Wakati Hakimu Mkazi Mfawidhi, Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akisoma hukumu ya viongozi 12 wa Cahdema na mmoja wa CCM (Mashinji) wanaokabiliwa na mashktaka ya uchochezi, Jeshi la Polisi limetumia nguvu kuwafurusha wafuasi wa Chadema waliokuwa wamekusanyika mahakamani hapo kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo.
Polisi waliagiza wafuasi wote wa Chadema kuondoka kwenye viunga vya mahakama hiyo, lakini waliendelea kukaa wakidai hawajavunja sheria yoyote kwenda kusikiliza hukumu ya viongozi wao. Hata hivyo polisi walitoa amri ya kutawanyika kwa hiari vinginevyo watatumia nguvu. Wafuasi hao walikataa kutawanyika na kuimba kwa hisia "Mkitaka mtuue, mtuue"
_
Baadae polisi wenye silaha za moto, wakisindikizwa na mbwa waliwavamia wafuasi hao kwa kipigo na kuwatawanya wakati hukumu ikiendelea kusomwa ndani ya mahamkama hiyo.!