Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,281
Mahakama ya Mwanzo Buguruni imevunja ndoa ya Wanandoa Raymond Kulaya (44) na Magreth Silaeli (37) waliotengana kwa miaka 10 baada ya kukubaliana kila Mtu akatafute Watoto ‘anapopajua’ baada ya kuishi miaka mitano bila kupata Mtoto, kwa sasa Magreth amepata Watoto wanne na Mwanaume mwingine.
Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Matrona Luanda ambapo amesema Mahakama hiyo iliangalia viini vikuu vitatu ikiwemo kama ndoa ya wawili hao ni halali baada ya kutengana tangu mwaka 2011.
Katika kesi hiyo Magreth aliiomba Mahakama itoe hati ya talaka, ili aolewe na Mwanaume anayeishi nae sasa ambaye amezaa nae, baada ya kutengana kwa muda na Kulaya, wawili hao walifunga ndoa ya Kikristo mwaka 2006 mkoani Kilimanjaro na waliishi pamoja kwa miaka mitano na kudai wakati anaolewa na Kulaya alimkuta tayari na Watoto wawili, lakini katika kipindi chote walichoishi pamoja hawakubahatika kupata watoto.
Alidai mwaka 2011 Mume wake alimueleza kuwa wamekaa kwa muda mrefu bila ya kuwa na Watoto na kumwomba watengane ili kila Mtu aende akatafute Watoto na kusema katika kipindi walichoishi pamoja, Familia ya Ndugu wa Mwanaume ilikuwa inawasumbua kuhusiana na Watoto na kuwasababishia kukosa raha.
Magreth alidai yeye na Kulaya walitengana kwa makubaliano hawakuwahi kuwa na ugomvi na sababu kubwa ya kutengana ilikuwa kukaa muda wa miaka mitano bila ya kupata Mtoto licha ya kwamba Mwanaume alikuwa na Watoto watatu kabla ya kumuoa Magreth.
Pia Soma >> Aeleza walivyokubaliana na mume wake kutafuta watoto nje ya ndoa