Wakuu,
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetoa hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, na waziri wa zamani wa ulinzi, Yoav Gallant, kwa makosa ya
uhalifu dhidi ya ubinadamu na
uhalifu wa kivita.
Uamuzi huu unamaanisha kwamba nchi 124 wanachama wa ICC zinapaswa kuwakamata Netanyahu na Gallant watakapokanyaga katika maeneo yao.
Soma pia:
Pamoja na “Arrest Warrant” ya Mahakama ya ICC, Putin atua Mongolia kibabe
Mahakama hiyo pia ilidai kuwa walikusudia na walijua kwamba Netanyahu na Gallav waliwanyima raia wa Gaza chakula, maji, dawa, vifaa vya matibabu, mafuta, na umeme kwa makusudi.
Netanyahu alikataa madai hayo akiyaita “ya kipuuzi na ya uwongo” na akasema ni “upotoshaji.”
Israel pia imepinga mamlaka ya ICC kwa kusema kuwa nchi nyingine za kidemokrasia hazijawahi kutendewa kwa njia ya upendeleo mbaya kama hiyo, huku ikisisitiza kwamba inaheshimu utawala wa sheria.
Aidha, ICC pia imetoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa Hamas, Mohammed Deif, kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.
Hata hivyo, Israel ilidai Agosti kwamba ilimuua Deif katika shambulio la anga lililofanyika Gaza mwezi mmoja kabla.