Tusome kwa pamoja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ibara ya 12 (6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria,
Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia
misingi kwamba:
(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo
kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kingenecho kinachohusika;
(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai
kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa
hilo;
(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya kitendo chohote ambacho alipokitenda hakikuwa ni
kosa chini ya sheria, na pia kwamba ni marufuku kwa
adhabu kutolewa ambayo ni kubwa kuliko adhabu
iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendwa;
(d) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu, heshima ya mtu itatunzwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi na uendeshaji wa mambo ya
jinai na katika shughuli nyinginezo ambazo mtu anakuwa chini ya ulinzi bila uhuru, au katika
kuhakikisha utekelezaji wa adhabu;
(e) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha
ZINGATIO
Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendesha shughuli zake kwa uzingativu wa Katiba ipi? Swali hili haliwahusu polisi kwa sababu wamejionesha kwa vitendo zaidi katika kuipuuza Katiba ya nchi. Msingi wao ni kutii amri wanazopewa na ccm hata kama zinakiuka katiba.
Mahakama ambayo inaendeshwa kwa kodi zetu, imekuwa ikionesha wazi bila kificho kuipuuza Katiba ya nchi hususan linapoluja suala la Haki za Binadamu pale mtuhumiwa anaponyakuliwa/ kutekwa nyara na vyombo vya dola.
Suala la utekwaji nyara akina Soka na wenzake mahakama imetoa kinga ya kisheria kws jeshi la polisi ambapo watekwa nyara walipochukuliwa na polisi na kuwazuia. Mahakama ilisema hawapo katika vituo vya polisi ingawa ushahidi kuwa waliitwa polisi ulikuwa wazi na hakuna namna inayoweza kufanikisha upatikanaji wao.
Mahakama, imeendelea kuzuia dhamana ya kijana Kombo wa Tanga kwa kosa linalofhaminika. Hukumu hiyo imetolewa bila hata kesi ya msingi kuanza kusikilizwa dhidi ya kijana huyo.
Matumizi ya mahakama kulinda maslahi ya CCM yamekuwa bayana bila kificho wala aibu. Jaji Mkuu amebariki hilo ndiyo maana hajawahi kukemea ukiukwaji wa Haki za watu wanaotuhumiwa kwa makosa yanayohusiana na siasa.
Mwabukusi,
Mdude_Nyagali na W. Slaa walikamatwa kwa amri ya IGP akiwatuhumu kwa kesi ya uhaini kwa sababu walipinga wazi wazi mkataba wa DP World. Tena walikamatwa baada ya kesi yao kupinga utaratibu wa mkataba ule. Mahakama ilishajiandaa kuwahukumu kwa kesi ya uhaini kama ilivyofanya kwa Mbowe. Amri ya kutengua maamuzi ama mwenendo wa kesi zinazoendelea hutoka JUU ndo maana tunasema kuwa nchi inapita kwenye giza na bonde la mauti.
Hitimisho
Mamlaka ya nchi haitoki tena kws Wananchi bali kutoka kwa vyombo vya usalama na Mahakama. Kama siyo kweli, njoo na hoja ya kupinga uhalisia huu