wa israel wanalijua hilo , na hata biden alihojiwa akasema wana kila sababu netanyahu ana personal interest na kuendelea kwa vita, tumieni akilo basi msiwe mnadanganyika kiurahisi hivyo
Uvamie nchi ya watu ,uue watu, ushangilie allahu akbar, wakutandike ,ujichanganye na raia ,utegemee kusiwe na collateral damage?
Hamas waliutaka wameupata!
 
Uvamie nchi ya watu ,uue watu, ushangilie allahu akbar, wakutandike ,ujichanganye na raia ,utegemee kusiwe na collateral damage?
Hamas waliutaka wameupata!
Na netanyahu kautaka sasahivi amekuwa kibaka kama vibaka wengine tu pamoja na back up ya marekani ila dunia imeshamkataa,ukiachana na mawaziri wake wawili wa ulinzi ambao walimchana wazi kama jamaa hajui anachofanya
 
Haya pata maoni ya biden na waziri wa vita aliyeamua kuachana na netanyahu kwa kujiuzulu baada ya kuona jamaa haelewi anachokifanya
Nikisoma post zako huko nyuma namna ulivyopoa siku hizi namheshimu sana na kumuogopa Myahudi
 
Na netanyahu kautaka sasahivi amekuwa kibaka kama vibaka wengine tu pamoja na back up ya marekani ila dunia imeshamkataa,ukiachana na mawaziri wake wawili wa ulinzi ambao walimchana wazi kama jamaa hajui anachofanya
Hakuna kitu Netanyahu atafanywa especially kipindi hiki cha mzee Trump.
Jamaa akiingia ofisini anatoa zuio la silaha tunahamia Yemen baada ya kufuta hizbullah kwenye uso wa dunia.
Myahudi ni mtu wa kisasi hakopeshi.
Jamaa hawakujua kuchagua vita
 
Inaonyesha mweupe sana kwenye anga za kimataifa ,trump huwa hataki vita ,na katika historia ya marekani yeye ndio aliondoa wanajeshi wa marekani afghanistan na kwingineko middle east,
Akiingia trump hakutokuwa na vita ukraine wala gaza na netanyahu analijua hilo
 
M
Mahakama ya kipuuzi. Huwezi kutoa hati ya mashtaka kwa kiongozi aliengoza kwa mafanikio makubwa operation tokomeza ugaidi.
Kumbuka hamas ndio walianza ugaidi Oct 7

Ilikuwa aibu adi leo kutotolewa iyo Hati mashilika yote ya haki za Binadamu zinashtumu Netanyahu na wenzake kwa kufanya unyama mkubwa ktk karne 21 lkn taasisi nyingi nilikuwa nimepigwa na Butwaa vip adi leo sheria aichukui mkondo. Hii itasaidia na kuna uwezekano yule mwendesha mashtaka ana uraia wa UK na chama kipya kilichoingia mamlakani PM wake alisema wao sasa awatozuia kutolewa ile Hati wataongea na KHAN kumbe yule Muindi alikuwa PM ndio alikuwa anazuia HATI isitolewe. Kenge yule
Hao ni wapumbavu, Waliyofanya Hamas Oktoba 7 sio unyama?
 
Okay sawa.

Lakini Israel kwenye suala hili ilianza kuchokozwa.
Endapo kama mashambulizi kwa Waisraeli ya 7 Oktoba, 2023 yasingefanyika naamini kwa dhati kabisa balaa hilo kwa Wapalestina lisingetokea
Kwani unadhani kabla ya October 7 walikuwa hawauliwi? Sema siyo kwa wingi kama hivi. Mateso walikuwa nayo, October 7 ilichofanya ni kuongezeka kwa idadi kubwa ya vifo na uharibifu mkubwa zaidi. Na pia dunia kufuatilia zaidi.
 
Unless kama hufuatilii international news, netanyahu hataki vita iishe kwa sababu zake binafsi wala siyo october 7, hata wananchi wa israel wanalijua hilo , na hata biden alihojiwa akasema wana kila sababu netanyahu ana personal interest na kuendelea kwa vita, tumieni akilo basi msiwe mnadanganyika kiurahisi hivyo
Netanyahu kweli hautaki vita iishe
 
Unless kama hufuatilii international news, netanyahu hataki vita iishe kwa sababu zake binafsi wala siyo october 7, hata wananchi wa israel wanalijua hilo , na hata biden alihojiwa akasema wana kila sababu netanyahu ana personal interest na kuendelea kwa vita, tumieni akilo basi msiwe mnadanganyika kiurahisi hivyo
Mateka wako wapi?

Anaachaje vita huku magaidi bado wana mateka wa Kiyahudi
 
nimewasikiliza al jazeera ndio habari pekee wanaiongelea leo. ajabu yake, hawajui kuwa hata PUTIN aliwahi kupewa arrest warrant, what happened then? viongozi kibao tu hapa duniani walishawahi kupewa arrest warrant. ICC haina meno, ni kibogoyo, inategemea netanyahu na mwenzake wakitembelea nchi wanachama wakamatwe na hizo nchi, ni nchi gani netanyahu alishawahi kutembelea kwa miaka 20 iliyopita, utaona ni Marekani peke yake. hawana shida kutembelea nchi zingine. na Israel sio member state wa ICC, so is the US and Russia.

kitu kingine, al jazeera huita vita ya Gaza ni GENOCIDE, wajiulize, kwanini ICC kwenye arrest warrant yake hajataja kosa la genocide? wamesema wanakamatwa kwa WAR CRIMES kwa minajili ya kuzuia chakula kuwafikia watu wa Gaza. jambo ambalo Netanyahu na mwezake hata wangekamatwa, wana justification, hata al jazeera na dunia nzima na UN yenyewe imeona kuwa kule GAZA misaada inayoenda ilikuwa inaishia kwa adui ambaye Israel anapigana nao, hata juzi waliteka malori mengi, kuna ushahidi mwingi hamas walishateka malori ya chakula, kwa hiyo it is justifiable kwa ISrael kuzuia chakula kwenda kwa adui. pamoja na kwamba hajazuia kabisa, amekuwa akiruhusu malori in a limited kwa uangalizi maalumu, hivyo hawawezi kuprove kosa hilo dhidi ya netanyahu na mwenzake kama wangekamatwa kweli.

swahi ni, nani wa kumkamata? Marekani na nchi yeyote ya ulaya hawawezi, na Netanyahu na mwenzake hawana interest kutembelea nchi zingine hizo, na inawezekana hawajawahi kutembelea, wakafanye nini? hivyo arrest warrent hii kwa mtu mwenye akili anajua ni butu, haina meno na wanajifurahisha tu.
Sasa kinacho kuliza ni Nini?
 
Mahakama ya kipuuzi. Huwezi kutoa hati ya mashtaka kwa kiongozi aliengoza kwa mafanikio makubwa operation tokomeza ugaidi.
Kumbuka hamas ndio walianza ugaidi Oct 7

Bibi likamatwe tu likatolewe mavi korokoroni
 
Back
Top Bottom