Mahakama ya Kisutu imewatia hatiani Viongozi wa CHADEMA na kuwahukumu kulipa faini ya Tsh. Milioni 350 au kwenda jela, Wapelekwa Segerea

Mahakama ya Kisutu imewatia hatiani Viongozi wa CHADEMA na kuwahukumu kulipa faini ya Tsh. Milioni 350 au kwenda jela, Wapelekwa Segerea

Anabatiza kwa Moto tuliambiwa na mzee makamba
Makamba siku anaitwa kubatizwa akakimbilia kuandika barua ya kujitoa CCM! Kaambiwa mzee mambo hayaendagi hivyo! Tulia ubatizwe! Siku ya kubatizwa alilia na kutokwa na machozi na makamasi mpaka kamati ya nidhamu ikamuhurumia na kumfutia makosa yake yote! Sasa nenda kwa makamba atawapa ushauri mzuri
 
Makamba siku anaitwa kubatizwa akakimbilia kuandika barua ya kujitoa CCM! Kaambiwa mzee mambo hayaendagi hivyo! Tulia ubatizwe! Siku ya kubatizwa alilia na kutokwa na machozi na makamasi mpaka kamati ya nidhamu ikamuhurumia na kumfutia makosa yake yote! Sasa nenda kwa makamba atawapa ushauri mzuri
Chizi umelogwa tena?Duh!walimwengu kweli hawana huruma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo ndio hukumu juu ya mashitaka ya viongozi wa CHADEMA kwa kufanya maandamano kudai haki yao ya mawakala kupewa barua za utambulisho kwa mawakala na kusabisha kifo cha Aquilina.

#NipasheHabari Leo ni hukumu, ikiwa inatimu miaka miwili na siku tano, tangu kuanza kwa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, na viongozi wanane waandamizi wa chama hicho.

=====

Hatima kina Mbowe kortini leo
3 minutes

Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka 13, wakituhumiwa kwa uchochezi, katika kesi iliyoanza kusilikizwa Machi 7, 2018 na Hakimu ambaye sasa ni Jaji, Wilbard Mashauri.

Mbali na Mbowe, wengine ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji na Katibu Mkuu wa sasa, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu visiwani, Salum Mwalimu na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na mbunge, Halima Mdee.

Wabunge wengine ni Esther Matiko, Esther Bulaya, Mchungaji Peter Msigwa na John Heche. Katika kesi hiyo, baadhi ya washtakiwa waliwekwa mahabusu kwa miezi mitatu kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.

Machi 14 mwaka jana, jalada hilo lilihamishiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, baada ya Hakimu Mashauri kupandishwa cheo na kuwa Jaji.

Hakimu Simba alitoa mwongozo kwa mawakili wa pande zote mbili ili kuzuia ucheleweshaji wa kusikilizwa kesi hiyo.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Februari Mosi na 16, mwaka 2018, wakiwa Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwa pamoja walikula njama na wengine ambao hawapo mahakamani kwa kutenda kosa la jinai na kuendelea na mkusanyiko isivyo halali na kusababisha chuki na uchochezi wa uasi.

Inadaiwa washtakiwa wote katika tarehe hiyo wakiwa kwenye barabara hiyo, kwa pamoja wakiwa wamekusanyika wao sita na wenzao 12 ambao hawako mahakamani, wakiwa katika maandamano au mkusanyiko wenye vurugu na kutozingatia amri ya kusitisha maandamano iliyotolewa na askari, waligoma kutawanyika na kuendelea na mkusanyiko huo wa vurugu uliosababisha kifo cha Akwilina Akwiline na majeraha kwa askari wawili.

Katika shtaka ambalo linamkabili Heche peke yake, inadaiwa Februari 16 mwaka huo, katika Viwanja vya Buibui Kinondoni katika mkutano wa hadhara, alitoa maneno ya chuki dhidi ya serikali.

Inadaiwa alisema "kesho patachimbika, upumbavu ambao unafanywa kwenye nchi hii... wizi unaofanywa na serikali ya awamu ya tano, watu wanapotea... watu wanauawa, wanaokotwa katika mitaro, lazima ukome", maneno ambayo yanadaiwa kusababisha chuki ya wananchi dhidi ya serikali.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi. ulifunga ushahidii ukiwa na mashahidi wanane huku Upande wa Utetezi uliongozwa na Wakili Peter Kibatala, ukiita mashahidi watano.

Hati ya mashtaka ya awali ilikuwa na mashtaka 12 yakiwamo ya kufanya mkusanyiko usio halali, lakini hati mpya iliyopo ina mashtaka 13 likiwamo la kufanya maandamano yasiyo halali wakiwa na lengo la kuvamia Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni.

Chanzo: Nipashe
Updates wapi
 
Mungu asimamie haki itendeke!

Wakati huu wa Kwaresma tunajikumbusha mengi kuhusu Wanasheria na yule Yuda aliyesaliti PIA Petro aliyekana!
Wanasheria ndio watu pekee walikua na uwezo na ujasiri wa kumpa YESU changamoto ya maswali.
 
acha ushabiki wa kijinga wewe mkurugenzi ndiye aliye andamana? hao wasio na akili timamu na akili za kushikiwa ndiyo chanzo wasingeandamana nani angekurupuka kupiga risasi hovyo hivi unaakilikweli mpaka unasema mkurugenzi? naona unafikiri kwa kutumia makalio
Punguza usenge wewe,usijione una akili kuliko wengine ,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu mlisema hukum inatolewa saa Saba ila mpaka sasa updates sizion au Ni saa Saba ya usiku?
 
Back
Top Bottom