Mahakama ya Rufani yabariki mtu binafsi kufungua mashitaka yanayohusu "Haki za Msingi na Majukumu" ( Basic Rights and Duties Enforcement )

Mahakama ya Rufani yabariki mtu binafsi kufungua mashitaka yanayohusu "Haki za Msingi na Majukumu" ( Basic Rights and Duties Enforcement )

Bunge lisipofanya hivyo mahakama imesema ikifika muda huo hawajafanya marekebisho ni kuwa kifungu hicho kitakuwa kimejifuta automatically in the ooks of our laws!
Kwenye checks and balances hakuna kusubiriana! Bunge wakichelewa ndiyo mahakama itakuwa imerekebisha hivyo!
 
Hapo mahakama ipo huru ee?
Lakini ikitoa hukumu tofauti na matarajio au mkiangukia pua, inakuwa mhimili wa mahakama unaingiliwa!
Na wewe acha upovu hauoni kama hiyo sheria ilikuwa hatari kwa hao Watu wa Mahakama wenyewe kwa kubebeshwa jinai zote za Mhimili mwingine? Acha sheria itenguliwe kila mmoja abebe dhambi zake mwenyewe,hakuna Mhimili wa Uungu Nchi hii Tanzania ni ya Wote.
 
Hapo mahakama ipo huru ee?
Lakini ikitoa hukumu tofauti na matarajio au mkiangukia pua, inakuwa mhimili wa mahakama unaingiliwa!
Huelewi maana ya uhuru wa mahakama wewe panzi. Mhimili unaingiliwa pale inapoonekana kwa makusudi kabisa sheria inapindishwa, Watu wana uwezo wa kuona pale haki inapopindishwa.Ndiyo maana Onesmo ole Ngurumwa alipinga hukumu.
 
Finally, we direct that, within 12 (twelve) months from the date
of this judgment, sections 6 and 7 of
the Written Laws (Miscellaneous
Amendments) (No. 3) Act, 2020, which amended section 4 of the BRADEA,
be repealed by the Parliament of the United Republic of Tanzania; failure of
which, the amendment under consideration in that Act shall have no legal
force. We make no order as to costs.
DATED at DAR ES SALAAM this 12th day of June, 2025.
M. C. LEVIRA
JUSTICE OF APPEAL
S. M. RUMANYIKA
JUSTICE OF APPEAL
P. J. NGWEMBE
JUSTICE OF APPEAL
Onesmo Olengurumwa vs Attorney General (Civil Appeal No. 134 of 2022) [2025] TZCA 587 (13 June 2025)

13 May 2025
MAWAKILI WAELEZEA KIINI CHA KESI HIYO YA KIHISTORIA YA KIKATIBA KUPELEKWA HADI MAHAKAMA YA RUFAA TANZANIA, AMBAYO NDIYO MAHAKAMA YA JUU KABISA

View: https://m.youtube.com/watch?v=T9qEEn0Dal4

Kesi ya muda mrefu ya Rufaa ya Kiraia Na. 134 ya mwaka 2022, inayomuhusisha mtetezi maarufu wa haki za binadamu wakili Onesmo Olengurumwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, imesikilizwa leo tarehe 13 Mei 2025 saa kuanzia 3:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kuhusu Kesi hiyo mleta maombi, Wakili Onesmo Olengurumwa amesema shauri hilo la Rufaa kuhusu kesi inayopinga vikwazo vya kisheria vilivyowekwa katika kufungua kesi za maslahi kwa umma ambazo zInahitaji mtu kuonyesha kuathirika binafsi ili kufungua kesi kuhusu ukiukwaji wa haki za msingi, jambo linalodaiwa kuzuia mashauri ya maslahi ya umma, kuingilia mgawanyo wa madaraka, na kudhoofisha uwajibikaji wa viongozi wa juu wa dola, Ilifunguliwa mnamo mwaka 2022 baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali shauri hilo.

Olengurumwa amesema kesi hiyo ni ya msingi kwa maslahi ya umma kwani sheria zinazopingwa kwenye shauri hilo zinakandamiza haki za binadamu ambao wanakandamizwa na wanahitaji kutetewa, kwani si kila mmoja ana uelewa wa masuala ya sheria.

OleNgurumwa akitolea mfano wa kesi ya Rebecca Gyumi iliyolenga kuwatetea watoto wanaoozeshwa chini ya miaka 18.

Kesi hiyo imesikilizwa mbele ya jopo la Majaji wa Rufaa watatu: Mh. Levira J.A., Mh. Rumanyika J.A., na Mh. Ngwembe J.A ambapo wakili Olengurumwa amewakilishwa na jopo la wataalamu wa sheria likiongozwa na wakili Profesa mstaafu Issa Shivji, wakili mwandamizi Mpale Kaba Mpoki, Dkt. Rugemeleza Nshala, na wakili John Beniel Seka.

Kesi hiyo ilianza baada ya mnamo tarehe 19 Juni 2021, Serikali ya Tanzania ilichapisha katika gazeti la serikali Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) ya mwaka 2020, iliyofanya mabadiliko makubwa katika Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi na Wajibu kwa kuongeza vifungu vya 4(2), 4(3), 4(4), na 4(5).

Kifungu cha 4(2) kinahitaji kila mtu anayepeleka shauri Mahakama Kuu kuhusu ukiukwaji wa haki za kikatiba kuambatanisha kiapo kinachoeleza jinsi alivyoathirika binafsi.

Kifungu cha 4(3) kinabana zaidi mashauri ya maslahi ya umma kwa kutaka mlalamikaji kuonyesha maslahi binafsi kwa mujibu wa Ibara ya 30(3) ya Katiba...
 
Hili ni fundisho muhimu kuwa Katiba ni chombo cha wananchi, na kila raia ana wajibu wa kuitetea, bila woga wala masharti.

Bunge sasa fanyeni kazi bila kupunguza kitu kwenye hukumu hiyo.

Angalizo kutoka kwa msomi Fatma Karume kuhusu katiba, bado kuna kazi kubwa:

TOKA MAKTABA, MAONO :

FATMA KARUME - KATIBA YA 1977 INAMLINDA MWENYEKITI WA CCM ALIYE RAIS NA WATEULE WAKE

Wakili msomi Fatma Karume apigilia msumari mfumo wa mwenyekiti wa CCM Taifa kuteua watendaji wote kwa kupitia katiba ya 1977 iliyotungwa kwa uchu wa CCM kupokonya madaraka kutoka kwa wananchi ..

Nondo za Fatma Karume Juu ya Utendaji wa Mahakama Dhidi ya Matamko ya Kisiasa​


View: https://m.youtube.com/watch?v=K4kVdwF9vrQ
  • Mwaka 1977 katiba iliyoundwa ina uchu wa madaraka ili chama dola kongwe CCM wabaki madarakani milele
  • Majaji walioteuliwa na Kikwete, Magufuli na Samia wamejaa ambao watabaki kuwa majaji kwa miaka 20 ijayo, athari mbaya za katiba ya 1977
  • Ukweli ni huu:1. 1977 CCM ilijitungia Katiba wenyewe bila ya kuwashirikisha Wananchi.
  • 1993 CCM ilibadilisha Katiba wenyewe bila kushirikisha jamii
  • .Katiba ya Warioba ni ya mwanzo (kwanza) kushirikisha Wananchi na CCM ikaipiga BUTI.
  • Ukweli ni kuwa Katiba ya 1977 si ya WANANCHI ni ya CCM..
  • Kuna tatizo juu ya independent transcripts of the court proceedings... Tanzania hakuna... jaji anajiandikia summary yake... hili ni tatizo .. anafanya summary tu kwani haifikii kiwango cha transcripts of court proceedings..
  • Uhuru wa mahakama hauwezi kubebwa na mtu mmoja au jaji mmoja , ni jambo pana...uwepo wa wanakili wa mwenendo wa kesi yaani stenographer, bajeti ya mahakama, uteuzi wa majaji n.k kwa pamoja ndiyo huleta uhuru wa mahakama
  • Jaji Mkuu anachaguliwa na Rais. In fact Rais kamuongezea muda kinyume na matakwa ya Katiba. *Majaji wote wa Mahakama Kuu ...
  • N.k
NO REFORMS NO ELECTION 2025
 
PRESS CONFERENCE IPO WAPI ? USHINDI HUU NI KWA UMMA, NI HAKI YAO WAFAHAMISHWE

Ni wakati sasa wa Olengurumwa kuitisha press conference akiwa na jopo lake la mawakili Prof. Shivji Issa, Mr. John Seka, Dr. Rugemeleza Nshala, na Mr. Paul Kisabo kufafanua na kuupa umma habari hii njema

Hatimaye mawakili watoa ufafanuzi, juu ya maana ya ushindi wa Olengurumwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu raia yoyote kuweza kufungua kesi kwa niaba ya umma, haya kama raia huyo haguswi au kupata madhara moja kwa moja bali kutetea wanyonge wasioweza kufika Mahakamani.

Profesa anafafanua kwa mifano k

14 June 2025

BAADA YA MAAMUZI YA MAHAKAMA YA JUU KABISA TANZANIA , MAWAKILI WAONGEA


Onesmo Olengurumwa vs Attorney General (Civil Appeal No. 134 of 2022) [2025] TZCA 587 (13 June 2025)

Prof Shivji Afunguka Uamuzi wa Mahakama Kuruhusu Rais, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kushitakiwa​


View: https://m.youtube.com/watch?v=lIgUTYvrqHw
Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imetoa uamuzi muhimu, Juni 13, 2025, kwa kubatilisha vifungu vinne vya Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3 ya 2020) vilivyokuwa vikiathiri mashauri ya kikatiba ya maslahi ya umma. Kesi hii iliwasilishwa na Wakili Onesmo Olengurumwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ikiwakilishwa na jopo la mawakili wakiongozwa na Prof. Issa Shivji. Uamuzi huu ni hatua kubwa katika kulinda haki za kikatiba na kuimarisha ushiriki wa wananchi katika masuala ya haki na utawala wa sheria.
 
Back
Top Bottom